uct >> stonecroft
>>wakati wa masomo
WAKATI WA MASOMO:
Mara zote anza masomo haya kwa maombi, ikiwa kama kuna mtu ana
hoja basi kundi liandike hiyo hoja yake na mtaiombea katikati mwa
juma.
Ikiwa kama hitaji lake ni maombi ya dhalula basi yajumuishwe siku
hiyo hiyo.
Kumbuka kila mara uanzapo somo la “Yesu ni nani” kila
mshiriki ataandika jibu lake katika kijitabu cha kujisomea, na uwakumbushe
kuwa ni vizuri wakawa wanajaza majibu kabla ya kuja darasani.
Soma na kuwapatia washiliki maelezo katika mtindo wa uwazi huku
ukiwangalia usoni, Kiongozi huwa najifunza na kusoma na kundi lote
la washiriki, hutakiwi kuwa umeisimea sana biblia.
KIONGOZI ANAHAKIKISHA NAFASI NA SAUTI HUTUMIKA VIZURI KATIKA
KUJISOMEA:
• Kuanza na kumaliza kwa muda mzuri, kumbuka masomo haya
ya biblia yatakuwa pamoja na shule ya kuwawezesha wanawake.ambao
watahitajika kwenda kushona.
• Tumia kitabu cha kiongozi na biblia ya Kiswahili hakita
hitajika ktabu cha ziada.
• Watie moyo kila mtu ili ashiliki katika kujadili, na hakikisha
hakuna ambaye anaongea kuliko wenginehakikisha unawatia moyo unapowasihi
wajadili.
• Mtazamo wako umuelekee Yesu, na usijadili misimamo ya mafundisho
ya kikanisa,au misimamo ya kisiasa, maswali ya misimamo na mafundisho
ya makanisa yashughurikiwe maeneo mengine.
Tafuta watu ambao watakuwa viongozi wa baadae wa kundi.
Kama kiongozi ni lazima uwe mifano wa kundi, hakikisha watu hawajadili
mambo ambayo yanapaswa kuwa siri, kwa mfano mambo yale ya nyumbani.uombe
pamoja nao na kuwasihi watafute mwongozo wa Mungu.
Baada ya masomo ya Stonecroft yakina mama kufikia tamati, kila
mtu ambaye anaoneka kuwa ni kiongozi basi apitie mafunzo maalum
ya uongozi, kwa kutumia video na kitabu maalum cha uongozi, ili
waweze kupeleka stonecroft nyumbani kwao. Na katika makanisa yao.
Uwaulize washiriki wafikilie watu ambao wanaweza kuwaarika, uwahimize
waanze kuwaarika watu katika masomo, na pia waanze kuwaombea kwa
kuwataja majina yao.
Mambo muhimu ya kukumbuka.
• Iwapo huwezi kuongoza masomo haya ya biblia kwa sababu
yeyote ile, basi kiongozi aliyethibitiswa aje na kuchukua nafasi
hiyo.
• Hutakiwi kumpatia mwenzako kitabu cha mwongozo mtu yeyote
Yule hata kama uko nae katika dara moja.
|