Project Hope     home>> mwongozo >> somo 3 >> somo 4
Mwongozo Somo #4
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

SOMO LA NNE (4)
MUNGU ANANIJUA MIMI?

LENGO LA SOMO
• Kutambua kuwa Mungu anatujua sisi, kila mtu Mungu anamfahamu vizuri.
• Kuelewa kuwa upendo wa Mungu hauishi na wala haubadiliki.
• Hama ya kumwabudu Mungu na kuwa na ushirika naye.

MAOMBI
Mungu wa milele, asante kwa kutuambia kuhusu wewe mwenyewe katika bilblia. Tusaidie ili tuweze kukuamini wewe katika kila siku na klatika mahitaji yetu. Tunaomba utusaidie kuelewa kuwa wewe Mungu una mipango chanya katika maisha yetu, tunaomba katika jina la Yesu ……………AMEN

MAONI YA UONGOZI
Tunasoma biblia kwa sababu tunataka kumjua mungu. Tunataka kujua kama mungu anatujua sisi. Kumbuka kichwa cha somo letu, kinasema mungu ananijua mimi? Je unawezaje kuelezaje utofauti uliopo kati ya sisi kumjua mungu na mungu kutujua sisi?............

Kwa sisi kumjua mungu ni lazima yeye ajifunue yeye mwenyewe kwetu sisi. Sisi kumhua mungu inategemeana ni jinsi gani tunatii na kuweza kuamini na kwa kufanya hivyo atajifunua kwetu kwa kupitia neno lake. Tumekuwa na masomo mengi amabyo yalikuwa yanatufundisha jinsi mungu alivyojifunua yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa hiyo tunatambua kuwa yeye mungu anataka sisis tuweze kumjua yeye.

Siri ya kumjua mungu inatakiwa sisis wenyewe tuchukue hatua kama tunaamini katika yeye.Je anaposema kuwa anataka sisi tumjue yeye, je tunaamini anavyomaanisha? Je kuna utofauti wowote unaoonekana pale tunapomuomba kuwa ajioneshe, tujue jinsi yeye alivyo.

Mungu anatufahamu kuliko vile sisi tunavyojifahamu sisi kama sisi au jinsi anavytufahamu mtu mwingine. Munguyeye hana hata muda wa kunanza kutusoma sisi. Yeye alitujua hata kabla ya kuja hapa dunianai.yeye kama yeye alikua ameshaandaa mpango kwa ajili ya maisha yetu. Mungu anatutambua sisi mar azote. Uliposoma somo lako ulisoma Zaburi 139. Inatuambia njia nyingi ambazo mungu anatujua sisi kabla hatujazaliwa. Anajua kila kitu kuhusiana na sisi.

Katika somo la nne kwenye kitabu cha kujifunzia, katika kusoma na kujifunza biblia kwa wiki kunathibitisha kuwa mungu anatujua sisi.

KUJISOMEA BIBLIA KWA JUMA

(Use your Bible or Africa Bible Verse Handbook)

Kila siku wiki hii, soma kifungu cha Biblia, kwa wiki thibitisha kuwa Mungu anatujua sisi.

Yohana 6:37
Utakuwaje ukija kwa Yesu?...... (Hatakuacha peke yako)

Ayubu 34:21
Vitu vingapi tunavyovifany ana mujngu anaona?....... (Kila kitu tunachokifanya)

Zaburi 139:1-4
Mistari hii inasemaje ukiunganisha na jinsi Mungu anavyojua kuhusu watu wake?.......
(Anajua kila kitu kuhusu wao, hakuna kilichojificha kwake)

Mithali 15:3, 11
Unajuaje kuwa Mungu anaweza kuona mawazo yako?.......
(Biblia inasema kuwa Mungu anaona kila kitu, hata kila mioyo ya kila mtu)

2 Mambo ya nyakati 16:9
Mungu anataka kuona nini?......
(Watu ambao mioyo yao imemwelekea yeye na ina nia nay eye)

Waebrania 13:5
Ni wakati gani ambao Yesu atakuacha?.......
(Hatakuacha wewe kamwe)

Yohana 14:21
Kuna muunganiko gani kati ya pendo letu kwa Mungu na utii wetu kwake?.......
Je Mungu anajibuje au anachukuliaje?......
(Yeye anatupenda sisi na amejiweka wazi kwetu)

• Chagua mstari ambao unaona kwako una maana sana kutoka katika mistari iliyosomwa katika wiki hii. Jiulize mstari huo ulivyo na maana kwako wewe kama wewe na utumie katika maisha yako.

Ni mstari gani ambao ulikua wa maana sana kwako?....... Je uliathirir wiki yako? Tuambie nini ambacho kilitokea………

1. Hadithi katika Mathayo 18:12-14, inaonyesha kuhusu mtazamo wa Mungu kuhusu kila mtu?....... (Mungu anatafuata kile kilichotokea)

2. Waefeso 2:10, inatuambia nini kuhusu Mungu alichokifanya kwa kila mtu?........ (Mungu ana mpango mzuri wa maisha yetu, ambao anataka sisi tufanye)

Mungu anampenda kila mmoja wetu na ana mpango maalumu kwa kila mtu.

Soma katika kitabu chako cha kujifunzia, Zaburi 100:3…….. Mungu alituumba sisi. Mungu anataka kutubariki sisi na Baraka za Rohoni. Anataka tuwe na ushirika nay eye. Biblia inathibitisha ukweli kuw-a Mungu anatupenda sana sisi, anajua kila kitu kuhusu sisi, na anataka sisi tujue mpango wake juu ya maisha yetu.

3. Ninapoongeza maarifa juu ya Mungu ninajifunza vitu vifuatavyo…… (Mungu anaishi, yeye ni wa milele, ana uweza na nguvu, Mungu anajua kila kitu, yeye yupo kila mahali, yeye ana haki, hekima, mtakatifu, ni mfalme, ni wa ajabu)

4. Zaburi 139:1-18 ni uthibitisho tu kwamba Mungu yeye ana ufahamu thabiti juu ya kila mtu. Unaposoma Zaburi hii, kopi mstari unaokuletea changamoto na utoe ni mstari gani ambao unafaraja kubwa sana……

5. Soma mambi ambayo yapo katika Zaburi 139:23-24……… Andika maombi yako mwenyewe kwa kutumia mawazo yaliyopo ndani ya hiyo mistari kama maombi maalumu.

6. a. Kwa kuwa Mungu anajua kila kitu kuhusu mahitaji yako, sasa kuna kitu gani ambacho kinakusababisha uogope?
Mathayo 6:25-34…… (Hakuna kitu)

b. Mungu anataka ufanye nini na vitu unavyoogopa?
1 Petro 5:6-7…… (Mwachie Mungu ashughulike nayo)

c. Ni wakati gani ambao Mungu anajua kuhusu mahitaji yako ya kila siku?
Mathayo 6:8…… (Kabla hata hujaomba)

Sasa kwa nini tunaomba wakati Mungu anajua yote kabla hata hatujaomba? Kwa sababu Mungu yeyey anataka sisi tuweze kuongea naye.

Maombi ni kazi ambayo inaonesha kuwa Mungu sisi tunamtegemea na kupeleka mahitaji yetu. Majibu ake ndiyo yanayotupa nguvu nakujua kuwa Mungu kweli yupo na anatusikia na anajibu maombi yetu.

Kuna wakati mwingine jibu ni “ndiyo” na wakati mwingine tunaweza kugundua kuwa Mungu alishajibu kabla hatujaomba. Kuna wakati mwingine jibu ni “subiiri” kuna wakati mazingira yanaweza yasiwe rafiki kwa kutoa majibu Mungu. Kuna wakati mwingine jibu ni “hapana” kwa sababu jibu chanya linaweza likaathiri kazi anayofanya ndani ya maisha yetu.

Warumi 8:28:39 inatuambia kuhusu uimara tulionao katika kristo………

Mungu hawezi kufanya kitu kinyume na mapenzi yake. Kwa kinachohitajika hatutakiwi kuogopa ndani ya maisha yetu kwa kuwa Mungu ameshapanga juu ya maisha yetu. Kwa kuwa yeye ni mtakatifu, anajua kila kitu, ni mkamilifu, na anatupenda kwa dhati, tunajua kuwa Mungu anataka mengi mazuri kwa ajili ya watoto wake.

7. Ili kumjhua vizuri Mungu tafuta kila ahadi aliyokuahidi Mungu katoka rejea za Agano la Kale.

Zaburi 37:4-5…..
(Unapojikita kwake, ukimwamini, atakupa moyo wa hamu)

Zaburi 3:5-6……
(Jitoe kwake na yeyey atakulinda )

Yeremia 29:13……
(Tukimtafuta Mungu kwa moyo wetu wote, tutamuona)

8. Fikiria kuhusu mambo ya baadae katika maisha yako, je ahadi hizi zinawezaje kuathiri au kuandaa mabo yako yajayo?

9. Mungu ana mipango gani juu ya maisha yako ya baadae?

Soma Yeremia 29:11…….
(Anatuwazia mema na baadae yetu kuwa yenye tumaini)

Mungu anajionesha mwenyewe katika upendo wa kihalisia na wenye uthibiti. Usiwe na shaka na upendo wake. Tunaweza kujua kuwa plani yake mar azote ni njema sana.

10. Kwa kuwa Mungu anakujua wewe binafsi, amaeonyesha upendo kwa kufanya yale mabo ambayo ilikua sio rahisi kwako wewe kuyafanya.

Je Mungu alifanya nini kulingana na Warumi 5:6-9?....... (Anatuilinda kutoka kwenye dhambi na ametuokoa kutoka katika hasira ya Mungu kwetu kwa sababu ya dhambi zetu, na kwa wale ambao walikua hawamtii yeye)

11. Tunapoachiilia maisha yetu kwa Mungu yaani (omnipotent) au mwenye nguvu, kwa nini tusiwe na kujiamini kwamba sisi tuko salama katika mikono yake?

Somakatika Zaburi 147:5…… (Mungu anajua ni nini ambacho kinafaa kwetu na ana uwezo wa kutuweka sisi salama, anaona hatari ambazo hatuwezi kuziona sisi)

12. Andika maombi yako kwa Mungu kwa kuelezea uwepo wake ambao ni endelevu. Kumbuka kuwa haya maombi hayatashirikishwa katika kundi. Kwa hiyo andika maombi yako hapa:

Tutaomab kwa ajili ya somo hili na kwa upendo wa Mungu mkuu kwa kutulinda.

MAOMBI
Mungu wetu uliye juu mbinguni, tunakushukuru kwa yote na kwa kutujua sisi jinsi tulivyo. Na bado pendo lako halijapoa kwetu. Asante Mungu kwa mipango yako mizuri juu yetu. Tusaidie kufanya haya mambo tuliyosoma kuwa ni sehemu ya maisha yetu. Tunaomba katika jina la Yesu kristo…………..AMEN

MAELEZO

_______________________________________________________________

_______________________________________________________________


 
 

This is a translation of 'What is God like?' Stonecroft's Guide Book Lesson #4 in Swahili, the English version of What is God like? is available online from Stonecroft's website.

In this fresh, engaging study, you will meet the Creator of life and the Sustainer of all things. As you study God's eternal characteristics, you will learn that He is majestic, all-powerful, holy, faithful, and just.

As you explore together what the Bible tells us about God, you'll also learn how to decide for yourself who He is and how He interacts with people. (6 lessons)

The Guide has her own Guidebook to help her lead and guide the lesson.

Download Full Guidebook

Download Lesson #2 Guidebook

Download Guidebook Bible Verses Lesson #2

Mwongozo Utakaotuongoza

 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us