uct >> stonecroft
>> masomo ya biblia ya stonecroft
MASOMO YA BIBLIA YA STONECROFT:
Karibu katika masomo ya kibiblia ya Stonecroft, tunajitahidi kumpatia
kila mmoja neno la Mungu haijalishi ana kiwango gani katika safari
hii ya Kiroho.
Ni maombi yetu kuwa masomo haya yatatoa fursa kwako ili upate kuwezeshwa
na neno la Mungu ili uweze kuifikia jamii yako na injili ya Yesu
Kristo.
MTAZAMO:
Masomo ya biblia ya stonecroft yaliandaliwa kwa msingi wa kufuatilia
mikutano ya kuwafikia wasio fikiwa, lakini kwa sasa masomo haya
yamekuwa mpaka kuwafikiwa magerezani na makanisani, maofisini, na
maeneo mengine.
SIFA MUHIMU:
Masomo ya biblia ya Stonecroft yameandaliwa ili kufanya uinjilisti
na uanafunzi, na injili hii imejumuishwa maeneo yote ambayo Stonecroft
inafanya kazi.
Kila somo limeandaliwa maalum kabisa ili wale ambao hawamjui Mungu
nao wapate kushiriki, kwa bahati mbaya wanawake wa Africa sio wote
walio na biblia na ndio maan kulasa za biblia zimetolewa na kuacha
vipengele vya biblia tu ili kuwawezesha nao kushiriki vizuri, na
hii imeandaliwa katika mpangilio maalum wa kimatukio.
Masomo ya biblia ya Stonecroft yanaendeshwa katika nyumba, maeneo
ya kazi, makanisani, mashuleni, hata chini ya mti katika vivuri
huku Africa.
Masomo haya yameandaliwa katika, kufundisha juu ya kichwa furani
cha somo lakini hata hivyo masomo yanayo husu vitabu vya biblia
yanapatikana katika hatua ya juu.
Masomo ya biblia ya Stonecroft ni rahisi kujisomea katika makundi
madogo na hata makundi makubwa, na masomo haya yanaanzia (4-14 masomo).
Na utatu masomo 6 kwa hiyo kitabu kimoja kna masomo 18.
Masomo mengi yanakuwa na kitabu cha mwongozo wa masomo, kitabu
hiki hutumika pamoja na biblia na kila anae shiriki masomo haya.
Majadiliano ni njia mojawapo katika ukuaji wa kiroho.
USHAURI WA KUJISOMEA:
Katika maeneo mengi ya Stonecroft washiriki hutumia kitabu cha
mwongozo na biblia ya Kiswahili, ambayo hupatikana madukani, lakini
kama nilivyosema kitabu cha mkononi cha biblia kinapatikana kwa
wale wasio na biblia.
Vikundi hivi vya kujisomea hukutana mara moja kwa wiki, kwa dakika
60-90. Kama dakika ni chache kundi wanaweza kuamua kugawa masomo
haya nusu, kwa kugawana maswali na kusoma andiko.ili kutanua kazi
ya uanafunzi tunashauri kuwa vikundi lazima vitafute njia za kuongeza
washiliki ili ufanisi wake uonekane katika jamii.
MAELEZO YA MASOMO:
Kuna aina tatu za masomo ya biblia ya Stonecroft:
• Masomo ya Utangulizi wa utatu.
• Masomo ya wakristo wanao kuwa.
• Na masomo yahusuyo vichwa vya somo.
Stonecroft waanze na somo la Utangulizi, ambalo linasema “Yesu
ni nani?”, 'Mungu yukoje?’ na 'Je Roho
mtakatifu yuko wapi?' Haya ni masomo muhimu sana kwa wakristo
wapya na hata wale wa zamani maana ni muhimu hata kwa wale wanao
taka majibu ya maswali yao. Haya masomo yote yamekwisha tafsiliwa
Kiswahili na kazi bado inaendela ya kutafsiri huko Congo na Malawi
pia.
|