Project Hope     home>> mwongozo >> somo 1 >> somo 2
Mwongozo Somo #2
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

SOMO LA PILI (2)
MUNGU ANA MW ONEKANO GANI?

LENGO LA SOMO
• Kugundua Mungu ambaye haonekani yukoje.
• Kuelewa jinsi ya kumjua yeye vizuri.
• Kujua na kutambua umilele wa Mungu ,na utakatifu wake.

MAOMBI
Mungu wa milele, tunakuabudu wewe,. Tumejifunza kuwa wewe huna Mwanzo wala huna mwisho. Tunatambua kabisa kuwa wewe ndio muumbaji wa kila kitu kinachoishi. Tusaidie jinsi ya kukufikiria vizuri wewe tunaposoma neno hili. Tunaomba katika jina la Yesu ………..AMEN

MAONI YA UONGOZI
Unaweza ukawa umesikia kuhusu mwalimu mmja ambaye alijikita katika picha aliyokuwa akiichoara:

“Unacora nini, Amina?” aliuliza.

“Ninachora picha ya Mungu” alijibu.

“Lakini, Amina,” mwalimu aliitikia, “hakuna, mtu anaye jua Mungu alvyo”.

“Watajua pale nitakapo maliza kuchora picha yangu hii,” Amina alijibu.

Hatutakiwi kuchora picha katika somo la leo, bali kinachotakiwa ni kuwa na neno la Mungu kwa kufikiria kuwa hivi Mungu yukoje.

1. Kwa kutumia maneno machache, elezea ni nini unachokiona ukifikiri kuhusu Mungu? Kuwa mkweli na sahihi unafikiri nini kuhusu Mungu. Mwisho mwa somo hili, hili Sali litaulizwa tena. (Sisitiza kila mtu aweze kushiriki.)

Fahamu zetu, sio kubwa kiasi kwamba tukamwelewa Mungu. Yeye hayuko kama sisi hivi tulivyo. Hakuna kitu ambacho tunaweza kulinganishwa nay eye. Hata kile tunachokifikiri kuhusu Mungu hakioneshi jinsi Mungu alivyo.

Nini tunachofikiri kuhusu Mungu ni kitumuhimu sana kwetu sisi.

Ili kufikiri vizuri kuhusu Mungu , inatakiwa sisi tuache kufikiri kuwa Mungu ana mwili kama wa kwetu hivi ambao unaweza ukaonekana. Tukiwa na mawazo kama hayo yana weka ukomo wa kuweza kumwelewa Mungu kiundani zaidi.

Mungu hayupo kama sisi wanadamu hivi tulivyo, vitu vini ambavyo tunavyo sisi vinatofautiana sana na vyake, kwa mfano tabia, maadili yake, n.k. hatuwezi kumfahamu yeye mpaka yeye mwenyewe aongee na sisi kuhusu yeye.

Biblia ndio chanzo kikuu kuhusu taarifa, za Mungu. Yeye anataka sana tuweze kumfahamu yeye, kwa hiyo amekuwa akijifunua sana ten asana kuhusu yeye mwenyewe hasa kwa kupitia Biblia.

Sasa tutazungumzia nini tulichhokisoma kuhusiana na Mungu kutoka katika maosmo mya Biblia.

Kila mtu achague mstari wa kujisomea na asome kwa sauti.

KUJISOMEA BIBLIA KWA JUMA

(Use your Bible or Africa Bible Verse Handbook)

Kila siku katika wiki hii, soma mistari ya Biblia, kwa siku kutoka katika agano jipya, na ueleze kila kifungu kinasema nini kuhusu Mungu.

1 Wakorintho 1:9…….. (Mungu anatakiwa kuaminiwa)

Warumi 16:27……. (Ni mmoja tu ambaye ni mwelewa zaidi)

Luka 1:37……… (Hakuna jambo ambalo hawezi kulifanya)

Yohana 3:16……. (Alitupenda sisi na kutupatia mwanae kufa kwa ajili yetu, ili tupate na tuwe na uzima wa mmilele)

Hesabu 23:19……… (Yeye sio mwanadamu, hata aseme uongo, anafanya chochote anachotaka kufanya)

Ufunuo 15:3-4……… (Mungu ni mtakatifu, kweli. Mataifa yatakuja kusujudu yeye kwa sababu ya haki na kazi yake kubwa )

Funuo 1:8……… (Ni wa milele. Yeye ni Mwanzo na mwisho)

Chgua mstari ambao wewe kwako una maana sana kutoka mistari tuliyosoma hapo juu. Fikiria kuhusu ukweli huo una maanisha kwako binafsi na uweze kuutumia ndani ya maisha yako.

Je mstari uliuchagua umefanyiaje mazoezi ?..........Je uliatiri vipi wiki yako? Tuambie nini kilitokea…………

Rudi katika aganoo jipya, soma wako; Losai 1:15-16……… Inasema nini kuhusu Mungu? Katika mstari wa 15 unasemaje kuhusu Mungu?.......(Mungu haonekani)

Mungu hana mwili kama wa kwetu. Fikra zetu zina makosa mengi sana, pale tunapofikiri kuwa Mungu yuko kama sisi, au ana ukomo kama sisi. Ukiangalia sisi hatukujiumba, wala hatukuamua sisi kwamaba tuanze kuishi, pia tunatakiwa tujiulize je tuliumba nywele, chakula?, au maji? Ambavyo hivi vinafanya maisha yetu yasonge mbele. Pia Mungu yeye ni mkamilifu yeyey kama alivyo. Yeyey hata msaada hataki kwa kuwa yeye ndio kila kitu.

Kila kitu tunachokiona katika dunia hii kilumwa au kilitengenezwa. Lakini Mungu hakuumbwa, wala hakujtengenezwa. Mungu ni wa tofauti katika kila kitu. Jina lake ni NIKO. Yeye yupo na atakuwepo milele yote. Yeye hatakuwa na mwisho wowote ule.

Utofauti mwingine ambao tunatofautiana na Mungu ni kwamba sisi ni binadamu nay eye ni Mungu. Kwa hiyo sisi ni vitu vinavyoonekana.

Swali la pili linatuambia vitu vingine zaidi kuhusu Mungu.

2 . Katika Yohana 4:24 inasema nini kuhusu Mungu?.........(Mungu nni Roho)

Mungu hana ukomo. Yeye ni Roho na anaweza kuwa mahali opote na kwa muda huohuo.
Biblia inatufundisha kuwa Mungu hana ukomo yeye ni wa milele.

Mistari mingi sana ndani ya Biblia inatuambia kuhusu hili. Mingi mistari imetolewa katika kitabu cha kujifunzia (Unaweza ukamweleza mtu ili aweze kusoma mistari hiyo)

MUNGU WETU HANA UKOMO
Sulemani alioma,

“Lakini Mungu je? Atakaa, kweli kweli juu ya nchi? Tazama, mbingu za mbingu semmbuse nyumba hii niliyojenga!” - 1 Wafalme 8:27.

Je wewe waweza kuvumbua ukuu wa Mungu?
Waweza kufikiria upeo wa huyo mwenyezi?
Ni juu mno kama mbingu; waweza kufanya nini wewe?
Ni wenye kina kuliko kuzimuni; waweza kujua nini wewe?
Cheo chake ni kirefu kuliko dunia, ni kipana zaidi ya bahari. - Ayubu 11:7-9.

YEYE NI ZAIDI YA UFAHAMU WETU

“Mungu huunguruma kwa kustaabisha kwa sauti yake; hufanya mambo makuu, amabyo hatuwezi kuelewa nayo. - Ayubu 37:5

“Maana mawazo yangu si mawazo yenu,
wala njia zenu si njia zangu; asema bwana.
Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi,
kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu,
na mawazo yangu kuliko mawazo yenu”. - Isaya 55:8-9.

Ufahamu wetu sisi una ukomo lakini wa Mungu hauna ukomo. Sisi ni wenye dhambi, yeye hawezi tenda dhambi, yeye ni mkamilifu katika kila njia. Yeye ni mkuu t hata tusengenye vipi.
Katika agano lako jipya rudi katika Warumi 11:33-36………

Biblia inazungumzia kuhusu mfalme au bwana. Zaburi 145:5 inasema “Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako, na Matendo yako yote ya ajabu”.

Fahamu zetu haziwezi kuwa na Mungu kwa kuwa yeye han a ukomo. Kw ahiyo kuhusu siri ya Mungu kwetu kwa sababu ya ukomo wetu katika mambo mengi hatuwezi kuelewa Mungu maana yeye hana aukomo. Kwa hiyo tunaweza kupokea vitu ambavyo hatuvielewi kwa imani ambavyo Mungu anasema, kwa sababu tuna kitu cha kuangalia ambacho ni Biblia. Mungu alitupatia kitabu ili tukitumie katika kumwellewa kuwa yeye ni nani.

3. Sifa ya uungu ya Mungu ni sifa bora sana ambapo ndio tunatambua ukweli wa Mungu. Katika kila mtari wa Biblia ufuatao unaambatanisha siafa ya uungu ya Mungu ndani yake. Soma mistari hiyo na uandike sifa katika kila mstari.

a. 1 Yohana 4:8…….. (Upendo)

b. 2 Wathethalonike 3:3……… (Mwaminifu)

c. Yakobo 1:17……… (Habadiliki)

d. Marko 10:18……… (Mwema)

e. Waebrania 1:8……… (Haki ya milele)

f. Luka 1:78……… (Mwenye huruma)

g. 1 Petro 1:15-16……… (Mtakatifu)

Ukutaka kujua zaidi kuhusu Biblia inasemaje kuhusu sifa hizi za Mungu, rudi katika baadhi ya kurasa katika agano jipya ili ujue vizuri kuhusu hili.

SIFA ZA MUNGU

MUNGU NI PENDO

Upendo ni sifa ya Mungu, lakini sio ufafanuzi wa Mungu. Mungu anafafanua upendo sio upendo unamfafanua Mungu. Hii inaonyesha tu jinsi Mungu alivyo.

Uaminifu, wema, huruma haki vyote hivi vinamwakilisha Mungu. Yeye yupo katika hivi lvitu tulivyovitaja. Upendo wa Mungu mara zote ni mtakatifu. Na mara zote umekuwa mwema, mwamnifu, na wa haki.

Hatuelewi namna sahihi ya kuelezea upendo,lakini tunaelewa upendo umefunuliwaje.upendo hutamani kutenda mema daima na wala hautaki baya limKumbe yeyote.upendo hutoa vyote bule kwa aliyependwa ,na Mungu hutupenda sisi sote mmoja mmoja.

Upendo ndio unaowafanya wakristo kuwa wa tofauti kwa kuwa upendo huo huwa unaleta mabadiliko ambayo ni chanya. Ambapo kama ni upend waMungu upo kwa kila mtu Yule aliye ndani ya kristo kwa hiyo atakuwa tofauti na watu ambaohawako nadni ya kristo.

Soma katika 1 Yohana 4:7-16……….

Ni vizuri kusoma zaidi kuhusu upendo wa Mungu . Soma katika Waefeso 2:4 -5……….

MUNGU NI MWAMINIFU

Tunaweza kumtegemea Mungu kwa kuwa Mungu ni mwaminifu. Anatimiza ahadi zake.tunaweza kuishi katika tumaini kwa maisha ya baadae kwa kuwa uaminifu wa Mungu haushindwi.

Tunapozungumzia uaminifu wa Mungu , tunaona umoja wa sifa zake. Tunaweza kusema kuwa sifa za Mungu zinaelezeana kila moja inaeleza sifa ya mwenzake. Tunaweza kusema kuwa kila sifa ya Mungu inaelezea nyenzake na kuvumvua ukamilifu wa Mungu.
Kutambua kuwa agano la kale linasemaje kuhusu uaminifu wa Mungu soma katika kitabu cha kumbukumbu la Torati 7:9 na Zaburi 92:1-2………….

MUNGU HABADILIKI

Kati ya sifa za Mungu ni kuwa yeye habadiliki. Tunatambua ya kua Mungu hawezi kuwa sio mwamifu kwa sababu angekuwa sio mwaminifu ingembidi yeye kubadilika. Mungu ni mkamilifu. Hawezi kushindwa hata siku moja.

Soma Malaki 3:6……

Sifa nyingine ni wema. Tunajua kuwa ili kuwa mwema zaidi ni kuwa mkarimu, mpole, mwenye maadili mazuri, mwenye upendo, na mtakatifu. Tunaelewa ubora wa wema kwa sababu kuna muda mwingine tunaweza kuona kuwa sisi kama sisi ni wema .

MUNGU NI MWEMA

Wema wa Mungu ni tofauti na wema wa mwanadamu, kwa sababu Mungu ni mkamilifu kila eneo.” Mungu peke yake ndio mwema”

Soma Zaburi 107:1...…

MUNGU NI WA PEKEE

Mungu yeye pekee amejikamilasha, na hawezi kuwa kitu kingine. Yeye ni wa pekee. Soma katika kumbukumbu la Torati 32:4………

Hakuna kitu katika haki ya Mungu ambacho kinachomzuia yeye kwamba asiwe mwenye huruma. Sifa zake zote hazifarakani.

MUNGU NI MWENYE HURUMA

Huruma na sifa ya Mungu. Yeye ni Mungu mwenye huruma sana na ni Mungu wa haki sana. Mungu aluwa mwenye huruma tangu Mwanzo .

Hata katika kutenda haki,yeye ni mwenye huruma,mara zote anaposhughulika na mwana damu huonyesha upedno wa hali ya juu sana,Upendo upitao sio tabia ya muda mfupi ya Mungu bali ndiyo alivyo ,Mungu alikuwa ni mwenye huruma hata kabla saa hazijakuwepo na mwenye huruma hata leo hii.

Soma 2 Wakorrintho 1:3………

MUNGU NI MTAKATIFU

Mungu yeye hana uhafu wowote yaani yeye ni msafi sana, na mwenye maadili ya hali ya juu sana.

Kwa sababu Mungu ni mtakatifu, kwa hiyo hata sifa zake pia ni takatifu. Kwa hiyo kila kitu tunachofikiria kinachohusuiana na Mungu, Mungu inatakiwa tufikiri kuwa ni kitakatifu.

Biblia inasema nini kuhusu utakatifu? Soma 1 Samweli 2:2 na Zaburi 99:9

4. a. Mungu anategemea nini kutoka kwa wakristo?
1 Petro 1:13-16……… (Kuwa watakatifu katikakila kitu tunachokifanya)

b. Kulingana na 1 Wakorintho 1:30, tunawezaje kuwa watakatifu?........ (Kwa kukaa na Mungu kupitia Yesu kristo)

Tunajua ya kuwa sisi sio watakjatifu na hatuwezi kuwa watakatifu kama Mungu alivyo. Lakini tunapompokea Yesu kristo, tunapokea kila kitu ambacho Mungu yuko. Katika 1 Wakorintho 1:30 tunaambiwa ya kwamba kristo ambaye yupo ndanni yetu ni hekima yetu, na utakatifu. Tunakuwa karibu na Mungu na ana tuweka huru. Kristo ndiye mtakatifu wetu.

Kuna mistari miwili yenye nguvu katika Yeremia 9 ambayo ni muhimu kwa maisha haya ya kila siku

Bwana asema hivi, "Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, Wala mwenye nguvu aijisifu kwa sababu ya nguvu zake, Wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wak; Bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, Ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni bwana nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; Maana mimi napendezwa na mambo hayo," asema Bwana. - Yeremia 9:23-2

Tumeshaanza kuona jinsi gni Mungu Mungu alivyo.

SIFA TATU (3) ZA KIPEKEE

Mungu ana nguvu zote. Aliumba ulimwengu huu na kila kitu kilichomo ndani yak e kwa kuongea tu. Na anatawala vyote. Ana nguvu ya kufanya miujiza. Kwa hiyo tuna sema kuw aMungu nijalali (yaani anaweza kufanya lolote atakalo).

Mungu anajua kila kitu katika ulimwengu huu. Hakuna kitu ambacho tunaweza kusema uwa hakijui. Nguvu ya Mungu na maarifa yake hayatengani. Hii tunaita omniscience (yaani utu).

Mungu yuko kila mahali na kwa muda mmoja. Yeye anapatikana karibu kila eneo au kila sehemu muda wote. Tunasema kuwa Mungu yupo kila mahali (omnipresent).

 

5. Soma mistari ifuatayo ya Biblia na uandike sifa hizo tatu za Mungukila sehemu ya mstari utakao soma. Maana mistari hiyi inaonesha omnipotence, omnipresent na omniscience.

Mathayo 28:20………………...….. (Omnipresence)

Mwanzo 17:1; 18:14………………..(Omnipotence)

Waebrania 4:13…………………….(Omniscience)

MUHTASARI
Kwa kile tulichokijadili katika somo la 1 na somo la 2, oredhesha maneno yanayomwelezea Mungu. Unaweza kuandika maneno yafuatayo katika ukuras aambao upo wazi mwisshoni mwa somo hili.

Maneno yanayomwelezea Mungu
Roho

Yupo kila mahali- omnipresent

Ni zaidi ya ufahamu wetu

Mwaminifu

Hana ukomo

Mtakatifu

Ana nguvu zote- omnipotent

Mwenye huruma Habadiliki

Anajua kila kitu- omniscient

Mwenye haki

A.W. Tozer muandishi maarufu sana,”Mungu tunae paswa kumjua ana nguvu za ajabu sana na yupo mbinguni,Mungu baba muumba wa Mbingu na nchi,Mungu mwenye hekima na mkombozi.

Yeye ndie akaaye katika mzunguko wa ulimwengu,yeye akunjuaye mbingu kama hema.
Je umeanza kuelewa kuwa Mungu ni nani? Je unahisi utakatifu wake, usafi, na hekima yake? Je unaweza ukathibitisha kuwa yeye hana ukomo?

Katiak somo la tatu na la sita andika mwenyewe maombi ya kufungia baada ya masomo yako, hii itakusaidia wewe ili kupeleka haja zako mbele za Mungu na kumwomba Mungu katika kila jambo wewe utakalo litaka. Maombi yako binafsi hayatasomwa au kushirikishwa katika kundi itakuwa ni siri yako.

MAOMBI
Mungu mwenyezi, asante kwa hiki tulichokisoma. Asante Mungu kwa kuwa upo kila mahali, na kwamba una nguvu zote, na unajua kila kitu. Wewe ni Mungu wetu mwema. Tuna furaha kwa kuwa wewe unatupenda na una tulewa sana. Tunakusifu wewe kwa Baraka zako zote. Katika jina la Yesu kristo……….AMEN

MAELEZO
_______________________________________________________________

_______________________________________________________________


 
 

 

This is a translation of 'What is God like?' Stonecroft's Guide Book Lesson #2 in Swahili, the English version of What is God like? is available online from Stonecroft's website.

In this fresh, engaging study, you will meet the Creator of life and the Sustainer of all things. As you study God's eternal characteristics, you will learn that He is majestic, all-powerful, holy, faithful, and just.

As you explore together what the Bible tells us about God, you'll also learn how to decide for yourself who He is and how He interacts with people. (6 lessons)

The Guide has her own Guidebook to help her lead and guide the lesson.

Download Full Guidebook

Download Lesson #2 Guidebook

Download Guidebook Bible Verses Lesson #2

Mwongozo Utakaotuongoza

 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us