Project Hope     uct >>stonecroft >> majukumu ya kiongozi
MAJUKUMU YA KIONGOZI:

Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

Kazi ya huyu mwongozaji ni kuongoza masomo haya ya kibiblia,na wakati huo huo washiliki watakuwa na muda wakuleta mabadiliko katika jamii ya kuwaleta watu kwa Yesu, katika kundi hilo pia wanaweza kuona ni nani anafaa kuanzisha kundi jingine la kujisomea biblia, hii ni baada ya kumaliza vitabu vyote vya utatu.

Masomo ya kibiblia ya Stonecroft na mwongozo wake:

• Kuwaombea wote ambao wanakuja katika masomo ya kibiblia.

• Anza masomo haya ya biblia kwa maombi.

• Kiongozi wa masomo haya ya kiungozi, ambaye atampa majukumu ya kusimamia kikundi husika lakini yeye ataendela kupewa taarifa.

• Huyu kiongozi atahakikisha kuwa anafuata kanuni na sheria za huduma ya huduma ya Stonecroft kwa kufuata maelekezo yaliyoko katika video.

• Anandaa kundi lake kwa kupitia kitabu cha mwongozo, atawakumbusha wana kikundi juu ya umuhimu wa siri katika kundi na kundi kuelekrza maswali yao katika maandiko.

• Masomo ya kibiblia ya Stonecroft pamoja na mwongozo wake unatoa fursa kwa wanakikundi kuielewa vizuri huduma ya Stonecroft, na nafasi za kujiunga nao.

• Atateua watu ambao watajaribu kupata majibu ya maswari yahusuyo imani, majadiliano yanhimizwa juu ya nini biblia inasema na sio nini makanisa yetu yanasema au kufundisha.

• Atahakikisha anakwepa majadiliano yote yahusuyo imani na misimamo ya watu, siasa,kanisa lipi linapinga au kukubali.

SIFA ZA KUWA KIONGOZI:

1. Kiongozi lazima awe kaokoka.

2. Awe ni mtu anae itanga nguvu ya mabadiliko kupitia neno.

3. Akubaliane na sheria na kanuni za Stonecroft.

4. Anawasiliana na kufanya kazi na wenzake.

5. Ana shauku ya kuona watu wanakuwa katika maisha yao ya kiroho na kumjua Mungu.

JINSI YA KUMHOJI MTU AMBAYE UNADHANI ANAWEZA AKAWA KIONGOZI:


KUMCHAGUA KIONGOZI

Wachungaji (kutoka Africa Training Bible School) ambao walifunzwa kuwa viongozi watawatambua viongozi hao kiurahisi, kwa kuomba, kwa hekima, na watoke katika makanisa yao, hawa baada kuwateuwa hao viongozi, watawezesha katika ukuaji na kutanuka kwa masomo ya ka kibiblia ya Stonecroft.

Ni muhimu sana katika kumtafuta Yule kiongozi atakae kuwa na sifa zitakazo endana na sifa zilizotajwa katika sehemu hii.

Maelezo yafuatayo ni muhimu sana unapotaka kumteua kiongozi.

Omba kabla hujaonana na mtu husika, omba ili Bwana awapeni nyote hekima Roho ya kupambanua.

1. Pangeni muda,muwe tayari kukubaliana juu ya masomo ya kibiblia ya Stonecroft na huduma.(ikihitajika).

2. Kwa yale maeneo tu ambayo yameolodheshwa katika fomu ya maombi ya Stonecroft.

o Toa maelezo juu ya huduma ya Stonecroft—mwelekezeke akasome:
• Kijitabu cha masomo ya biblia cha Stonecroft.
• Tembelea mtandao stonecroft.org kwa maelezo zaidi.

o Mwambie akupatoe ushuhuda wake wa kumwanini Yesu tu katika wokovu wake na akupe maandiko ya biblia.

o Muulize je anaweza akajibu nini iwapo ataulizwa Yesu ni nani.

o Muulize kwanini anataka kujiunga na masomo ya kibiblia ya Stonecroft.

o Chunguza juu ya utayari wake wa kufanya kazi na watu, wa imani tofauti na tamaduni tofauti.

o Muulize juu ya mambo mengine anayo yafanya, na pia anafurahishwa na nini katika kusoma neon na kuwaongoza wengine katika kujisomea biblia.

o Hakikisha anazielewa sheria na kanuni za Stonecroft na imani.
Mtu yeyote anaetarajia kuwa kiongozi lazima aelewe Kanuni na sheria za Stonecroft, na mwongoz wake.

Majukumu ya mchungaji ambaye atakuwa Coordinator (Muunganishaji)
Uwe umekwisha pata fomu ya maombi ya mtu anaye taka kuwa kiongozi.

Kwa umakini wa hali ya juu soma fomu ya maiombi na hakikisha kuwa ushuhuda wa kiongozi uko sahihi.

Kwa maombi unapaswa kumuuliza huyo mtu maswali machache kuhusiana na Yesu, kwa mfano.

1. “Ninashauku ya kusikia safari yako na Mungu, hivi Yesu ana nafasi gani?

2. Iwapo mshiriki wa Stonecroft kakuuliza kuwa anawezaje kuwa na uhusiano na Yesu utajibu nini?

3. Unaelewa nini kuhusu injili na unawezaje kuihubiri?
Unaweza ukataka kusoma kupitia hili neon je unaweza amini?
Kitabu na mwongozo.

Panga muda wa kumfundisha muhusika kama kiongozi ,tumia nyenzo zifuatazo

Kitabu cha kibiblia cha Stonecroft cha Africa.

Iwapo hajawahi kukisoma kitabu cha Sonetabu kama “Yesu ni nani” ili wapate kuelewa ni kitu gani kinahusika katika haya masomo.

Mchungaji au mkurugenzi atakuwa na fomu za maombi katika faili lake.

Kumbuka kwamba sio kila mtu yuko tayari kwa ajili ya kuongoza, ukihisi kuwa huyo mtu hawezi akaepukana na mambo yanayoweza kuleta mkanganyiko kama vile siasa na mambo mengine ya kijamii ,basi mtie moyo kuwa yeye asiwe kiongozi bali abaki kama mshiriki tu , wa hicho kikundi.

Baada ya kumaliza haya mafunzo ya uongozi wasiliana na kiongozi wa Stonecroft wa Africa kwa barua pepe. Na mawasiliano mengine ya ziada.

Kiongozi wa Stonecroft wa kijimbo ambaye ni Mchungaji David Akondowe, atawasiliana na huduma ya Stonecroft ya Marekani ,anaweza akafanya hivi kwa barua pepe: connections@stonecroft.org.

Atuma anuani ya kiongozi iliyo kamili, namba ya simu,na barua pepe.
Nao Stonecroft wakisha pokea hayo maelezo watamkaribisha huyo kiongozi mpya kwa barua pepe, ambayo itatafsiriwa katika lugha ya eneo husika, na kuanzanzia hapo huyu kiongozi ataunganishwa katika mtandao wa watu wakujitolea na anaweza kunza kupikea barua na majarida katika barua pepe.na anaweza kutembelea mtandao wa viongozi, na kujipatia mambo mengi ya kujisomea katia mtandao wa Stonecroft Ministries website. www.stonecroft.org

Hawa viongozi wapya watatambuliwa kama viongozi kwani tunatambua mchango wa kila mmoja wetu katika kazi hii muhimu ya kuufikia ulimwengu na injili ya Yesu.

KUWAWEZESHA VIONGOZI WA STONECROFT:

Walimu waliofunzwa vizuri ni muhimu sana katika hii kazi ya kuwafundisha watu katika imanina hata wale ambao wako katika masomo ya kibiblia kwa miaka mingi.

Hawa viongozi wengi hutuma majarida mara kwa maana ili kuwa na mawasiliano na watu, hata mawasiliano ya kuhusu kongamano iwapo wapo katika skype, na mawasiliano mengine ya mtandao wa kijamii.
Hawa wakurugeni waandae mikutanio ambayo wanaweza kukutana na viongozi hawa kwa mwaka mara moja ili watiane moyo na kuweshana ili Stonecroft ipate kusonga mbele.

Mambo mengi yana shuhudiwa katika mawasiliano, kuwa na maono mamoja, na kujifunza kwa pamoja,na namna ya kujibu maswali magumu.

Kuwafundisha walimu wapya kunaweza kupangwa katika kipindi maalum kama vile,muda wa Krismass, na likizo nyingine.

Haya ni mawazo muhimu iwapo unajipanga kuwa na mafunzo ya viongozi:

• Muda maalum kwa ajili ya maombi na ushirika na Mungu.

• .Changamoto ya maandiko au maombi.na kuwatia moyo;

• Utangulizi na kushuhudia matokea chanya ya kujisomea biblia
muda wa kujifunza.: i.e. namna unavyo shuhudia inasadia kuongeza namna ya kuwafikia wengine, kuanzisha Stonecroft katika makanisa, na huu uwe muda wa kujifunza kutoka hata wkwa wengine, tuwe na kiongozi ambae anaelezea namna anavyo waalika wengine,matatizo waliyo kutana nayo.na eneo lipi walimwona Mungu akiwatetea. Hitimisha kwa maombi na kuwatia moyo.

MWONGOZO KWA KIONGOZI:

DHUMUNI:

Kuwafikia wasio fikiwa – haya masomo yanawezesha kuhubiri wokovu kwa kupitia Yesu.

Tunataka kutanua huduma ya Stonecroft kupitia makanisa 280 ambayo yana wanafunzi wake katika chuo cha Africa Training Bible School (ATBS) katika nchi za Tanzania, Malawi, Zambia na DR Congo na pia kupitia Hope Community Centre, Kampala, Uganda.
Pia tunamwamini Mungu tunaweza kujumuisha haya kupitia mradi ule wa kuwezesha wanawake Mkakati wa Stonecroft wa Kuwawezesha Wanawake (Women’s Empowerment Program) ambao mtajifunza mengi hapo baadae. Mradi huu wa kuwawezesha wanawake utatumia vitabu vya Stonecroft kuanzia vile vijitabu vya utatu, Mungu yukoje? Yesu ni nani? na Roho Mtakatifu yuko wapi?

Katika kuhakikisha kuwa tunaukuza mradi wa SWEP mafunnzo ya kiafrica, hawa wanawake watahimizwa kuwa viongozi, watatumia Video ya mafunzo ya kiafrica, na pia kitabu hiki ambacho kitawawezesha kuanzisha, Stonecroft katika nyumba zao, makanisa na hata vijiji vyao, kwa kupata ruhusa maalum kutka kwa mchungaji wao.

Uanafunzi – wakristo wapya na hata wale wa kale wanaweza kijifunza habari za Yesu na kuweza kuwa na mahusiano ya karibu na Mungu, masomo haya yanatufundisha namna ya kutumia biblia katika mazingira yetu ya kila siku, kuna vitabu vingi ambavyo navyo vitatafsiliwa katika lugha nyingine. Africa Training Bible School watatumia masomo haya kama nyenzo moja wapo za kufundishia katika mitahara yao. Kwa mfano, maisha mapya, kuishi maisha yangu, wafilipi, Yakobo, Warumi na vingine vingi.

UFAUTI:

Fautisha masomo ya kibiblia ya Stonecroft na masomo mengine ya biblia?

• Masomo haya yameandaliwa mahususi ili yatumike katika agano jipya ambalo linapatikana sana katika nchi ya Tanzania, lengo kuu ni kuihubiri injili ya Yesu Kristo, na kuwatia moyo watu ili wapate kujisomea maandiko kila siku, hatujajumuisha namba ya kila ukulasa katika biblia maana wengine wanaweza wasiwe na biblia.

• Masomo haya ni rahisi hata kw wale ambao ndio wanaanza kujisomea.

• Kumbuka kuwa kiongozi sio mwalimu wa biblia lakini wote wanasoma pamoja na washiriki wa kikundi.
.
NYENZO:

Masomo ya kibiblia ya Stonecroft hisi kuyasoma.
Kuna maeneo ambayo yamefungiwa ambayo hupaswi kuyasoma kwa sauti .

Maneno yaliyo chapishwa katika boksi unapaswa kuyasoma kwa sauti ili washiriki wapate kusikia.

Kwa mfano nucta zikifululiza (.....) inakwambia kuwa kiongozi awaruhusu washiriki wachangie kwa kuuliza maswali,kusoma biblia au kujadili somo.

Ukiona wino umekolezwa unao ambatana na nucta Tano, ina maanisha mstari wa biblia usome kwa sauti kubwa na msomaji.
Ikiwa kama kifungu kilicho nukuliwa kimeandikwwa katika maandishi ya kawaida ina maana, hakihitaji majibu au ni kirefu sana kusoma hadhatrani.

KABLA YA MASOMO YA BIBLIA
Vitu muhimu –

Unaweza ukawa kiongozi uliye thibitishwa na Stonecroft wetu kwa kujaza fomu iliyo tafsiriwa kwa Kiswahili.

Tunataka kujua kanisa lako na wadhfWe wan wako huko kanisani.
Tunataka kujiridhisha kuwa baada ya kusoma kanuni na sheria pamoja na maelezo yetu ya imani, huna wasiwasi tena nasi.

Vitu vinavyo hitajika katika kujisomea:

1. Vitabu vya utangulizi vya utatu vilivyotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili vinaweza patikana, katika makao makuu ya ATBS, Mbeya, Tanzania.

2. Vitabu vya mwongozo vinapatikana makao makuu ya ATBS, Mbeya, Tanzania.

3. Biblia ya Kiswahili inapatika 'Tanzania Bible Society', na madukani.

4. Je unaweza kuamini hili? Nacho kimetafsiriwa kwa Kiswahili kinapatikana katika makao makuu ya ATBS, Mbeya, Tanzania.

5. Kadi ya maelezo nayo imetafsiliwa inapatikana makao makuu ya ATBS, Mbeya, Tanzania.

6. Fomu ya maombi ya kiongozi nayo inapatika katika makao makuu ATBS, Mbeya, Tanzania.

Tafuta eneo zuli kwa ajili ya kujisomea biblia, labda nyumbani, kanisani, shuleni, nyumbani katika kivuli chini ya mti.


MAANDALIZI YA KIONGOZI KABLA YA MASOMO:

Hakikisha unajibu maswali yote ya kijitabu cha mwongozo kabla ya kuanza kusoma vitabu, hii itakuwezesha kuelewa watakao kuwa na wajibu wanapitia katika wakati gani kabla ya kupata majibu halisi.

• Fanya zoezi la kusoma hayo masomo kwa sauti,ikiwezekana,pigia msitali maneno muhimu utakayo ongelea katika kundi lako,masomo hayo yasizidi saa moja na nusu1 – 1 1/2 hasa pale ambapo masomo haya yanaendeshwa katika kuwezesha wakina mamam yani 'Stonecroft Women’s Empowerment Program' (SWEP) maana wanawake watahitaji kuondoka na kuanza kujifunza kushona

• Wakati huo huo wanafunzi wa SWEPwanapofurahi masomo yao,watoto wao watakuwa wakihudhulia Powerclub wakijifunza njia za Mungu kupitia Kids in Ministry International (KIMI) pamoja na watoto wengine kutoka katika mkakati wa Kids Evangelism Expolosion (Kides EE)..

• Maeneo haya kwa wakatio huu yatakuwa;
Tanzania – Africa Training Bible School (ATBS) – Mbeya, Tanzania
Uganda – Hope Community Centre, Kampala, Uganda.
Malawi – Africa Training Bible School (ATBS) – Uluwa and Vulwa, Malawi.

• Omba juu ya wale watakao kuwa wanakuja.

WAKATI WA MASOMO:

Mara zote anza masomo haya kwa maombi,ikiwa kama kuna mtu ana hoja basi kundi liandike hiyo hoja yake na mtaiombea katikati mwa juma.

Ikiwa kama hitaji lake ni maombi ya dhalula basi yajumuishwe siku hiyo hiyo.

Kumbuka kila mara uanzapo somo la “Yesu ni nani” kila mshiriki ataandika jibu lake katika kijitabu cha kujisomea, na uwakumbushe kuwa ni vizuri wakawa wanajaza majibu kabla ya kuja darasani.

Soma na kuwapatia washiliki maelezo katika mtindo wa uwazi huku ukiwangalia usoni, Kiongozi huwa najifunza na kusoma na kundi lote la washiriki, hutakiwi kuwa umeisimea sana biblia.

KIONGOZI ANAHAKIKISHA NAFASI NA SAUTI HUTUMIKA VIZURI KATIKA KUJISOMEA:

• Kuanza na kumaliza kwa muda mzuri, kumbuka masomo haya ya biblia yatakuwa pamoja na shule ya kuwawezesha wanawake.ambao watahitajika kwenda kushona.

• Tumia kitabu cha kiongozi na biblia ya Kiswahili hakita hitajika ktabu cha ziada.

• Watie moyo kila mtu ili ashiliki katika kujadili, na hakikisha hakuna ambaye anaongea kuliko wenginehakikisha unawatia moyo unapowasihi wajadili.

• Mtazamo wako umuelekee Yesu, na usijadili misimamo ya mafundisho ya kikanisa, au misimamo ya kisiasa, maswali ya misimamo na mafundisho ya makanisa yashughurikiwe maeneo mengine.

Tafuta watu ambao watakuwa viongozi wa baadae wa kundi.
Kama kiongozi ni lazima uwe mifano wa kundi, hakikisha watu hawajadili mambo ambayo yanapaswa kuwa siri, kwa mfano mambo yale ya nyumbani.uombe pamoja nao na kuwasihi watafute mwongozo wa Mungu.

Baada ya masomo ya Stonecroft yakina mama kufikia tamati, kila mtu ambaye anaoneka kuwa ni kiongozi basi apitie mafunzo maalum ya uongozi, kwa kutumia video na kitabu maalum cha uongozi, ili waweze kupeleka Stonecroft nyumbani kwao. Na katika makanisa yao.

Uwaulize washiriki wafikilie watu ambao wanaweza kuwaarika, uwahimize waanze kuwaarika watu katika masomo, na pia waanze kuwaombea kwa kuwataja majina yao.

Mambo muhimu ya kukumbuka.

• Iwapo huwezi kuongoza masomo haya ya biblia kwa sababu yeyote ile, basi kiongozi aliyethibitiswa aje na kuchukua nafasi hiyo.

• Hutakiwi kumpatia mwenzako kitabu cha mwongozo mtu yeyote Yule hata kama uko nae katika dara moja.

 
     
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us