Women's Empowerment Sponsorship Program
Contact us
    uct >>stonecroft >> mkakati wa stonecroft wa kuwawezesha wanawake

MAELEZO YA KIUTUME YA STONECROFT:

Utume wa shirika la Stonecroft ni kuwezesha wakina mama ili nao waweze kufikia jamii kwa kupitia injili ya Yesu Kristo, Kumuinua Yesu na kuhakikisha kuwa Yesu anatukuzwa kwa kuhubiri injili ya wokovu .

MAONO YA STONECROFT:
Ni kutoa mwongozo wa kimataifa katika kuwafikia wakina mama kwa ajili ya Yesu, Stonecroft inawawezesha na kuwatia moyo wakina mama ili wamuhubiri Yesu.

Uinjilist ndilo lengo letu kuu—Msingi wa kila jitihada za huduma .Utume wetu ni kuwafikia wanawake wa kila umri, na kila kabila kwa ajili ya injili ya Yesu Kristo.

Maombi ndio msingi wa kila jambo tunalo tunalotenda, Yesu alisema ,”Pasipo mimi ,hamuwezi kufanya lolote” (Yohana 15:5).

Kumtegemea Mungu, Kutafuta mwongozo wake na Baraka,ni muhimu,uanafunzi ni nyenzo muhimu katika uinjilisti, mwanamke anakuwa mfuasi wa Yesu,wakati huo huo huduma ya Stonecroft inatoa nyenzo za kumuwezesha huyu mwanamke kukua katika imani, na baada ya hapo ili aweze kuwaongoza wengine kufuata na kuwa na mawasiliano na Yesu.

Kuwawezesha wanawake ndio msingi wa stonecroft, kuwasaidia ili waweze kugundua vipawa Mungu alivyo viweka katika maisha yao. Kuwawezesha ili wawe viongozi makini,ambao wanaleta mabadiliko katika nyumba zao, vijiji, jamii, na hata nchi zao na mwisho kabisa dunia nzima.

Lengo la stonecroft na masomo yake ya biblia ni uanafunzi na uinjilisti ,haya ni masomo rahisi ambayo mtu anaweza akajifunza katika makundi madogo dogo, ili kuwatia moyo katika ukuaji wa kiroho.

Stonecroft inahubiri injili kwa kuwafikia wanawake dunia nzima. Zaidi ya watu 25,000 ambao ni watu wa kujitolea wa Stonecroft wanafanya kazi ya kuwafikia wanawake dunia nzima.

Watu wa kujitolea katika Nchi ya marekani na nchi nyingine zaidi ya 30 wanatumia vitabu vya stonecroft,ili kuhubiri injili, kwa zaidi ya miaka 75 Stonecrift wamekuwa wakitegemea maombi katika kueneza injili.

HISTORIA YA STONECROFT:


  Wezesha Kitabu cha mkononi YOU TUBE
     
Copyright ©  2019 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us