Project Hope     home >>vijana wa stonecroft>> mwongozo >> somo 1
Mwongozo Somo #1
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

MUNGU ANA MWONEKANO GANI?

SOMO LA KWANZA(1)

MUNGU YUPO

Lucille Sollenberger. B.S., M. A.

Stonecroft Ministries
www.stonecroft.org
P.O.Box 9609, Kancas City, MO 64134-0609

Download Full Guidebook

Download Lesson #1 Guidebook Introduction

Download Lesson #1 Guidebook

Download Guidebook Bible Verses Lesson#1

LENGO LA SOMO
• Anza kuelewa Mungu kuwa yukoje na anakuwa kama nini.
• Tambua kuwa Mungu mara zote ana furaha
• Ikubali Biblia kama ndiyo chanzo cha majibu.

MAOMBI
Baba yetu uliye juu, tunataka kujifunza kitabu hiki ulichokiandika mwenyewe ili sisi tukuelewe wewe. Fungua macho yetu, masikio yetu, na mioyo yetu ili tuweze kuelewa kile unachotaka sisi kujifunza kutoka kwako. Twaja kwako kwa jina laYesu kristo …….AMEN

MAONI YA KIONGOZI

Kutusaidia sisi kufaidika kutoka katika haya masomo, kuna mwongozo ambao tutaufuata.

JINSI YA KUJIFUNZA MASOMO YA BIBLIA KATIKA STONECROFT

(Use your Bible or Africa Bible Verse Handbook)

Kwa sababu hii ni shule ya Biblia, lengo letu kuu ni kujifunza kile ambacho Biblia inasema na jinsi gani tunaweza kutumia katika maisha yetu. Kijitabu hiki na Biblia ndivyo vitakuwa vitabu vyetu ambavyo tutavitumia katika masomo yetu.

Inatakiwa tujiandae kwa somo kwa kumaliza maswali katika vijitabu vyetu hivi vya awali. Hii itatusaidia katika majadiliano yetu ya wiki kufanya kwa urahisi na kuelewa vizuri kuhusiana na somo husika kwa wakati huo. Tutajifunza somo la kwanza sote kwa pamoja.

Masomo yetu haya ya Biblia yataanza katika muda muafaka na yatachukua muda wa dakika 60 mpka 90. Tutaondoka pale ambapo somo letu husika tunalolisoma litakapokuwa limefikia mwisho kwa hiyo hatutaacha kitu tutamaliza.

Kwa sababu tunatoka katika mazingira tofauti tofauti na (ukijumuisha tunatoka katika makanisa tofauti tofauti) kwa hiyo tutaheshimu mawazo ya kila mtu na imani yake.

Katika wiki chache, tungependa kuanza masomo mapya ya Biblia katika maeneo mapya na kwa watu wapya. Hebu fikiria mtu ambaye ungependa umwalike katika masomo haya.

Mungu yeye ni nani? Swali limekuwa linasumbua sana watu kwa karne nyingi sana zilizopita. Wametafuta katika historia, wakajaribu ,kujua kuiwa Yesu ni nani na anafanyaje kazi.

Lengo la masomo haya ni:
• Kujifunza Biblia inavyosema kuhusu Mungu.
• Kutambua jinsi maisha ambavyo yatakuwa baada ya kumjua Mungu na kuwa na ushirika na yeye.
• Kutumia tuliyojifunza na kuendeleza kwa undani zaidi, uhusiano tulionao na Mungu.
Ili kuchochea kufikiria kwetu, kumbuka yafuatayo:

MUNGU YUPO
Biblia inatuambia ukweli kuwa Mungu yupo. Hakuna utuibitisho mwingine kuwa Mungu hayupo, Mungu yupo. Hakuna mjadala juu ya hili. Mtu anayechukua Biblia kwa mara ya kwanza na kuisoma ni kwamab atajua kaisa kuwa Mungu yupo na bila hata mashaka yeyote yale. Mungu, ni kweli na ni Mungu mwenyezi yupo. Ni yeye aliyefanya kila kitu katika dunia hii.

Mungu ,muda wote amekuwapo,
na atakuwepo,
uweza wake unawakilishwa na maneno mawili tu:
Mungu yupo. 

Unaweza ukawa na mwitikio upi katika maelezo haya? (Jadiri, tambua na tia moyo mawazo)

Mwenyezi , huwakilisha Mungu, ambaye anajua kila kitu, yuko mahali hapa. Mara zote atakuwepo, kwa sababu Mungu yupo .

“lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao”.
- Waebrania 11:6

Agano jipya linazungumzia ukweli kwamba “Mungu yupo” kwa kutumia neno linguine badala ya “yupi” au “ni”.

1. Usome Waebrania 11:6…….. je ni neno gani ambalo linatumika katika mstari huu kuonesha ukweli kuwa Mungu yupo? ……(anaishi, au yu hai).

Mungu amekuwa akiishi au yu hai na ataendelea kua hai tu. Watu wanaishi nawe pia unaishi. Miili yetu ina Mwanzo na ina mwisho wake. Lakini, Mungu han a Mwanzo wala mwisho. Kusema kuwa, Mungu yu hai ni sahihi. Hakuna muda, ambao Mungu hakuwepo. Alikuwepo na atakuuwepo tu.

MUNGU NI MUUMBAJI

Tangu Mwanzo hakukuwa na kitu ; lakini Mungu pekee yake ndiye aliyekuwepo. Kulikuwa hakuna mbingu, dunia, jua, mwezi, au nyota. Mungu alisema tu na mambo yote yakatokea na uumbaji ukaanzia hapo. Alianza kujaza utupu uliokuwepo, kuumba vitu kutoka katika sehemu ya utupu. Mungu yeye ni muubaji wa kila kitu katika ulimwengu huu.

Je agano la kale linasema nini kuhusu kuwa Mungu ni muumbaji?

2. Soma mistari ifuatayo ya Bibblia, na ueleze kwa amaneno yako mwenyewe ukweli wa kila mstari kuwa unafundisha nini?
(Kumbuka maandiko ya agano la kale yanaandikwa katika kila mwisho wa somo.)

Nehemia 9:6…….

WakoLosai 1:15-16……..

Ukweli ulioandikwa katika mistari hii ni (Mungu ndiye muumbaji wa vitu, vyote.)

Mungu ni muumbaji wa vitu vyote. Mwanzo , kuitabu cha kwanza katika Biblia, inatuambia kuwa Mungu akasema tu na vitu vikatokea. Neno lake lina nguvu sana. Alisema na kukawa na nuru. Alisema na vitu ambavyo havkuwepo vikatokea ambavyo havikuwwepo. Kwa hiyo kila kitu unachokiona Mungu alisema tu na kikatokea, na kuhusiana na sisi wanandamu Mungu alitufanya kwa mikono yake mwenyewe. Je ni Mungu gani wa ajabu, huyu ambaye tunaye. Aliumbakila kitu kinachoonekana katika ulimwengu huu ambao tupo.

MUNGU NI WA MILELE

Maneno haya mawili kuwa Mungu yupo yanaonesha kuwa Mungu ni wa milele. Umilele ni wazo ambalo ni vigumu sana kulielewa, kwa kuwa tunaishi kwa muda.

Sis ni wafungwa wa muda. Muda tulipozaliwa ulirekodiwa, ,kwa hiyo kuna ,muda ambao tutakufa. Kila kitu tunachokifanya katika maisha yetu haya, kuanzia Mwanzo mpaka mwisho, vinapimwa na muda yaani miaka, siku, masaa, na dakika. Tuliumbwa kwa ufahamu wa mjuda, kwa hiyo ni vigumu sana sisi kulewa kablaya wakati.

3. Soma mistari ifuatayo ya Biblia na uandike kwa maneno yako mwenyewe, ukweli unaofundishwa katika mistari hiyo.

Zaburi 102:12, 25-27………… (Mungu ni wa milele)

Mungu yeye alikuwepo kabal ya wakati, hana Mwanzo na wala hana mwisho. Anaishi milele.

Tunaishi katia nyakati tatu, wakati uliopita, wakati uliopo, na wakati ujao. Tumeshaishi wakati, uliopita kwa sasa tunaishi katika wakati uliopo, na tutaishi wakati ujao. Mungu alikuwa akiishi hata kabla ya kila kitu kuwepoi hapa duniani na ataishi milele.

Mungu hana Mwanzo wala mwisho. Ila sisi tuna mwanazo na tuna mwisho, lakini cha ajabu zaidi ni kuwa hatutakuwa na mwisho. Miili yetu hii itakufa, lakini nafsi zetu na Roho zetu zitaishi milele.

Biblia inatuambia sisis katika Mwanzo 2:7 jinsi Mungu alivyomfanya mwanadamu ili kuishi milele. Inasema kuw Mungu aliweka pumzi ya milele kwa mwanadamu au katika maisha ya mwanadamu, na akawa nafsi inayoishi.

Mungu aliumba watu ili wamjue yeye. Na hilo ndio lengo la somo hili, kumjua Mungu na kujifunza kuwa yukoje. Katika somo hili tumejifunza kuwa:

- Mungu yupo. Hana Mwanzo na hana mwisho.

- Yeye ni muumbaji wa kila kitu katika mbingu na duniani.

- Yeye ni wa milele- yeye yupo hivyo na ataishi hivyo.

Kitu kingine cha muhimu ambacho Biblia inatuambia kuhusu Mungu nui kuwa yeye ni wa pekee na yuko peke yake.

MUNGU MMOJA TU PEKE YAKE

4. Soma mistari ifuatayo na ujibu swali hili. Unaamini kuwa kuna Mungu mmoja tu anayeishi?........

Toa sababu juu ya jibu lako……..

Isaya 44:6………..

Isaya 45:5………..

(Kuna Mungu mmoja tu kwa sanbabu Biblia inatuambia hivyo, na kwa sanbabu Mungu anasema ni Mwanzo na mwisho. Hakuna Mungu mwingine na hakutakuja kutokea Mungu mwingine).

JE BIBLIA NI KWELI?
Tangu tumekuwa tukijibu maswali kutoka kattika Biblia, sasa unaweza kukawa unajiuliza maswali mengi kwa nini Biblia ni kutegemewa sana juu ya majibu yetu.

Waandishi wa Biblia wnasema kuwa walikuwa wanarekodi kila neno la Mungu. Kitu cha kushangaza ni kuwa, ingawa hiki si ma dai ya waandishi, waaandishi wote 40, walizungumzia msukumo. Takribani mara 3000 waandishi tofauti tpfauti wa Biblia, kwa njia moja ama nyingine, walikuwa wanawapa watu neno la Mungu.

Kitu cha kushangaza kingine ni kuwa hawa waandishi wa Biblia walitokea katika mabara matatu yaani Asia, Afrika na Ulaya. Maandishi yao yalitawanyika kwa zaidi ya miaka1500. Walikuwa wakitembea kwa muda tofautitofauti na waliandika maandishi hayo katika lugha tau tofauti tofauti. Lugha zilizotumika katika kuandika zilikuwa ni Kiebrania, Aramaic na Kigiriki.

Biblia tangu Mwanzo mpaka mwish o ni kweli kabisa. Ingawa inatoa mafundisho magumu kweli kweli. Kila kijisehemu kinataka kijisehemu kingine ili kuweza kukamilisha hadithi, inayotakiwa. Biblia ni Ufunuo uliojitosheleza, jinsi Mungu alivyotoa wokovu kwa watu wote na kupokea zawadi kuu ya ajabu.

Vitabu vingine ndani ya Biblia viliandikwa na ma nabii. Hawa walikuwa ni watu waliokuwa wanaongea neno la Mungu kwa watu. Waliwaambia vitu vitakavyotokea kabla havijatokea.

Len go la unabii ndani ya Biblia ni kutukumbusha tu kuwa Mungu anaishoi na kwamaba ana mpango na huu ulimwengu na kwa kila mtu ana mpango wake mzuri kabisa. Pia kwa ajili ya hawa manabii Mungu anatukumbusha tu kuwa .nini kitatokea wakati ujao.

Katiaka agano la kale .tunaona unabii ambao ulikuja kutimia wakati wa agano jipya. Kwa mfano unabii kuhusu kuzaliwa, kufa kuishi, na kufufuka kwa Yesu kristo. Hatuwezi kukaa kuangalia kila unabii kwa sababau ya muda. Kuna nabii mbili tu ambazo tutaangalia katika maswali mawili yanayofuata.

5. Tunaweza kuangalia kama utabiri kweli ulikuwa sahihi.

Nabii mika, alitabiri sehemu ambapo Yesu atazaliwa miaka 700 kabla hajazaliwa.

Mika 5:2………

“Bali wewe , Bethelehemu Efrata, uliye mdogo kuliko miongoni mwa elfu za yuda;
kutoka kwako wewe atanitokeammoja atakayekuwa mtawala katika Israeli;
ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele”.

Unabii huu ulitimia soma katika Mathayo 2:4-6……….

Yesu ilitakaiwa azaliwe wapi?.............. (Bethelehemu)

Maria aliishi mashariki mwa palestina, katika Nazareth katika ujauzito wake. Na bethelehemu ilikuwa kusini mwa palestina. Na pia serikali ya kirumi iliamuru kuchukua hesabu ya watu kwa ajili ya kukusanya kodi. Kwa hiyo kila mmoja alitakiwa kurudi katika sehemu yake yaani nyumbani kwao alikotoka ili waweze kuhesabiwa. Yufusu na maria walitoka katika ufalme wa daudi, ambapo wao kwao kulikuwa ni bethelehemu (1 Samweli 16:1……). Andiko lilitimia kwa sababu Yesu alizaliwa wakiwa tayeri wameshafika bethelehemu, na sio nazareth. Kwa hiyo Mungu peke yake angeweza kuwaweka pamoja na sio mtu mwingine.

6. Daudi alizungumzia sana maswala ya kuteswa katika shairi lake aliloliandika miaka 1000 kabla ya kristo. Kwa mfano :

Zaburi 22:18……………

“Wanagawanya nguo zangu,
na vazi langu wanalipigia kura.”

Tunaona kutimia kwa unabii huu katika Yohana 19:23-24……..

Je akari walifanya nini?...........

(Waligawa mavazi katika makundi manne, na kuyapigia kura.)

Utabiri huu ulimtimizwa na askari wa kirumi ambao walikuwa hawajui ya kwamba walikuwa wanatimiza utabiri wa wayahudi. Walikuwa hawajafungamanishwa na mtu ambaye tayari wamesha mtesa.

7. Andika ufupisho kwa kile Yesu alisema kuhusu agano la kale.

Luka 24:27, 44……….

(Kila kitu ambacho kimendikawa kuhusu Yesu katia agano kale inatakiwa yatimie.)

 

Wakati wa kuja kwake Messiah, kifo chake, kuharibiwa kwa yerusalemu, kuharibiwa kwa hekalu yote haya yalitabiriwa katika kitabu cha danieli miaka 100 kabla hayajatokea haya yote. Haya yote yalitimia ili unabii utimie na ndipo unajua kuwa Biblia ni kitabu ambacho kimehuishwa.

8. Je 2 Timotheo 3:16, inasema kuhusu msukumo wa Biblia?.........

(Maandio yote yamehuishwa na Mungu, na yanatumika katika kufundisha ukweli.)

MUHTASARI
Katika kila mwisho wa kulasa kuna eneo unaloweza kuandika. Tunaweza kutumia ukurasa huu kuandika vitu ambavyo tunataka kuvikumbuka.

Labda unapoendelea unaweza ukaendelea kuandaa notsi kuhusu mambo ambayo unataka Mungu akutendee au ayafanye. Katika ukurasa huu, unaweza pia ukarekodi mawazo mbalimbali kuhusu jinsi gani ambavyo unaweza ukjatumia mawazo haya ya kiBiblia katika maisha yako. Huu ni ukurasa wako. Tumia jinsi uwezavyo, kuleta maana nzuri kwa upande wako.

Kwa mfano unaweza ukaandika baadhi ya haya mambo ambayo tumejjifunza leo.

Tumejifunza nini kuhusu Mungu tunaposoma Waebrania 11:6?........(Mungu yu hai, au Mungu yupo.)

Tunaposoma Nehemia 9:6, tumegundua au tumehekikisha ukweli gani?..........(Mungu ni muumbaji wa kila kitu, ndaani ya mbingu na dunia pia.)

Mungu hana Mwanzo na wala hana mwisho. Je ni neno gani linguine ambalo linatumika badala ya hilo………….. (Milele.)

Biblia imekuwa ikirudia rudia na kutuambia kuwa Mungu wako wako wangapi?.......... (Ni mmoja tu.)

Sabababu moja ambayo ambayo tunaweza kuamini kuwa Biblia ni kweli ni hii, mtu mmoja tu ambaye alithibisha katika kuongea ukweli ndani ya Luka 24:27 ambaye ni (Yesu.)

9. Neno hili “MUNGU YUPO” lina umuhimu gani kwako, au lina maana gani kwako tangu umelisoma katika somo hili ?........(Kubali majibu yote, lakini sisitiza sana kuwa Mungu mara zote aliishi au alikuwepo na ataendelea kuwepo.)

Juma lijalo,somo la 2 ambalo ni utambulisho wa kujisomea wa juma,kila siku,soma mstari katika Biblia au Kitabu cha Biblia,ambacho ni kiambatanisho cha mwongozo huu ,mistari ya Biblia inaelezea sana kuhusu Mungu na hata kujibu maswari mawiri au matatu.
Hakikisha unaandika mambo mapya uliyojifunza kuhusu Mungu katika mwisho wa ukurasa wa somo hili.

Wiki ijayo katika somo la kwanza utaulizwa unaona nini unapofikiria kuhusu Mungu? Andika kitu cha kwanza kinapokuja ndani ya ufahamu wako. Andika kama ni halisia kwa upande wako. Mungu ni nani kwako?

Watu wengine wanafikiria kuwa Mungu ni :
- Mtu mkubwa saana anayeishi mbali sana.
- Asili
- Nguvu iliyopo angani
- Muumbaji aliyetuumba na kutuacha sisi peke yetu.
- Ni mwangaza mzuri na anang’aa na analeta utakatifu mbinguni.
- Mwanaume anayekaa katika kiti chake cha enzi na akiwa amekasirika kulingana na kile kinachotokea katika ulimwengu huu.

MAOMBI
Mungu mwenyezi, tumeanza kuona jinsi gani ulivyo mkuu. Tusaidia kulitambua hilo, ingawa uko zaidi ya ufahamu wetu, unataka sisi tukujue wewe. Endelea kutusaidia na kuelewa jinsi wewe Mungu ulivyo. Tunaomba katika jina la Yesu kristo ………AMEN

MAELEZO

____________________________________________________________________

____________________________________________________________________


 
 

 

This is a translation of 'What is God like?' Stonecroft's Guide Book Lesson #1 in Swahili, the English version of What is God like? is available online from Stonecroft's website.

In this fresh, engaging study, you will meet the Creator of life and the Sustainer of all things. As you study God's eternal characteristics, you will learn that He is majestic, all-powerful, holy, faithful, and just.

As you explore together what the Bible tells us about God, you'll also learn how to decide for yourself who He is and how He interacts with people. (6 lessons)

The Guide has her own Guidebook to help her lead and guide the lesson.

Download Full Guidebook

Download Lesson #1 Guidebook Introduction

Download Lesson #1 Guidebook

Download Guidebook Bible Verses Lesson#1

Mwongozo Utakaotuongoza

 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us