Project Hope     home >>stonecroft>>mwongoo utakaotuongoza
Stonecroft Mwongoo Utakaotuongoza
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

MWONGOZO UTAKAOTUONGOZA KATIKA KUJIFUNZA MASOMO YA BIBLIA YA STONECROFT

LENGO:
KUWAFIKIA:
Masomo haya yanatuwezesha kupata njia ya kushirikiana kujua wokovu wa Yesu Kristo na watu wengine.kwa wale ambao wana makundi wanaombwa kualika marafiki zao, famila, wafanya kazi wenzao na pia majirani zao.

Uanafunzi: Wakristo wapya na wale waliokomaa wanaweza kusoma saaana kuhusu MUNGU na kuweza kukua naye katika uhusiano uliomzuri. Msomo haya yanatufundisha pia jinsi gani unaweza kutupia kanuni za kiBiblia katika mazingira ya kila siku.

UPEKEE:
Nini kinachofanya masomo ya stonecroft kuwa wa kipekee sana kuliko masomo mengine ya kiBiblia katika soko la mafundisho ya Biblia?

• Habari njema ya agano jipya: masomo haya yameundwa katika mtindo wa kutumia agano jipya kwa sababu kurasa zimewekwa katika vifungu vile unavyotakiwa kuvitafuta ndani ya Biblia ili kuweka urahisi kwa wasomaji wa masomo haya. Kurasa hizi zilizowekwa katika vifungu hivyo vimetoka katika Biblia ya toleo na tafsiri hizi zinakubaliwa sana na watu mbalimbali katika madhehebu tofauti tofauti.
• Masomo haya yameandikwa katika kwa mfumo ambao ni rahisi wa kwamba hata Yule ambaye ni mara yake ya kwanza kutumia Biblia basi anaweza kuyatumia vizuri tu. Na haya masomo yanaweza kutafsiriwa kwa urahisi tu sana katika ulimwengu mzima kwa kutumia lugha yeyote ile.
• Kiongozi ni mwezeshaji tu na sio mwalimu wa Biblia.

VIFAA:
Masomo ya stonecroft ya kiBiblia ni rahisi sana kusoma.

Maelezo kwa kiongozi yamefungiwa katika mistari iliyowekewa nukta nukta. Kwa hiyo hayatakiwi kusomwa kwa sauti.

Maelezo mengine yameandikwa yakiwa ndani ya viboksi yapo katika kitabu kile cha kujisomea au cha kusoma. Sehemu hii inatakiwa kusomwa kwa sauti na wale wahisika wenyewe yaani wanafunzi wa mmasomo haya.

Ukionna nukta zimeongozana namna hii (…..) inaonyeshs ya kwamba kiongozi inatakiwa aruhusu kundi ili kuweza kushiriki kwa kujibu maswali, kusma mistari ya Biblia, au kujadili maada husika.

KABLA YA MASOMO :
Vitu vichache vya muhimu:
• Uhakikiwe kuwa wewe ni kiongozi wa stonecroft kwa kukamilisha mchakato wa maombi katika Stonecroft.
• Soma malengo, na maelekezo ya masomo haya husika.
• Pata vifaa mbalimbali utakavyo taka kwa ajili ya masomo yako kutoka katika huduma hii ya Stonecroft _ (800) 525-8627.
• Vifaa vinavyohitajika katika mafunzo haya ni :
- Vitabu vya kujifunzia
- Mwongozo
- Kadi za taarifa
• Tafuta sehemu nzuri kwa ajili ya kujifunzia. Kuwa na muda wa kujifunza ukiwa upo nyumbani, ofisini, kwenye migahawa na katika sehemu mbalimbali.

KUJIANDAA KWA AJILI YA KUJIFUNZA:
• Maliza somo kwa kukamilisha kuandika majibu yako kkatika kitabu chako cha kujifunzia ,kabla ya kusomo mwongozo. Hii itakusaidiakatika kujua na kuelewa mafkirio yaw engine na jinsi ambavyo majibu yako uliyoyajibu yapo.
• Fanya mazoezi ya kusoma kwa sauti kama inawezekana. Pigia mstari maneno na vifungu ambavyo vitakusaidia katika kuelezea mbele ya kundi lako. Kumbuka muda ambao unatakiwa kwa ajili ya kusoma ujumbe wako, hii itakusaidia katika kujua muda gan uliobaki wa majadiliano katika kipindi hicho.
• Thibitisha mahali, muda na ulinzi wa watoto kama kutakuwa na uwezekano wa kufanya hivyo.
• Waombee wote wale ambao watakuwa wakihudhuria katika masomo kujifunza.

WAKATI WA KUJIFUNZA/ WAKATI WA MASOMO:
Gawa vitabu vya kujifunzia na agano jipya na pia kusanya malipo. Kusanya mapato au malipo na rudisha vile vitabu vilivyobaki wakati ulikuwa unagawa.

Anza kipindi kwa maombi. Kukiwa na mtu yeyote anayeuliza, utamruhusu kuwa aandike swali lake nyuma ya kitabu chake sehemu ya maombi ili iwe kama kumbukumbu yay ale maombi ya katikati ya wiki. Kama swali lililoulizwa linataikiwa kjibiwa kwa wakati huo liambatanishe na kulijibu wakati unaanza kipindi.

Kumbuka kuwa katika kipindi cha awali yaani cha kwanza, kila mtu ataandika majibu katika kitabu chake ha kujifunzia wakati wa kujifunza, au wakati wa masomo. Hamasiha makundi yote kusoma kabla ya kuonana ili kuweka kumbukumbu ya somo hilo.

Soma na uwakilishe taarifa katika kitabu kile cha mwongozo kwa njia ya kujadiliana, hapo ukiwa unawaangalia kwa sana wanafunzi wanachokifanya. Jifunze na soma na makundi yaliyopo; hutakiwi kuwa wewe ndio mjuaji sana wa Biblia.

Kiongozi anaseti toni na kasi ya kujifunza kwa:
• Kuanza na kumaliza kwa wakati uliopangwa.
• Kutumia mwongozo na Biblia kama vitabu vya kurejea. Vifaa vingine havitakiwi ambavyo havina maana yeyote katika kipindi hicho.
• Kuhamasiha kila mtu katika kushiriki katika majadiliano na kuangalia kuwa hakuna mtu anayetawala kundi kwa kuzunumza yeye peke yake.
• Kuweka hisia kwa Yesu Kristo, iswe kisiasa, au kimaandishi, au katika mambo ya kijamii. Kumbuka kuwa mabo ya kisiasa, mambo ya kijamii yote haya yana mazingira yake ya kuweza kuyaelezea.

Mara zote angalia wale ambao wako ndani ya kundi hilo unalowafundisha ambao hao ndio watakuwa viongozi wazuri kwa masomo ya baadae.

Kama kiongozi, kuwa wa mfano kwa wale unaowaangoza. Kataza watu kuzungumza vitu sirini, mbali na kundi lenyewe husika, omba pamoja nao na uwahamasishe katika kutafuta ushauri mzuri wa kiMungu.

Waulize wahusika wenyewe yaani wanafunzi katika kufikiria ni watu gani ambao wanaweza kuwaalika kwenye masomo mengine. Wahamasishe katika kuwaombea watu wengine kwa majina yao.

VITU MUHIMU VYA KUKUMBUSHA:
Kama huwezi kuongoza masomo kwa sababu yeyote ile, kama kuna mtu anayeweza kufanya hiyo kazi vizuri basi anaweza kufanya hiyo kazi badala yako.
Kwa taarifa zaidi kuhusu taratibu, vifaa, au au jinsi gani uanaweza kuongoza wasiliana nasi kupitia stonecroft bible studies at (800) 525-8627.

“Kesheni, simameni kimara katika imani, fanyeni kiume, mkawe hodari. Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo”
1 Wakorintho 16:13-14.

Bibliography

Enns, Paul, The Moody Handbook of Theology. Chicago: Moody Press, 1989.

Eerdmans, Wm. B., Eerdmans’ Handbook to Christian Belief. Grand Rapids: WM. B. Eerdmans Publishing Co., 1982.

Elwell, Walter, A., Evangelical Dictionary of Theology. Grand Rapids: Baker Book House, 1996.

Harrison, Everett F., Editor and Chief, Baker’s Dictionary of Theology. Grand Rapids: Baker Book House, 1960.

Hodge, Charles, Systematic Theology. Grand Rapids: Baker Book House, 1992.

McDowell, Josh. Evidence That Demands a Verdict. Arrowhead Springs, CA: Campus Crusade for Christ, International, 1972.

Moody.November-December, 1998. Chicago: Moody Bible Institute, 1998.

New Geneva Study Bible, Nashville: Thomas Nelson Publishers, 1995.

Packer, J.I., Knowing God. Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1973, 1993.

Ryrie, Charles C., Basic Theology. Wheaton: Victor Books, 1986.

Sproul, R.C., Pleasing God. Wheaton: Tyndale House Publishers, 1988.

Tozer, A.W., The Knowledge of the Holy—The Attributes of God: Their Meaning in the Christian Life. New York: Harper Collins Publisher, 1961.

Willmington, H.L., Willmington’s Guide to the Bible. Wheaton: Tyndale House, 1986

 
     
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us