Project Hope     home>> mwongozo >> somo 2 >> somo 3
Mwongozo Somo #3
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

SOMO LA TATU (3)
MUNGU YUKO WAPI?

LENGO LA SOMO
• Kanza kuelewa zaidi kuwa Mungu yuko wapi na anafanana na nini.
• Kutambua ukaribu wa Mungu na mwendelezo wa uwepo wake.
• Kutambua utayari wake kutujibu pale tunapomwita.

MAOMBI
Mungu mwenyezi, tunataka kujifunza zaidi kuhusu wewe.Tusaidie kuelewa vitu tunavyovisoma katika neno lako kila siku. Tunatamani kujua kuwa wewe uko wapi pale tunapokwita wewe. Tunaomba katika jina la Yesu…….AMEN

MAONI YA UONGOZI
Somo ,hili litaongoza ufahamu wetu, tunapoendelea kusoma kuw a Mungu yeye ni nani na anafanana na nini.

Ukuu wake uko juu zaidi ya ufahamu wetu. Ufahamu wa mwanadamu hauwezi hata kidogo katika kufanana na ule ukuu wa Mungu. Mungu ameumba kila kitu ambacho kipo hapa duniani.

Kila siri yiliyopo Mungu kaumba, hata dakika moja katika seli ya mwanadamu,ni zaidi ya ufahamu wetu.je ni namana gani mwana damu wa kawaida akaanza kumwelewa Mungu ambaye yeye aliumba kila kkitu kilichpo hapa duniani? Kwa kweli Mungu ni wa ajabu sana nay eye ndiye anaye jua yote.

Kwa hiyo siri mojawapo Mungu anataka sisi tumjue yeye na inawezekana kabisa. Kumjua Mungu sisi I rahisi sana kwa sababu anaonekana kwetu sisis nasi tunamfahamu kwa kupitia neno lake ambalo lipo ndani ya bibl;ia. Jinsi unavyokazana kusoma Biblia ndiyo hivyo hivyo Mungu unamfahamu zaid..jinsi tutakavyoweza kumjua yeye Mungu kuwa ni nani ndivyo hivyo amabavyo tutajenga ukaribu nay eye sana na mkumjua zaidi.

Katika vifungu vya Biblia vya kjusoma katika wiki vimeeleza kabisa kuwa Mungu yuko wapi.

KUJSOMEA BIBLIA KWA JUMA

(Use your Bible or Africa Bible Verse Handbook)

Kila siku katika wiki hii, soma vifungu vya Biblia kwa siku na ujibu maswali.

Zaburi 34:18
Mungu yuko wapi pale unapomhitaji?....
(Mungu yuko karibu na watu waliovunjika mioyo.)

Zaburi 193:19
Kiti cha enzi cha Mungu kiko wapi?
(Kiti cha enzi cha Mungu kiko mbinguni.)

Zaburi 145:18
Mstari huu unatuam,bia nini kuhusu Mungu?
(Mungu anasikia pale tnapomwita, kwa ajili ya mahitaji yetu.)

Isaya 37:16
Mstari huu unasema Mungu anakaa wapi?
(Mungu anakaa katikakati ya makerubi.)

Isaya 40:22
Mstari huu unatuambia nini kuhusu kuwa Mungu yuko wapi?
(Mungu anaishii au anakaa juu ya dunia, mbinguni.)

Isaya 43:2
Mungu anakuwa wapi wakati uko kwenye matatizo?
(Mungu yuko karibu na kila mtu. Hayuko mbali, ila tunashindwa kumtambua yeye.)

Chagua mstari ambao unaona kwako una maana sana kutoka katika mistari iliyosomwa katika wiki hii. Jiulize mstari huo ulivyo na maana kwako wewe kama wewe na utumie katika maisha yako?

Karibu kila mstari tuliosoma hapo aw3ali unatoka katika agano la kale. Angalia katika agano jipya linasema nini kuhusiana na kwamba Yesu yuko wapi, angaliakatika swali la kwanza.

1. Mungu anaishi wapi?
1 Timotheo 6:16……….
(Anaishi katika nuru amabko hakuna mtu anayeweza kumfikia)

Mungu kumfikia inakuwa ni ngumu kwa sababu ya nuru yake na utukufu wake ulivyo juu zaidi. Lakini Mungu ni mwema sana alipogundua kuwa hatuwezi kuishi katika maisha ya mazuri nay a kumpendeza yeye aliamua kujifunua katika jnjia rtofauti amabyo tunaweza kumwelewa. Kwa mfano, jina lake linaonesha tabia yake na utu wake. Tunajifunza jinsi ya kuwa karibu na Mungu kwa kupitia kitabu alichotuandikia ambacho ni BIBLIA.

2. Biblia inasemaje kuhusu sehemu ambapo Mungu haishi?

a. Matendo 17:24-25……………..
(Mungu haishi kwenye majengo yaliyojengwa na binadamu)

b. 1 Wafalme 8:27………………….
(Mbinguni na katika kila eneo….”mbingu za mbingu”. Sio kubwa kwake yeye!)

Biblia inatuambia kuwa Mungu hana ukomo, kjwamba aishi katika majengo au mbinguni. Kwa mujibu wa Biblia hatutakiwi kusema kwamb a Mungu anaishi kama sisi tunavyotaka aishi au manaishi kwa matakwa yetu hapana tunatakiwa tusifkiri hiyo.

Uwepo wa munu mumetawala dunia yote, mbingu yote, na katika maeneo yote. Kwa kuwa eneo aliloliumba halina mwisho, basi tunajua ya kwamab anaweza akawa hata zaidi ya hapo . Je hicho kinatusaidia kujua jinsi Mungu alivyo mkuu kwetu?

Munu yuko pamoja na sisi, iwe tunafahamu au hatufahamu, mara nyingi anatulinda pamoja na mali zetu, anatuokoa kutoka katika hatari wakati hata hatutarajii kwamba hiki au kile kitatoklea.

Sulemani mfamle wa Israeli alijenga hekal kwa ajili ya Mungu lakini akagundua baaae kuwa Mungu anaweza akawa haishi humu yeyey yupo mahali popote pale. Kwa hiyoo yeye jingo halimzuii.Yupo kila mahali, lakini mambo yote nhayatimiliki katika kiwango sawa.

“ hakai duniani kama anavyofanya mbinguni, au kwa wanyama kama kwa wanadamu, kwa viumbe hai au visivyo hai, kwwa wasiowatakatifu au watatkatifu, au katika kanisa kama afanyavyo katika kanisa”

3. Kama Mungu anaishi sehemu ambayo hatuwezi kufikia na sio katika kanisa au jingo je katika 1 Yohana 4:12 inasema kuhusiana na kwamaba duniani anaishi wapi?......... (Anaishi katika umoja na sisi.)

Kwa kuwa kitabu cha 1 Yohana kiliandikwa kwa ajili ya wakristo “yaaani kwetu sisi” katika mstari wa 12 kinaelekeza kwa watu wale waliomwamini Yesu; wale wote walioweka tumaini lao kwake.

Soma kagtika Isaya 57:15…… Mstari huu unasema ya kwamab ingawa Mungu huwezi kumfikia aliko lakini anakuja duniani kuwatia moyo wale wote wlaio wake.Mungu yuko juu ya kila mtu.Mungu yuko kila mahali. Hakuna sehemu unaweza ukajificha kwa ke.

Soma Yeremia 23:24…….. Mungu anapenya hadi katika kila jammbo ndani ya maisha yetu. Kila eneno limejawa na uwepo wake.

Mungu yeye ndiye muumbaji wa kila kitu pamoja na historia yote. Anatuongoza mambo ya kufanya. Kwa kupitia Yesu kristo, Mungu anapatikana kwa kila mmoja anayetaka kuingia ndani yake.

4. Andika kuhusu muda ule ambao ulikuwa na ,ufahamu au utambuzi kuhusu uwepo wa Mungu au kama kuna muda amabao ulikuwa na utambuzi kuwa Mungu kuna kitu cha muhimu sana kwako alikuwaanafanya. ……

Mungu anataka kutufahamisha ukweli kuhusu yeye kwetu sisi. Anaruhusu maswala Fulani kujtokea ndani ya maisha yetu ili tuwe waangalifu. Kwa hiyo tutajua kuwa tunahitaji nguvu kubwa ndani ya maisha yetu katika ulimwengu huu ,ambao ni wa matatizo na uliojaa uozo. Maana bila Mungu hapa hatutajua kitu chochote kile.

Soma katika Warumi 1:20…………..

Mungu alijionesha sifa yake ambayo ilikuwa haionekani , yaani nguvu ya ndani, uungu wake kwa watu wote kwa kupitia uumbaji. Kwa kuelezea tu jinsi ulimwengu ulivyoumbwa ni kusema ni njia ambayo tunaweza kusema kuwa Mungu ndiuye aliyeumba dunia hii.

Pia mili kuelewa zaidi jinmsi ya kujua Mungu soma katika Warumi 2:15………..

Kitu cha muimu ambcho hata wiki iliyopita tulikizungumzia ni kuhusu omnipresence yaani Mungu yuki kila mahali. Omni maana yake ni kwamba wote “zote” kwa hiyo hili neno maana yake ni kuwa Mungu yuko kila mahali. Mungu hajadhibitiwa na eneo .Mungu yuko kila mahali maana yeye ni Roho.

5. Jinsi gani omnipresent (yaani ,Mungu kuwepo kila sehemu au kila mahali) inakutia moyo wakati magumu yanapokupata?....... (Inakuwa ni faraja yakmo kujua kuwa Mungu yuko pamoja na wewe kila muda, haijalishi ni kitu gani kinatokea. Mungu anajua nini kimetokea na kwa nini. Na pia ana uwezo wa kubadilisha mambo au kuachilia mazuri yatokee.)

Mungu ataendelea kuwepo kwa uhalisia katika maisha yetu.

6. Mistari ifuatayo ya Biblia inatoa ,uthibitisho juu ya uwepo wa Mungu. Soma mistari hiyo, alafu ukariri, mstari unaofit katika hali yako au katika eneo lako uwe msaada hata kwa mtu mwingine unayemfahamu.

Kutoka 33:14………..

Zaburi 16:11………….

Zaburi 21:6……………

Zaburi 31:20…………..

Zaburi 46:1……………

Zaburi 89:15…………….

Zaburi 139:7-12……….

Yohana 14:3……………

Kama mstari mmja wapo kati yah ii kama itakuwa ni msaada kwa mtu mmoja wapo unayemfahamu basin i vizuri ukaweza kushirikiana naye huyo mtu ilia pate faraja.

Mungu anataka kuwa na watu wake. Mungu anajua kila kitu na anajionesha kwetu katika njia ambayo ni nzuri kwetu sisi. Yeye ni tumaini letu.

Kusema kwamba hatuko pamoja na Mungu kunakuja pale ambapo tunakuwa na uwoga na tunapokuwa na matatizo.

Mungu alipomuumba mwanadamu, alimpa uzima wa millele ndani yetu, na mtu akaanza kuishi. Hiki ndicho kilimfanya mwanadmau kuonekana wa tofauti katia uumbaji.

Soma Mwanzo 2:7………

Mpango wa Mungu ni kwamba watu wote waishi nay eye milele. Mungu aliwapa Adamu na Eva nguvu ya uchaguzi wao wakashindwa kumtii Mungu.

Madhara ya kutokumtii Mungu ni kwamba ni kifo, na kutenganishwa na Mungu. Soma katika mambo kunbukumbu la Torati 30:19……

Kwa hiyo kutokutii kwa Adamu na Eva hakubadilisha mpango wa Mungu. Mungu alikuwa ameshaandaa tayari njia ya kuwa hawa watu atawasamehe vipi. Na kwa wale watenda dhambi kuwa wasafi tena. Tukifuata vile amavyo Mungu ameandaa tutaishi milele katika ushirika na yeyena katika sehemu aliyoiandaa kwa ajili yetu sisi.

Usome 1 Yohana 2:24-25………

Unakumbuka ambapo ulichukua uamuzi wa kumkaribisha Yesu katika maisha yako? Je umetoa maisha yako kwake?Ni uamuzi sahihi ambao inatakiwa tuufanya. Mungu anataka tuwe nay eye milele yote.

Tunakwenda kuishi milele katika eneo tuliloandaliwa.Sisi ,ndio tutakaochagua kwenda au kutokwenda. Usikate tama wala usije ukaishia njiani kuhusu uamuzi uliouchukua. Mungu anataka sisi tuwe pamoja nay eye milele yote.

7. Andika maombi yako kwa Mungu kwa kuelezea uwepo wake ambao ni endelevu. Kumbuka kuwa haya maombi hayatashirikishwa katika kundi. Kwa hiyo andika maombi yako hapa:

MAOMBI
Ee Mungu wetu, wewe ambaye ,baba umejificha, amabye huwezi kufikiwa tunashkuru kwa uwezo wako. Tunaomba baba tusaidie kuendelea kujitambua mbele zako na kuweza kukufahamu wewe siku zote za maisha yetu. Tutakapokuwa tunaendelea wiki ijayo, fungua macho yetu, ili tuweze kutambua ukweli wa neno lako. Tunakuabudu wewe, katika jina la Yesu kristo…………AMEN

MAELEZO

_______________________________________________________________

_______________________________________________________________


 
 

This is a translation of 'What is God like?' Stonecroft's Guide Book Lesson #3 in Swahili, the English version of What is God like? is available online from Stonecroft's website.

In this fresh, engaging study, you will meet the Creator of life and the Sustainer of all things. As you study God's eternal characteristics, you will learn that He is majestic, all-powerful, holy, faithful, and just.

As you explore together what the Bible tells us about God, you'll also learn how to decide for yourself who He is and how He interacts with people. (6 lessons)

The Guide has her own Guidebook to help her lead and guide the lesson.

Download Full Guidebook

Download Lesson #2 Guidebook

Download Guidebook Bible Verses Lesson #2

Mwongozo Utakaotuongoza

 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us