Women's Empowerment Sponsorship Program
Contact us
    uct >> stonecroft >>  mkakati wa stonecroft wa kuwawezesha wanawake

MKAKATI WA STONECROFT WA KUWAWEZESHA WANAWAKE

(STONECROFT WOMEN’S EMPOWERMENT PROGRAM - (SWEP)
Masomo haya ya kibiblia ya stonecroft yanapangiliwa kutenda kazi pamoja na mpango wa kuwawezesha wakina mama kupitia mradi wao wa kujishonea (SWEP) huu ni ushirikiano wa mashirika mawili yani Stonecroft and United Caribbean Trust (UCT), shirika la kibarbados ambalo limesajiliwa kama shirika la huduma za kijamii.tunaamini kuwa mwanamke mwenye uwezo wa kupata elimu, na akijua haki zake, anaweza kubadirisha dunia hii.

Wakina mama ambao wanapitia mpango wa kushona wa Stonecroft watakuwa katika mafunzo kwa muda wa mwaka mmoja.

Kila wiki atakuwa akihudhuria ‘Kukutana na Mungu’ huu ni wakati wa kuomba, na tutatumia vitabu vya kujisomea vya Stonecroft vilivyo tafsiriwa katika lugha za maeneo husika.

Na pia atahudhuria dalasa la kushona nguo na mitindo,masomo ya computer, na kujifunza moringa na ufugaji wa wanyama.

US $40 kila mwezi itatumika katika kuwawezesha wanawake ambao watakuwa wakihudhuria hayo masomo, ambapo yatamsaidia katiak kupata elimu, masomo ya kazi za mikono, na vifaa vitakavyo muwezesha kuwa na mradi utakao muwezesha kujipatia kipato.

Lakini zaidi ya yoote,haya mambo yatafungua mlango ili mwanamke ajifunze uongozi kupitia masomo ya ya Stonecroft.

Na pia atapatiwa nafasi ya kumleta mtoto mmoja atakae kuwa anaingia katika mradi uitwao ‘After School Feeding Club’ ambao utatoa chakula cha kimwili na kiroho.

Ni shauku yetu katika kuwafikia wanawake wa Tanzania, Malawi, Zambia, DR Congo na Uganda, kwa kuwaonyesha upendo wa Mungu na kuwafungua kutoka katika umaskini.

Tunawashukuru Stonecroft kwa kujitoa kwao katika kuwafikia wanawake katika maeneo yaitwayo 10/40 window (wasio fikiwa).


  Wezesha Kitabu cha mkononi YOU TUBE
     
Copyright ©  2019 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us