Project Hope     home >> stonecroft>> mwongozo >> somo 2 >> mistari ya biblia
Mistari ya Biblia - Somo #2
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club
Je Mungu yukoje?

Mistari ya Biblia

Usomaji wa Biblia wa kila juma

1 Wakorintho 1:9
9 Mungu ni mwaminifu ambaye aliwaita muwe na ushirika na Mwanae, Yesu Kristo, Bwana wetu.

Warumi 16:27
27 Mungu aliye pekee mwenye hekima, atukuzwe milele na milele kwa njia ya Yesu Kristo! Amina.

Luka 1:37
37 Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilo wezekana.”

Yohana 3:16
16 “Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu kiasi cha kumtoa Mwanae pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Hesabu 23:19
19 Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?

Ufunuo 15:3-4
3 Nao waliimba wimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu na wimbo wa Mwana-Kondoo wakisema, ‘ ‘Matendo yako Bwana Mungu Mwenyezi, ni makuu na ya ajabu! Njia zako wewe Mfalme wa Mataifa ni za haki na za kweli! 4 Ni nani asiyekucha wewe Bwana na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako ni mtakatifu. Mataifa yote yatakuja na kukuabudu kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha dhihirishwa.”

Ufunuo 1:8
8 “Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu, “Aliyeko na aliyekuwako na ata kayekuja, Mwenyezi.”

Wakolosai 1: 15-16
15 Kristo anafanana kabisa na Mungu asiyeonekana. Yeye ali kuwepo kabla Mungu hajaumba kitu cho chote. 16 Yeye ndiye ali yeumba vitu vyote mbinguni na duniani; vitu vinavyoonekana na visivyoonekana; kama ni viti vya enzi au nguvu, au watawala au milki na mamlaka: vyote viliumbwa na yeye kwa ajili yake.

Swali #2

Yohana 4:24
24 Mungu ni roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”

Warumi 11: 33-36
33 Jinsi utajiri wa Mungu ulivyo mkuu! Hekima yake na maarifa yake hayana mwisho. Njia zake na maamuzi yake hayachu nguziki! 34 Kwa maana ni nani amepata kufahamu mawazo ya Mungu au kuwa mshauri wake? 35 Au ni nani amewahi kumpa cho chote ili arudishiwe? 36 Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake na vipo kwa ajili yake na vyote vinadumu kwake. Utukufu ni wake milele. Amina.

Swali #3

1 Yohana 4:8
8 Mtu asiye na upendo hamjui Mungu; kwa maana Mungu ni upendo.

2 Tesalonike 3:3
3 Lakini Bwana ni mwaminifu. Ata waimarisheni na kuwalinda kutokana na yule mwovu.

Yakobo 1:17
17 Kila kipawa chema na kila zawadi kamilifu hutoka mbinguni, ikishuka kutoka kwa Baba wa nuru za mbinguni ambaye habadiliki kama kivuli.

Marko 10:18
18 Yesu akamwambia, “Mbona unaniita mwema? Hakuna ali yemwema isipokuwa Mungu peke yake.

Waebrania 1:8
8 Lakini kuhusu Mwana, anasema: “Kiti chako cha enzi, Wewe Mungu, kitadumu milele na milele, na haki takuwa fimbo ya ufalme wako.

Luka 1:78 - 79
78 kwa ajili ya wingi wa rehema za Mungu wetu. Nuru ya jua itatujia kutoka mbinguni na

1 Petro 1:15-16
15 Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, kadhalika ninyi muwe watakatifu katika mwenendo wenu;16 maana imeandikwa: “Muwe watakatifu kwa sababu mimi ni mtakatifu.”

SIFA ZA MUNGU

1 Yohana 4: 7-16
7 Wapendwa, tupendane, kwa sababu upendo hutoka kwa Mungu. Mtu mwenye upendo amezaliwa na Mungu na anamjua Mungu. 8 Mtu asiye na upendo hamjui Mungu; kwa maana Mungu ni upendo. 9 Na hivi ndivyo Mungu alivyoonyesha upendo wake kwetu: alimtuma Mwana wake wa pekee ulimwenguni ili kwa ajili yake sisi tupate kwa kupitia kwake. 10 Na huu ndio upendo: si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi hata akamtuma Mwanae awe sadaka ya kulipia dhambi zetu.11 Wapendwa, kwa kuwa Mungu ali tupenda kiasi hicho, sisi pia tunapaswa kupendana. 12 Hakuna mtu aliyepata kumwona Mungu; lakini tukipendana, Mungu anaishi ndani yetu, na upendo wake unakamilika ndani yetu.
13 Tunajua ya kwamba tunaishi ndani yake na yeye anaishi ndani yetu kwa sababu ametupatia Roho wake. 14 Na sisi tumeona na kushuhudia kwamba Baba amemtuma Mwanae awe mwokozi wa ulim wengu. 15 Kila mtu anayekiri kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, na yeye hukaa ndani ya Mungu. 16 Kwa hiyo tunajua na kutegemea upendo alio nao Mungu kwetu sisi. Mungu ni upendo, na mtu mwenye upendo hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake.

Waefeso 2: 4-5
4 Lakini Mungu, ambaye ana huruma nyingi, kutokana na upendo wake mkuu ambao alitupenda nao, 5 japokuwa tulikuwa bado tumekufa kiroho kwa sababu ya makosa yetu, alitufanya tuwe hai pamoja na Kristo Yesu. Mmeokolewa kwa neema.

GOD IS FAITHFUL

Kumbukumbu la Torati 7:9
Basi jueni ya kuwa BWANA Mungu wenu Ndiye Mungu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wale wampendao, na kushika amri zake hata vizazi elfu.

Zaburi 92:1-2
Nineno jema kumshukuru BWANA ,
Na kulumbia jina lako, ee uliye juu,
Kuzitangaza rehema zako asubuhu
Na uaminifu wako wakati wa usiku.

GOD IS UNCHANGING

Malaki 3:6
Kwa maana mimi BWANA sina kigeugeu;
Ndio maana ninyi hamku angamizwa ninyi wana wa Jakobo.

GOD IS GOOD

Zaburi 107:1
1 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.

GOD IS JUST

Torati 32:4
4 Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.

GOD IS MERCIFUL

2 Wakorintho 1:3
3 Ashukuriwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa huruma na Mungu wa faraja zote.

GOD IS HOLY

1 Samweli 2:2
Hakuna aliye mtakatifu kama Mungu,
Kwa maana hakuna yeyote ila wewe,
Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu.


Zaburi 99:9
Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu; Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu;Maana BWANA, Mungu wetu, ndiye mtakatifu.

Swali #4

1 Petro 1:13-16
13 Kwa hiyo, ziandaeni nia zenu, muwe na kiasi, wekeni tumaini lenu lote katika neema ile mtakayopewa wakati ule Yesu Kristo atakapodhihirishwa.14 Kama watoto watiifu, msikubali kutawaliwa na tamaa mbaya mlizokuwa nazo wakati mkiishi katika ujinga. 15 Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, kadhalika ninyi muwe watakatifu katika mwenendo wenu;16 maana imeandikwa: “Muwe watakatifu kwa sababu mimi ni mtakatifu.”

1 Wakorintho 1:30
30 Mungu ndiye chanzo cha uhai wenu ndani ya Kristo Yesu. Amemfanya yeye kuwa hekima yetu, haki yetu na utakaso na ukombozi

Yeremia 9:23-24
23 Bwana asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake;
24 bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema Bwana

Swali #5

Mathayo 28:20
20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

Mwanzo 17:1
Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.

Hebrews 4:13

 

 
 

The Guide has her own Guidebook to help her lead and guide the lesson.

Download Swahili Lesson #2 Guidebook

Download Swahili Guidebook Bible Verses Lesson #2

JE MUNGU YUKOJE?

Mistari ya Biblia

 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us