Project Hope     home >>vijana wa stonecroft>>
Vijana wa Stonecroft
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

Karibu katika masomo ya kiafrica ya biblia ya Stonecroft, maelezo haya yanatokana na mtandao wa Stonecroft kwa ruhusa kutoka kwao ili kutengeneza huu mwongozo ili utumike katika kufundishia Africa, katika kitabu hiki mambo ya kitamaduni yamezingatiwa ili kuhakikisha kuwa kinakubarika katika mazingira ya kiafrica na nchi zake.

Stonecroft ni shirika la kimataifa ambalo haliko chini ya kanisa lolote.

MAELEZO YA KIUTUME YA STONECROFT:
Utume wa shirika la Stonecroft ni kuwezesha wakina mama ili nao waweze kufikia jamii kwa kupitia injili ya Yesu Kristo, Kumuinua Yesu na kuhakikisha kuwa Yesu anatukuzwa kwa kuhubiri injili ya wokovu .

MAONO YA STONECROFT:
Ni kutoa mwongozo wa kimataifa katika kuwafikia wakina mama kwa ajili ya Yesu, Stonecroft inawawezesha na kuwatia moyo wakina mama ili wamuhubiri Yesu.
Uinjilist ndilo lengo letu kuu—Msingi wa kila jitihada za huduma. Utume wetu ni kuwafikia wanawake wa kila umri, na kila kabila kwa ajili ya injili ya Yesu Kristo.

Maombi ndio msingi wa kila jambo tunalo tunalotenda, Yesu alisema, ”Pasipo mimi, hamuwezi kufanya lolote” (Yohana 15:5).

Kumtegemea Mungu, Kutafuta mwongozo wake na Baraka,ni muhimu, uanafunzi ni nyenzo muhimu katika uinjilisti, mwanamke anakuwa mfuasi wa Yesu, wakati huo huo huduma ya Stonecroft inatoa nyenzo za kumuwezesha huyu mwanamke kukua katika imani, na baada ya hapo ili aweze kuwaongoza wengine kufuata na kuwa na mawasiliano na Yesu.

Kuwawezesha wanawake ndio msingi wa stonecroft,kuwasaidia ili waweze kugundua vipawa Mungu alivyo viweka katika maisha yao.kuwawezesha ili wawe viongozi makini, ambao wanaleta mabadiliko katika nyumba zao, vijiji, jamii, na hata nchi zao na mwisho kabisa dunia nzima.

Lengo la stonecroft na masomo yake ya biblia ni uanafunzi na uinjilisti, haya ni masomo rahisi ambayo mtu anaweza akajifunza katika makundi madogo dogo, ili kuwatia moyo katika ukuaji wa kiroho.

Stonecroft inahubiri injili kwa kuwafikia wanawake dunia nzima.Zaidi ya watu 25,000 ambao ni watu wa kujitolea wa Stonecroft wanafanya kazi ya kuwafikia wanawake dunia nzima.
Watu wa kujitolea katika Nchi ya marekani na nchi nyingine zaidi ya 30 wanatumia vitabu vya stonecroft, ili kuhubiri injili.

Kwa zaidi ya miaka 75 Stonecrift wamekuwa wakitegemea maombi katika kueneza injili.

HISTORIA YA STONECROFT:
Kufikia leo hii,huduma ya Stonecroft inawafikia maelfu ya watu dunia nzima kila mwaka, lakini historia ya Stonecroft ilianza na mwanamke mmoja aitwaye— Helen Duff Baugh – mwanamke aliye na imani isio teteleka, mwanamke wa Maombi, mwanamke ambaye aliguswa sana na maisha yaw engine.

Kuanza hapo mwaka 1938, makundi kama hayo ya kiamama wafanyao biashara yalianzishwa nnchi nzima, mnamo1948, Binti Mary E. Clark, Mwanamke aliyekuwa mfanya biashara hapo kale na mmishenari, aliamua kuitikia wito wa Mungu na kujiunga Mama Baugh katika kumsaidia kwenye huduma yake ya uinjilisti ambayo ilikuwa inakuwa kwa haraka sana.

Katika mwaka 1952, Mungu kwa neema yake aliweza kuwapatia Jengo katika mji wa Kansas,Missouri, ambapo hapo ndipo palikuwa ofisi zao za kitaifa, Jengo hilo likaitwa Stonecroft, likiwa na maana ya “Nyumba ya Mwamba”. Hii ilikuwa ni ukumbusho kuwa Yesu Kristo ni Mwamba na ni jiwe kuu la msingi.

Kwa zaidi ya mika 70, Mungu kwa uaminifu amekuwa akilinda,kuwapatia mahitaji yao, na kuongoza huduma ya Stonecroft, katika tamaduni inayo badirika haraka sana, mambo mawili ni muhimu sana, kujitoa kwetu katika maombi na Uinjilisti.

Stonecroft kwa sasa wamehamia ofisi ndogo maana ofisi zao za mwanzo wameuza ili pesa za ziada wapate kuzipeleka katika uinjilisti.

UONGOZI WA STONECROFT:
Viongozi wa Stonecroft wanafanya majukumu yao katika ofisi ya kitaifa na hata kazi ambazo ziko mbali na hapo.

Lorraine Potter Kalal: Raisi

Lorraine Potter Kalal Huduma yake iliyo jawa na mafanikio, Pamoja na upendo wake wa Stonecroft na maono na historia, Yeye kama raisi hujiona kuwa ndie Mtumwa mkubwa, Lorrain anahitaji kuona kuwa huduma ya Stonecroft ikimtegemea Mungu ili kukamilisha mahitaji yote.

Doris Thompson anawasaidia wanawake kufikia maono yao na mawazo yao katika matendo, akiwa kama makamu wa Raisi, Doris anataka kuwafikia wanawake wengi zaidi katika ulimwengu huu,na anawasaidia wanawake wengi kupitia Stonecroft, na anawasaidia wale wanao jitolea kuwafikia wengine katika maeneo mengi zaidi. Anafanya kazi ya kuibadiri Stonecroft ili iweze kuwafikia watu walio katika maeneo mapya zaidi, Pia kuna watu wengi zaidi katika uongozi ambao hamuwezi kuwa na mawasiliano nao.

Huduma ya Stonecroft inatamani kuwaunganisha wanawake kwa Mungu na kwa wanawake wenzake na katika jamii zao.

Stonecroft inawatia moyo wanawake,kuwa na mawasiliano na wenzao na hata katika jamii zao, na pia kuwaalika katika masomo ya biblia katika vijiji vyao na miji yao.

Haya masomo ni rahisi kuyafuata, na pia ni makundi yanayo leta uzima wa kiroho katika maeneo mkakati wa muda mrefu katika maisha ya waumini.

Hili toleo la kiafrica litaleta matokeo mawili tofauti,la kwanza ni mkakati wa Stonecroft wa kuwafikia wasio fikiwa, na la pili ni mkakati wa Stonecroft wa masomo ya kibiblia.katika madarasa ya kujisomea biblia, mwongozo wa vitabu vya Stonecroft utatungwa ili kuwa na vikundi vya kujisomea biblia na kuwafikia wasio fikiwa, wasio amini na wanao amini, watatiwa moyo ili wajiunge katika makundi haya .makundi haya yataundwa na wanawake ambao wamemaliza kujisomea vitabu vya “Utatu” lakini hawajafikia kiwango cha kuongoza lakini wanataka kuendelea kujisomea, hili litawezesha ukuwaji na kutanuka kwa stonecroft katika bara la Africa.

Huduma ya Stonecroft inaelewa na kushukuru huduma ya mwanamke mmoja, ukimfikia mwanamke nae akakokoka basi umeweza kuifikia jamii, mume wake, watoto, marafiki, majirani, na anao fanya nao kazi.

Askofu David Akondowi, ambaye ni muwakilishi wa United Caribbean Trust’s (UCT) Tanzania na muasisi wa mafunzo ya wachungaji katika chuo kitwacho Training Bible School (ATBS) na mchungaji wa House of Freedom – Tanzania, ambapo UCT wana mradi wa kuwawezesha wanawake uitwao ‘Women's Empowerment Sewing Project’ yeye anazungumzia juu ya mithari ya Kiswahili isemayo, ’Ukimuwezesha mwanamke umeiwezesha jamii’."

Stonecroft wanawawezesha wanawake ili waweze kufikia jamii zao ki ukamilifu.

MAELEZO YA IMANI YA STONECROFT:
• Huduma ya Stonecroft inaamini katika utendaji wa kiroho,na uvuvio wa neno la Mungu,na tunaamini kuwa biblia haina kosa, inafaa kwa mafundisho na ndio yenye maamuzi ya mwisho na usemi wa mwisho.
• Tunaamini katika utatu wa Mungu – yani Mungu baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu;
• Tunaamini katika utu wa Mungu; Utu na uungu ya Yesu (Yesu na Mungu ni Mtu mmoja, Yesu Kristo ni Mungu aliyekuwa katika mwili) aliyezaliwa kwa uweza wa Roho Mtakatifu na mtu aliyekuwa bikra, yeye ni Mungu halisi na ni Mwanadamu halisi, na ni utu wa Roho mtakatifu.
• Tunaamini katika ufufuo wa Yesu kristo,—kuwa mwili wake ulifufuliwa kutoka katika wafu,sawasawa na maandiko, na pia akapaa kwenda mbinguni na kuketi katika mkono wa kuume wa Mungu baba kama wakili wa waamini.
• Tunaamini katika hali ya dhambi ya mwanadamu—kuwa kila mwanadamu anazaliwa na asili ya dhambi, na hawawezi kujiokoa wenyewe bali wanamuhitaji mkombozi ili awaokoe kutoka dhambini;
• Tunaamini katika utakaso—Kuwa Yesu alifanyika kuwa dhambi pale alipotoa dhabihu ambayo ni damu yake mwenyewe ili dunia nzima wapate msamaha wa dhambi.
• Tunaamni katia umuhimu wa kuzaliwa upya—wokovu ni kwa neema .kwa imani.na sio kwa matendo, imani iokoayo itaimalisha matendo mema katika maisha yetu.
• Tunaamini katika ufufuo halisi wa mwili wa waaminio na wasio amini.
• Tunaamini katika Baraka za umilele kwa walio amini na adhabu ya milele kwa wasio amini.
• Tunaamini katika uinjilisti wa dunia nzima,—Agizo kuu la Mungu ni kuihubiri injili ya Yesu Kristo kwa watu wote wa kila rika.
• Tunaamini juu ya ujio wa mara ya ili wa Yesu sawa sawa na maandiko.

MASOMO YA BIBLIA YA STONECROFT:
Karibu katika masomo ya kibiblia ya Stonecroft, tunajitahidi kumpatia kila mmoja neno la Mungu haijalishi ana kiwango gani katika safari hii ya Kiroho.
Ni maombi yetu kuwa masomo haya yatatoa fursa kwako ili upate kuwezeshwa na neno la Mungu ili uweze kuifikia jamii yako na injili ya Yesu Kristo.

MTAZAMO:
Masomo ya biblia ya stonecroft yaliandaliwa kwa msingi wa kufuatilia mikutano ya kuwafikia wasio fikiwa, lakini kwa sasa masomo haya yamekuwa mpaka kuwafikiwa magerezani na makanisani, maofisini, na maeneo mengine.

SIFA MUHIMU:
Masomo ya biblia ya Stonecroft yameandaliwa ili kufanya uinjilisti na uanafunzi, na injili hii imejumuishwa maeneo yote ambayo Stonecroft inafanya kazi.

Kila somo limeandaliwa maalum kabisa ili wale ambao hawamjui Mungu nao wapate kushiriki,kwa bahati mbaya wanawake wa Africa sio wote walio na biblia na ndio maan kulasa za biblia zimetolewa na kuacha vipengele vya biblia tu ili kuwawezesha nao kushiriki vizuri.na hii imeandaliwa katika mpangilio maalum wa kimatukio.

Masomo ya biblia ya Stonecroft yanaendeshwa katika nyumba, maeneo ya kazi, makanisani, mashuleni, hata chini ya mti katika vivuri huku Africa.

Masomo haya yameandaliwa katika, kufundisha juu ya kichwa furani cha somo lakini hata hivyo masomo yanayo husu vitabu vya biblia yanapatikana katika hatua ya juu.
Masomo ya biblia ya Stonecroft ni rahisi kujisomea katika makundi madogo na hata makundi makubwa, na masomo haya yanaanzia (4-14 masomo).na utatu masomo 6 kwa hiyo kitabu kimoja kna masomo 18.

Masomo mengi yanakuwa na kitabu cha mwongozo wa masomo, kitabu hiki hutumika pamoja na biblia na kila anae shiriki masomo haya
Majadiliano ni njia mojawapo katika ukuaji wa kiroho.

USHAURI WA KUJISOMEA:
Katika maeneo mengi ya Stonecroft washiriki hutumia kitabu cha mwongozo na biblia ya Kiswahili, ambayo hupatikana madukani, lakini kama nilivyosema kitabu cha mkononi cha biblia kinapatikana kwa wale wasio na biblia.

Vikundi hivi vya kujisomea hukutana mara moja kwa wiki, kwa dakika 60-90 .kama dakika ni chache kundi wanaweza kuamua kugawa masomo haya nusu, kwa kugawana maswali na kusoma andiko.ili kutanua kazi ya uanafunzi tunashauri kuwa vikundi lazima vitafute njia za kuongeza washiliki ili ufanisi wake uonekane katika jamii.

MAELEZO YA MASOMO:
Kuna aina tatu za masomo ya biblia ya Stonecroft:
•Masomo ya Utangulizi wa utatu.
• Masomo ya wakristo wanao kuwa.
• Na masomo yahusuyo vichwa vya somo.

Stonecroft waanze na somo la Utangulizi, ambalo linasema “Yesu ni nani” Mungu yukoje?’ na Je Roho mtakatifu yuko wapi.haya ni masomo muhimu sana kwa wakristo wapya na hata wale wa zamani maana ni muhimu hata kwa wale wanao taka majibu ya maswali yao. Haya masomo yote yamekwisha tafsiliwa Kiswahili na kazi bado inaendela ya kutafsiri huko Congo na Malawi pia.

KANUNI NA SHERIA ZA MASOMO YA KIBIBLIA YA STONECROFT
Huduma ya Stonecroft imejiwekea kanuni kwa jili ya masomo yake ya kibiblia, ni muhimu kwa mtu yeyote anae hudumu katika huduma hii ya Stonecroft afuate hizosheria na kanuni
Injili ya Yesu ambayo imeandikwa katika kila somo la Stonecroft ni muhimu kuwa ihunbiriwe kwa uhakika na umakini mkubwa.

Huduma ya Stonecroft hawana msimamo mwingine wa imani, au msimamo wa kisiasa nje ya maelezo yao ya imani.

Wote ambao wanajihusisha na Stonecroft watafanya haya yafuatayo:
• Kukubariana na msingi wa imani ya huduma ya Stonecroft.
• Kutenda kazi kwa ushiriano na kanisa lako.
• Kila neno litakalo nenwa katika mjadala au mazungumzo wakati wa masomo huo sio msiomamo wetu kama huduma ya Stonecroft.

Katika kujisomea haya masomo ya biblia ya Stonecroft, ni muhimu wahusika wote wakatumia vitabu ambavyo vimethibitishwa na Sonecroft, katika somo la utangulizi inashauliwa kuwa wahusika wote watumie aina moja ya biblia ya Kiswahili.

Watu wote ambao watakuwa wanaisimamia au kuongoza haya masomo ya kibiblia ya Stonecroft ni lazima watume maombi,waongozaji na wakufunzi hufundishwa na kiongozi wa eneo husika, video ya masomo hayo imekwisha andaliwa na Stonecroft Barbados ili kuwezesha kuwafunza wale watu ambao wako Tanzania, Malawi, Uganda na nchi nyingine za Kiafrica,hii video ya dakika 15 itarecodiwa kwa Kiswahili na lugha nyingine za kiafrika, hii yote ni katika kuhakikisha kuwa tunawafunza wale ambao watakuwa viongozi, ukiambatanisha na Mwongozo hii itawapa uwezo mkubwa katika huduma.

MKAKATI WA MWONGOZO WA KUFUNZA:

Kazi ya huyu mwongozaji ni kuongoza masomo haya ya kibiblia,na wakati huo huo washiliki watakuwa na muda wakuleta mabadiliko katika jamii ya kuwaleta watu kwa Yesu, katika kundi hilo pia wanaweza kuona ni nani anafaa kuanzisha kundi jingine la kujisomea biblia, hii ni baada ya kumaliza vitabu vyote vya utatu.

Masomo ya kibiblia ya Stonecroft na mwongozo wake:
• Kuwaombea wote ambao wanakuja katika masomo ya kibiblia.
• Anza masomo haya ya biblia kwa maombi.
• Kiongozi wa masomo haya ya kiungozi, ambaye atampa majukumu ya kusimamia kikundi husika lakini yeye ataendela kupewa taarifa.
• Huyu kiongozi atahakikisha kuwa anafuata kanuni na sheria za huduma ya huduma ya Stonecroft kwa kufuata maelekezo yaliyoko katika video.
• Anandaa kundi lake kwa kupitia kitabu cha mwongozo, atawakumbusha wana kikundi juu ya umuhimu wa siri katika kundi na kundi kuelekrza maswali yao katika maandiko.
• Masomo ya kibiblia ya Stonecroft pamoja na mwongozo wake unatoa fursa kwa wanakikundi kuielewa vizuri huduma ya Stonecroft, na nafasi za kujiunga nao.
• Atateua watu ambao watajaribu kupata majibu ya maswari yahusuyo imani, majadiliano yanhimizwa juu ya nini biblia inasema na sio nini makanisa yetu yanasema au kufundisha.
• Atahakikisha anakwepa majadiliano yote yahusuyo imani na misimamo ya watu, siasa, kanisa lipi linapinga au kukubali.

SIFA ZA KUWA KIONGOZI
1. Kiongozi lazima awe kaokoka.
2. Awe ni mtu anae itanga nguvu ya mabadiliko kupitia neno.
3. Akubaliane na sheria na kanuni za Stonecroft.
4. Anawasiliana na kufanya kazi na wenzake.
5. Ana shauku ya kuona watu wanakuwa katika maisha yao ya kiroho na kumjua Mungu.

JINSI YA KUMHOJI MTU AMBAYE UNADHANI ANAWEZA AKAWA KIONGOZI.
KUMCHAGUA KIONGOZI

Wachungaji (kutoka Africa Training Bible School) ambao walifunzwa kuwa viongozi watawatambua viongozi hao kiurahisi, kwa kuomba, kwa hekima, na watoke katika makanisa yao, hawa baada kuwateuwa hao viongozi, watawezesha katika ukuaji na kutanuka kwa masomo ya ka kibiblia ya Stonecroft.

Ni muhimu sana katika kumtafuta Yule kiongozi atakae kuwa na sifa zitakazo endana na sifa zilizotajwa katika sehemu hii.

Maelezo yafuatayo ni muhimu sana unapotaka kumteua kiongozi.

Omba kabla hujaonana na mtu husika, omba ili Bwana awapeni nyote hekima Roho ya kupambanua .

1. Pangeni muda, muwe tayari kukubaliana juu ya masomo ya kibiblia ya Stonecroft na huduma.(ikihitajika).

2. Kwa yale maeneo tu ambayo yameolodheshwa katika fomu ya maombi ya Stonecroft.
o Toa maelezo juu ya huduma ya Stonecroft—mwelekezeke akasome:
• Kijitabu cha masomo ya biblia cha Stonecroft.
• Tembelea mtandao www.stonecroft.org kwa maelezo zaidi.
o Mwambie akupatoe ushuhuda wake wa kumwanini Yesu tu katika wokovu wake na akupe maandiko ya biblia.
o Muulize je anaweza akajibu nini iwapo ataulizwa Yesu ni nani .
o Muulize kwanini anataka kujiunga na masomo ya kibiblia ya Stonecroft .
o Chunguza juu ya utayari wake wa kufanya kazi na watu, wa imani tofauti na tamaduni tofauti
o Muulize juu ya mambo mengine anayo yafanya, na pia anafurahishwa na nini katika kusoma neon na kuwaongoza wengine katika kujisomea biblia.
o Hakikisha anazielewa sheria na kanuni za Stonecroft na imani.

Mtu yeyote anaetarajia kuwa kiongozi lazima aelewe Kanuni na sheria za Stonecroft, na mwongoz wake.

Majukumu ya mchungaji ambaye atakuwa Coordinator (Muunganishaji)

Uwe umekwisha pata fomu ya maombi ya mtu anaye taka kuwa kiongozi.

Kwa umakini wa hali ya juu soma fomu ya maiombi na hakikisha kuwa ushuhuda wa kiongozi uko sahihi.

Kwa maombi unapaswa kumuuliza huyo mtu maswali machache kuhusiana na Yesu, kwa mfano.
1. “Ninashauku ya kusikia safari yako na Mungu, hivi Yesu ana nafasi gani?
2. Iwapo mshiriki wa Stonecroft kakuuliza kuwa anawezaje kuwa na uhusiano na Yesu utajibu nini?
3. Unaelewa nini kuhusu injili na unawezaje kuihubiri?
Unaweza ukataka kusoma kupitia hili neon je unaweza amini?

Kitabu na mwongozo.

Panga muda wa kumfundisha muhusika kama kiongozi, tumia nyenzo zifuatazo.

Kitabu cha kibiblia cha Stonecroft cha Africa.

Iwapo hajawahi kukisoma kitabu cha Sonetabu kama “Yesu ni nani”ili wapate kuelewa ni kitu gani kinahusika katika haya masomo.

Mchungaji au mkurugenzi atakuwa na fomu za maombi katika faili lake.
Kumbuka kwamba sio kila mtu yuko tayari kwa ajili ya kuongoza,ukihisi kuwa huyo mtu hawezi akaepukana na mambo yanayoweza kuleta mkanganyiko kama vile siasa na mambo mengine ya kijamii ,basi mtie moyo kuwa yeye asiwe kiongozi bali abaki kama mshiriki tu, wa hicho kikundi.

Baada ya kumaliza haya mafunzo ya uongozi wasiliana na kiongozi wa Stonecroft wa Africa kwa barua pepe na mawasiliano mengine ya ziada.

Kiongozi wa Stonecroft wa kijimbo ambaye ni Mchungaji David Akondowe, atawasiliana na huduma ya Stonecroft ya Marekani, anaweza akafanya hivi kwa barua pepe: connections@stonecroft.org.

Atuma anuani ya kiongozi iliyo kamili, namba ya simu, na barua pepe.
Nao Stonecroft wakisha pokea hayo maelezo watamkaribisha huyo kiongozi mpya kwa barua pepe, ambayo itatafsiriwa katika lugha ya eneo husika, na kuanzanzia hapo huyu kiongozi ataunganishwa katika mtandao wa watu wakujitolea na anaweza kunza kupikea barua na majarida katika barua pepe.na anaweza kutembelea mtandao wa viongozi, na kujipatia mambo mengi ya kujisomea katia mtandao wa Stonecroft Ministries website. (www.stonecroft.org)

Hawa viongozi wapya watatambuliwa kama viongozi kwani tunatambua mchango wa kila mmoja wetu katika kazi hii muhimu ya kuufikia ulimwengu na injili ya Yesu.

KUWAWEZESHA VIONGOZI WA STONECROFT:
Walimu waliofunzwa vizuri ni muhimu sana katika hii kazi ya kuwafundisha watu katika imanina hata wale ambao wako katika masomo ya kibiblia kwa miaka mingi.

Hawa viongozi wengi hutuma majarida mara kwa maana ili kuwa na mawasiliano na watu,hata mawasiliano ya kuhusu kongamano iwapo wapo katika Skype, na mawasiliano mengine ya mtandao wa kijamii.

Hawa wakurugeni waandae mikutanio ambayo wanaweza kukutana na viongozi hawa kwa mwaka mara moja ili watiane moyo na kuweshana ili Stonecroft ipate kusonga mbele.
Mambo mengi yana shuhudiwa katika mawasiliano, kuwa na maono mamoja, na kujifunza kwa pamoja,na namna ya kujibu maswali magumu.

Kuwafundisha walimu wapya kunaweza kupangwa katika kipindi maalum kama vile, muda wa Krismass, na likizo nyingine.

Haya ni mawazo muhimu iwapo unajipanga kuwa na mafunzo ya viongozi:
• Muda maalum kwa ajili ya maombi na ushirika na Mungu.
• Changamoto ya maandiko au maombi.na kuwatia moyo;
• Utangulizi na kushuhudia matokea chanya ya kujisomea biblia.

Muda wa kujifunza: i.e. namna unavyo shuhudia inasadia kuongeza namna ya kuwafikia wengine, kuanzisha Stonecroft katika makanisa,na huu uwe muda wa kujifunza kutoka hata wkwa wengine, tuwe na kiongozi ambae anaelezea namna anavyo waalika wengine, matatizo waliyo kutana nayo.na eneo lipi walimwona Mungu akiwatetea. Hitimisha kwa maombi na kuwatia moyo.

MWONGOZO KWA KIONGOZI:
DHUMUNI:

Kuwafikia wasio fikiwa – haya masomo yanawezesha kuhubiri wokovu kwa kupitia Yesu,
Tunataka kutanua huduma ya Stonecroft kupitia makanisa 280 ambayo yana wanafunzi wake katika chuo cha ‘Africa Training Bible School’ (ATBS) katika nchi za Tanzania, Malawi, Zambia na DR Congo na pia kupitia Hope Community Centre, Kampala, Uganda.
Pia tunamwamini Mungu tunaweza kujumuisha haya kupitia mradi ule wa kuwezesha wanawake

‘Stonecroft Women’s Empowerment Program’ (SWEP) ambao mtajifunza mengi hapo baadae. Mradi huu wa kuwawezesha wanawake utatumia vitabu vya Stonecroft kuanzia vile vijitabu vya utatu, Mungu yukoje? Yesu ni nani? na Roho Mtakatifu yuko wapi?

Katika kuhakikisha kuwa tunaukuza mradi wa SWEP mafunnzo ya kiafrica, hawa wanawake watahimizwa kuwa viongozi, watatumia Video ya mafunzo ya kiafrica, na pia kitabu hiki ambacho kitawawezesha kuanzisha, Stonecroft katika nyumba zao, makanisa na hata vijiji vyao, kwa kupata ruhusa maalum kutka kwa mchungaji wao.

Uanafunzi – wakristo wapya na hata wale wa kale wanaweza kijifunza habari za Yesu na kuweza kuwa na mahusiano ya karibu na Mungu, masomo haya yanatufundisha namna ya kutumia biblia katika mazingira yetu ya kila siku, kuna vitabu vingi ambavyo navyo vitatafsiliwa katika lugha nyingine. ‘Africa Training Bible School’ watatumia masomo haya kama nyenzo moja wapo za kufundishia katika mitahara yao. Kwa mfano, maisha mapya, kuishi maisha yangu, wafilipi, Yakobo, Warumi na vingine vingi.

UFAUTI:
Fautisha masomo ya kibiblia ya Stonecroft na masomo mengine ya biblia?
• Masomo haya yameandaliwa mahususi ili yatumike katika agano jipya ambalo linapatikana sana katika nchi ya Tanzania, lengo kuu ni kuihubiri injili ya Yesu Kristo, na kuwatia moyo watu ili wapate kujisomea maandiko kila siku, hatujajumuisha namba ya kila ukulasa katika biblia maana wengine wanaweza wasiwe na biblia.
• Masomo haya ni rahisi hata kw wale ambao ndio wanaanza kujisomea.
• Kumbuka kuwa kiongozi sio mwalimu wa biblia lakini wote wanasoma pamoja na washiriki wa kikundi.
.
NYENZO:
Masomo ya kibiblia ya Stonecroft hisi kuyasoma.

Kuna maeneo ambayo yamefungiwa ambayo hupaswi kuyasoma kwa sauti.

Maneno yaliyo chapishwa katika boksi unapaswa kuyasoma kwa sauti ili washiriki wapate kusikia.

Kwa mfano nucta zikifululiza (.....) inakwambia kuwa kiongozi awaruhusu washiriki wachangie kwa kuuliza maswali, kusoma biblia au kujadili somo.

Ukiona wino umekolezwa unao ambatana na nucta Tano, ina maanisha mstari wa biblia usome kwa sauti kubwa na msomaji.

Ikiwa kama kifungu kilicho nukuliwa kimeandikwwa katika maandishi ya kawaida ina maana, hakihitaji majibu au ni kirefu sana kusoma hadhatrani.

KABLA YA MASOMO YA BIBLIA
Vitu muhimu –
Unaweza ukawa kiongozi uliye thibitishwa na Stonecroft wetu kwa kujaza fomu iliyo tafsiriwa kwa Kiswahili.

Tunataka kujiridhisha kuwa baada ya kusoma kanuni na sheria pamoja na maelezo yetu ya imani, huna wasiwasi tena nasi.

Vitu vinavyo hitajika katika kujisomea:
1. Vitabu vya utangulizi vya utatu vilivyotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili vinaweza patikana, katika makao makuu ya ATBS, Mbeya, Tanzania.
2. Vitabu vya mwongozo vinapatikana makao makuu ya ATBS, Mbeya, Tanzania.
3. Biblia ya Kiswahili inapatika Tanzania Bible Society.na madukani.
4. Je unaweza kuamini hili? Nacho kimetafsiriwa kwa Kiswahili kinapatikana katika makao makuu ya ATBS, Mbeya, Tanzania.
5. Kadi ya maelezo nayo imetafsiliwa inapatikana makao makuu ya ATBS, Mbeya, Tanzania.
6. Fomu ya maombi ya kiongozi nayo inapatika katika makao makuu ATBS, Mbeya, Tanzania

Tafuta eneo zuli kwa ajili ya kujisomea biblia, labda nyumbani, kanisani, shuleni, nyumbani katika kivuli chini ya mti.

MAANDALIZI YA KIONGOZI KABLA YA MASOMO:
Hakikisha unajibu maswali yote ya kijitabu cha mwongozo kabla ya kuanza kusoma vitabu, hii itakuwezesha kuelewa watakao kuwa na wajibu wanapitia katika wakati gani kabla ya kupata majibu halisi.
• Fanya zoezi la kusoma hayo masomo kwa sauti,ikiwezekana,pigia msitali maneno muhimu utakayo ongelea katika kundi lako,masomo hayo yasizidi saa moja na nusu1 – 1 1/2 hasa pale ambapo masomo haya yanaendeshwa katika kuwezesha wakina mamam yani ‘Stonecroft Women’s Empowerment Program’ (SWEP) maana wanawake watahitaji kuondoka na kuanza kujifunza kushona
• Wakati huo huo wanafunzi wa SWEP wanapofurahi masomo yao,watoto wao watakuwa wakihudhulia “Powerclub” wakijifunza njia za Mungu kupitia ‘Kids in Ministry International’ (KIMI) pamoja na watoto wengine kutoka katika mkakati wa ‘Kids Evangelism Explosion’. (Kids EE)
• Maeneo haya kwa wakatio huu yatakuwa;
Tanzania – Africa Training Bible School (ATBS) – Mbeya Tanzania
Uganda – Hope Community Centre, Kampala
Malawi – Africa Training Bible School (ATBS) – Uluwa and Vulwa, Malawi
• Omba juu ya wale watakao kuwa wanakuja.

WAKATI WA MASOMO:
Mara zote anza masomo haya kwa maombi, ikiwa kama kuna mtu ana hoja basi kundi liandike hiyo hoja yake na mtaiombea katikati mwa juma.

Ikiwa kama hitaji lake ni maombi ya dhalula basi yajumuishwe siku hiyo hiyo.
Kumbuka kila mara uanzapo somo la “Yesu ni nani” kila mshiriki ataandika jibu lake katika kijitabu cha kujisomea, na uwakumbushe kuwa ni vizuri wakawa wanajaza majibu kabla ya kuja darasani.

Soma na kuwapatia washiliki maelezo katika mtindo wa uwazi huku ukiwangalia usoni, Kiongozi huwa najifunza na kusoma na kundi lote la washiriki, hutakiwi kuwa umeisimea sana biblia.

KIONGOZI ANAHAKIKISHA NAFASI NA SAUTI HUTUMIKA VIZURI KATIKA KUJISOMEA:
• Kuanza na kumaliza kwa muda mzuri, kumbuka masomo haya ya biblia yatakuwa pamoja na shule ya kuwawezesha wanawake.ambao watahitajika kwenda kushona.
• Tumia kitabu cha kiongozi na biblia ya Kiswahili hakita hitajika ktabu cha ziada.
• Watie moyo kila mtu ili ashiliki katika kujadili, na hakikisha hakuna ambaye anaongea kuliko wenginehakikisha unawatia moyo unapowasihi wajadili.
• Mtazamo wako umuelekee Yesu, na usijadili misimamo ya mafundisho ya kikanisa, au misimamo ya kisiasa, maswali ya misimamo na mafundisho ya makanisa yashughurikiwe maeneo mengine.

Tafuta watu ambao watakuwa viongozi wa baadae wa kundi.

Kama kiongozi ni lazima uwe mifano wa kundi, hakikisha watu hawajadili mambo ambayo yanapaswa kuwa siri, kwa mfano mambo yale ya nyumbani. Uombe pamoja nao na kuwasihi watafute mwongozo wa Mungu.

Baada ya masomo ya Stonecroft yakina mama kufikia tamati, kila mtu ambaye anaoneka kuwa ni kiongozi basi apitie mafunzo maalum ya uongozi, kwa kutumia video na kitabu maalum cha uongozi, ili waweze kupeleka stonecroft nyumbani kwao. Na katika makanisa yao.

Uwaulize washiriki wafikilie watu ambao wanaweza kuwaarika, uwahimize waanze kuwaarika watu katika masomo, na pia waanze kuwaombea kwa kuwataja majina yao.

Mambo muhimu ya kukumbuka.
• Iwapo huwezi kuongoza masomo haya ya biblia kwa sababu yeyote ile, basi kiongozi aliyethibitiswa aje na kuchukua nafasi hiyo.
• Hutakiwi kumpatia mwenzako kitabu cha mwongozo mtu yeyote Yule hata kama uko nae katika dara moja.

MKAKATI WA STONECROFT WA KUWAWEZESHA WANAWAKE
‘STONECROFT WOMEN’S EMPOWERMENT PROGRAM’ - (SWEP)

Masomo haya ya kibiblia ya stonecroft yanapangiliwa kutenda kazi pamoja na mpango wa kuwawezesha wakina mama kupitia mradi wao wa kujishonea (SWEP) huu ni ushirikiano wa mashirika mawili yani Stonecroft and United Caribbean Trust (UCT), shirika la Kibarbados ambalo limesajiliwa kama shirika la huduma za kijamii. Tunaamini kuwa mwanamke mwenye uwezo wa kupata elimu, na akijua haki zake, anaweza kubadirisha dunia hii.

Wakina mama ambao wanapitia mpango wa kushona wa Stonecroft watakuwa katika mafunzo kwa muda wa mwaka mmoja.

Kila wiki atakuwa akihudhuria ‘Kukutana na Mungu’ huu ni wakati wa kuomba, na tutatumia vitabu vya kujisomea vya Stonecroft vilivyo tafsiriwa katika lugha za maeneo husika.
Na pia atahudhuria dalasa la kushona nguo na mitindo, masomo ya computer, na kujifunza moringa na ufugaji wa wanyama.

US $40 kila mwezi itatumika katika kuwawezesha wanawake ambao watakuwa wakihudhuria hayo masomo, ambapo yatamsaidia katiak kupata elimu, masomo ya kazi za mikono, na vifaa vitakavyo muwezesha kuwa na mradi utakao muwezesha kujipatia kipato.
Lakini zaidi ya yoote, haya mambo yatafungua mlango ili mwanamke ajifunze uongozi kupitia masomo ya ya Stonecroft.

Na pia atapatiwa nafasi ya kumleta mtoto mmoja atakae kuwa anaingia katika mradi uitwao ‘After School Feeding Club’ ambao utatoa chakula cha kimwili na kiroho.

Ni shauku yetu katika kuwafikia wanawake wa Tanzania, Malawi, Zambia, DR Congo na Uganda, kwa kuwaonyesha upendo wa Mungu na kuwafungua kutoka katika umaskini.
Tunawashukuru Stonecroft kwa kujitoa kwao katika kuwafikia wanawake katika maeneo yaitwayo 10/40 window (wasio fikiwa).

MFUMO WA UANAFUNZI WA KIAFRICA:
Huu mfumo wa kiafrica wa ambao ni wa kugawanya na kuzidisha ni muhimu kuliko wa kuongeza!
1. Mfumo huu utaanzishwa kwanza Tanzania kupitia, ‘Africa Training Bible School’ (ATBS) ambao lengo lao la kwanza ni kuwa funza wachungaji kutoka makanisa 280 ambao wamo katika mpango wa ATBS ili wajiunge na masomo ya kibiblia ya Stonecroft. Watafundishwa kwa kupitia video na ktabu cha kiafrica cha kufundishia, hawa wachungaji watakuwa viongozi wa kwanza wa Stonecroft Tanzania, na Bwana akipenda kila mmoja wao atapatiwa kitabu ca utatu 10, Mungu yukoje? 10 Yesu ni nai? 10 na Roho Mtakatifu yuko wapi? Na kitabu ambacho kimejumuisha vitabu vyo hivi vitatu.
2. Hawa wachungaji watachukua taarifa hii na kwenda nayo katika vijiji vyao ambao nao watachagua mwanamke mmoja, labda kiongozi wa kinamama, na baada ya hapo atamfundisha huyu mama,na mchungaji atabaki kuwa mwangalizi wakufuatilia kazi inaendaje tu.
3. Watapatiwa kitabu cha mwongozo cha Stonecroft na vitabu 10 vya Stonecroft ‘Mungu anaonekanaje?’ Vyote hivi vimetafsiriwa katika lugha yake anayo ielewa, na atapewa vitabu vingine 10 ,naye atatafuta wenzake 5 katika kanisa ili waanze kujifunza.
Na hawa 5 nao walete mmoja kila mmoja wao, katika huduma ya Stonecroft,na wataanza kujifunza utatu, ‘Mungu anaonekanaje?’ Baada ya hapo ataendelea na “Yesu ni nani?” Na atahitimisha na “Roho Mtakatifu yuko wapi?” Na atatumia videa na kitabu kuwafundisha ili nao wakawafikie wengine.
4. Na akifikia hapo atakuwa kiongozi wa wenzake hao 5. Na atakacho kifanya ni kurudia masomo ya Stonecroft kwa wanawake watano wengine tena kanisani.hawa watano wa sasa watatiwa moyo kuwaletwa watu wasio okoka kanisani, sasa ataanza kuwafikia wasio fikiwa. .
5. Mchungaji kwa wakati huu atakuwa ni mtu wa kutoa ushauri na mwangalizi.
6. Hawa viongozi wapya 5 pamoja na mwana maombi wao, watamtafuta mtu mmoja kanisani au kijijini ambaye ana sifa za kuwa kiongozi, wamfundishe kwa ruhusa ya mchungaji wao.
7. Kwa pamoja hawa wakina mama 5 watawasihi wasio mwamini Mungu wajiunge na masomo ya Stone croft,ya utatu,kwa kawaida kila mmoja awe na wakina mama 2, kumbuka masomo haya yawe na wakina mama 10 - 12 wanawake.
8. Wakisha kujifunza masomo haya ya utatu basi huyu mwangalizi atawafundisha wakina mama 2, mmoja toka kanisani kwake na mwingine kanisa jingine ambao watakuwa viongozi wa Stonecraft wa kizazi cha nne. Wana maombi wake watabaki na darasa hili katika kulifundisha.
9. Mtindo huu utandelea katika kanisa ambalo limejifunza mkakati huu.
10. Iwapo kuna swali ambalo huyu kiongozi hawezi kulijibu basi amuhusishe mwangalizi wake.
11. Kwa kadri muda unavyo zidi kuendelea tutapata waangalizi wengi zaidi kwa kadri mtandao huu unavyozidi kutanuka na video nyingi sana zitatengenezwa.
12. Kumbuka - kugawa na kuzidisha !
13. Kuzidisha ni bora kuliko kuongeza!'


‘Uwe macho, Simama imara katika imani, Uwe jasiri,uwe mwenye nguvu. Fanya kazi zote kwa upendo ’

1 Corinthians 16: 13 – 14

 
     
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us