Project Hope     home >> stonecroft>> mwongozo >> somo 5 >> mistari ya biblia
Mistari ya Biblia - Somo #5
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

Nani awezaye kumjua Mungu?

Mistari ya Biblia

Usomaji wa Biblia wa kila juma

Yohana 14:21-23
21 Mtu anayezishika amri zangu na kuziti miza ndiye anayenipenda. Na mtu anayenipenda, Baba yangu atam penda; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.” 22 Yuda, siyo Iskariote, akamwuliza, “Bwana, itakuwaje ujidhihirishe kwetu tu na si kwa ulimwengu mzima?”23 Yesu akamjibu, “Mtu akinipenda atashika mafundisho yangu na Baba yangu atampenda, nasi tutafanya makao yetu kwake.

Warumi 5:6-9
6 Yesu alipomwona amelala hapo, na akijua kwamba amekuwa katika hali hiyo kwa muda mrefu, alimwul iza, “Unataka kupona?”7 Yule mgonjwa akajibu, “Bwana, sina mtu wa kuniingiza bwawani maji yanapotibuliwa. Ninapoanza kwenda bwawani, mgonjwa mwingine huniwahi akaingia kabla yangu.” 8 Yesu akamwambia, “Simama, chukua mkeka wako, utembee!” 9 Mara moja yule mtu akapona, akachukua mkeka wake, akaanza kutembea! Jambo hili lilitokea siku ya sabato.

1 Timotheo 2:1-6
Basi, kwanza kabisa, naagiza kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zitolewe kwa ajili ya watu wote: 2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi maisha ya utulivu na amani, tukimcha Mungu na kuwa wenye heshima kwa kila njia. 3 Jambo hili ni jema na linampendeza Mungu Mwokozi wetu 4 ambaye anapenda watu wote waokolewe na wapate kuijua kweli. 5 Maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, yaani mwanadamu Kristo Yesu, 6 aliyejitoa mwenyewe kuwa fidia kwa ajili ya wote. Yeye ni uthibitisho wa mambo haya, uliotolewa kwa wakati wake.

Yakobo 4:7-10
7 Kwa hiyo, jinyenyekezeni kwa Mungu . Mpingeni shetani, naye atawakimbia. 8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia. Takaseni mikono yenu, ninyi wenye dhambi; na takaseni mioyo yenu, ninyi wenye nia mbili.9 Huzunikeni, ombolezeni na kulia. Kicheko chenu kiwe kilio na furaha yenu iwe huzuni. 10 Jinyenyekezeni mbele za

2 Petro 3:9
9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake kama watu wengine wanavyochukulia kukawia, bali yeye anawavumilia, maana hapendi mtu ye yote aan gamie, bali wote waifikie toba.

Waebrania 11:6
6 Na pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu kwa maana kila mtu anayemjia ni lazima aamini kuwa yupo na kwamba yeye huwapa tuzo wale wanaomtafuta kwa bidii.

Mathayo 11:27-30
27 Nimekabidhiwa vitu vyote na Baba yangu: na hakuna mtu amjuaye Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na mtu ye yote ambaye Mwana anapenda kumdhihirisha Baba kwake.”
28 “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jifungeni nira yangu; jifunzeni kutoka kwangu; kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu. 30 Kwa maana nira yangu ni rahisi, na mzigo wangu ni mwepesi.”

Swali #1

Zaburi 46:10
Acheni mjue ya kuwa mimi ni Mungu, Nitatukuzwa katika mataifa nitatukuzwa katika nchi.

Zaburi 145:18-19
Bwana yu karibu na wote wamwitao, Na wote wamwitao kwa uamnifu.
Atawafanyia wamchao matakwa yao; Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa.

Isaya 55:3
Tega sikio lako na uje kwangu. Sikieni na nafsi zenu zitaishi…

Waebrania 10:22
22 basi tumkaribie Mungu kwa moyo wa kweli na imani timilifu, mioyo yetu ikiwa imenyunyizwa na kuwa safi kutokana na dhamiri mbaya na miili yetu ikiwa imeoshwa kwa maji safi.

Swali #2

Yohana 14:6-7
6 Yesu akawaam bia, “Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu. 7 Kama mngekuwa mnajua mimi ni nani, mngemfahamu na Baba yangu. Tangu sasa mnamfahamu Baba yangu na mmemwona.”

1 Yohana 1:5
5 Huu ndio ujumbe tuliousikia kutoka kwake, ambao tunawatan gazia: Mungu ni nuru na ndani yake hamna giza kamwe.

Warumi 3:20-24
20 Kwa hiyo hakuna binadamu hata mmoja atakayehesabiwa kuwa na haki mbele za Mungu kwa kufuata sheria; bali sheria hutufanya tutambue dhambi.
21 Lakini sasa, njia ya Mungu ya kuwahesabia watu haki pasipo sheria, njia ambayo sheria na manabii huishuhudia, imekwisha dhihirishwa. 22 Haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa kumwaminiYesu Kristo. Mungu huwatendea hivi watu wote wamwa minio Kristo pasipo kubagua, 23 kwa maana wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;24 wote wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kwa ukombozi ulioletwa na Yesu Kristo.

Ezekiel 18:32
“Maana mimi sikufurahii kufa kwake afaye”
Asema Bwana “Mungu,basi ghairini mkaishi!”

Warumi 3:23
23 kwa maana wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;

Matendo Ya Mitume 4:12
12 Wokovu unapatikana kwake tu; kwa maana hakuna jina jingine duniani ambalo wamepewa wanadamu kuwaokoa ila jina la Yesu, na ni kwa jina hilo peke yake tunaweza kuokolewa!”

Swali #3

Yohana 6:29
29 Yesu akawajibu, “Kazi anayotaka Mungu muifanye ni hii: mumwamini yeye aliyenituma.”

Yohana 5:24
24 Ninawaambia hakika, ye yote anayesikiliza maneno yangu na kumwamini yule aliyenituma, anao uzima wa milele na hatahukumiwa. Amevuka kutoka kwenye mauti, na kuingia katika uzima.

1 Yohana 5 :10-12
10 Mtu anayemwamini Mwana wa Mungu anao ushuhuda huo ndani yake. Mtu asiyemwamini Mungu, amemfanya Mungu kuwa ni mwongo, kwa sababu hakuamini ushuhuda alioutoa Mungu kuhusu Mwanae. 11 Na ushuhuda wenyewe ndio huu: Mungu ametupatia uzima wa milele, na uzima huu umo kwa Mwanae. 12 Aliye naye Mwana anao uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana uzima.

Swali #4

Yohana 3:1-8
Kiongozi mmoja wa Wayahudi wa kundi la Mafarisayo aitwaye Nikodemo,2 alimjia Yesu usiku akamwambia, “Rabi, tunafahamu kuwa wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kufanya miujiza hii uifanyayo, kama Mungu hayupo pamoja naye.”
3 Yesu akamjibu, “Ninakwambia hakika, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona Ufalme wa Mungu.” 4 Nikodemo akasema, “Inawezekanaje mtu mzima azaliwe? Anaweza kuingia tena katika tumbo la mama yake na kuzaliwa mara ya pili?” 5 Yesu akamwambia, “Ninakuambia hakika, kama mtu hakuzaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia katika Ufalme wa Mungu. 6 Mtu huzaliwa kimwili na wazazi wake, lakini mtu huzaliwa kiroho na Roho wa Mungu. 7 Kwa hiyo usishangae ninapokuambia kwamba huna budi kuzaliwa mara ya pili.8 Upepo huvuma po pote upendapo. Mvumo wake unausikia lakini huwezi ukafahamu utokako wala uen dako. Ndivyo ilivyo kwa kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.”

Swali #5

Yohana 3:36
36 Ye yote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele; asiyemtii Mwana hatauona uzima bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake daima.”

Yohana 16:24
24 Mpaka sasa hamjaomba lo lote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapewa ili furaha yenu ipate kukamil ika.

Warumi 4:7-8
7 “Wamebarikiwa wale ambao makosa yao yamesame hewa, ambao dhambi zao zimefunikwa.8 Amebarikiwa mtu ambaye Bwana hamhesabii dhambi zake.”

Warumi 5:1
Basi, kwa kuwa tumekwisha kuhesabiwa haki kwa imani, tuna amani na Mungu kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo.

2 Wakorintho 5:17
17 Kwa hiyo mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama, mapya yamekuja.

Efeso 1:13
13 Ninyi pia mliingia ndani ya Kristo mliposikia neno la kweli, Injili ya wokovu wenu. Nanyi mmemwa mini, mkawekewa muhuri na Roho Mtakatifu ambaye mliahidiwa.

Waebrania 13:5
5 Maisha yenu yasitawaliwe na tamaa ya kupenda fedha, na mridhike na mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, “Sita kupungukia kamwe wala sitakuacha.”

Waefeso 1:3-6
3 Asifiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ametu bariki sisi kwa kila baraka za kiroho zitokazo mbinguni tukiwa ndani ya Kristo. 4 Mungu alituchagua sisi tuwe ndani ya Kristo hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na lawama mbele zake. 5 Kwa upendo wake, alipanga kabla ya mambo yote, kutufanya sisi kuwa watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo kwa mapenzi yake mwenyewe; 6 na hivyo apewe sifa kwa ajili ya neema yake tukufu ambayo tumepewa bure katika Mpendwa wake.

Wafilipi 3:8-9
8 Zaidi ya hayo, nahesabu mambo yote kuwa hasara tupu yakilinganishwa na faida kubwa ninayopata kwa kumjua Kristo Yesu aliye Bwana wangu. Kwa ajili yake nilikubali kupoteza kila kitu na kuona mambo hayo yote kuwa ni takataka ili nipate faida ya kuwa na Kristo; 9 na nikiwa kwake nisionekane kama mtu mwenye haki yake mwenyewe, inayotokana na kushika sheria, bali niwe na ile haki inayotokana na kumwamini Kristo, ambaye yeye ni haki itokayo kwa Mungu inayopatikana kwa imani.

 
 

 

The Guide has her own Guidebook to help her lead and guide the lesson.

Download Swahili Lesson #5 Guidebook

Download Swahili Guidebook Bible Verses Lesson #5

JE MUNGU YUKOJE?

Mistari ya Biblia

 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us