Project Hope     home >> stonecroft>> mwongozo >> somo 3 >> mistari ya biblia
Mistari ya Biblia - Somo #3
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

Je Mungu yuko wapi?

Mistari ya Biblia

Usomaji wa Biblia wa kila juma

Zaburi 34:18
18 Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa.

Zaburi 103:19
19 Bwana ameweka kiti chake cha enzi mbinguni, Na ufalme wake unavitawala vitu vyote.

Zaburi 145:18
BWANA yu karibu na wote wamwitao,
Wote wamwitao kwa uaminiru.

Isaya 37:16
Ee BWANA wa majeshi Mungu wa Israeli ukaae juu ya makerubi, wewe naam wewe pekeyako ndiwe MUngu wa falme zote za dunia wewe ndiwe uliye ziumba mbingui na nchi.

Isaya 40:22
Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanao kaa ndani yake huwa kama panzi, yeye ndiye azitanaye mbingi kama pazi na kama hema ya kukaliwa.

Isaya 43:2
Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawena katika mito haitakughafilisha, huendapo katika moto hauta teketea wala mwali wa moto hauta kuunguza.

Yeremia 23:23
Mimi ni Mungu aliye karibu asema BWANA mimisi MUngu aliye mbali.

Swali #1

1 Timotheo 6:16
16 Yeye peke yake ndiye asiyekufa, na ndiye aishiye katika nuru isiyoweza kukaribiwa; hakuna mwanadamu ali yepata kumwona wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina.

Matendo 17:24-25
24 Yesu na wanafunzi wake walipofika Kapernaumu, wakusanyaji kodi ya Hekalu walimjia Petro wakamwuliza, “Je, mwalimu wako hulipa kodi ya Hekalu?” 25 Petro akajibu, “Ndio, analipa.” Petro aliporudi nyumbani, Yesu akawa wa kwanza kusema, akamwuli za, “Unaonaje Simoni’ wafalme wa ulimwengu hupokea ushuru na kodi kutoka kwa nani? Unadhani kutoka kwa jamaa zao au kutoka kwa wageni?”

1 Wafalme 8:27
Lakini Mungu atakaa kweli kweli juu ya nchi, tazama mbingu hazikutoshi wala mbingu za mbingu sembuse hii nyumba niliyo ijenga?

Swali #2

1 Yohana 4:12
12 Hakuna mtu aliyepata kumwona Mungu; lakini tukipendana, Mungu anaishi ndani yetu, na upendo wake unakamilika ndani yetu.

Isaya 57:15
Maana yeye aliye juu aliye tukuka akaaye milele,ambaye jina lake ni mtakatifu asema hivi, naka mimi mahali palipo inuka palipo patakatifu, tena pamoja nay eye aliye na roho iliyo tubu an kunyeyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.

Yeremia 23:24
“…….Je sizijazi nchi mbingu na nchi? Asema BWANA.

Swali #4

Warumi 1:20
20 Tangu Mungu alipoumba ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani uwezo wake wa milele na Uungu wake, umedhihirika wazi wazi kutokana na vitu alivyoviumba. Kwa hiyo watu hawana kisingizio.

Warumi 2: 15
15 Kwa jinsi hii matendo yao yanaonyesha kwamba yale yaliyoagizwa katika she ria ya Musa yameandikwa ndani ya mioyo yao. Dhamiri zao pia hush uhudia hivyo; kwa maana mawazo yao mara nyingine huwashtaki na mara nyingine huwatetea.

Swali #6

Kutoka 33:14
Na akasema ” Uwepo wangu utaambatana nanyi name ntawapa pumziko.”

Zaburi 16:11
Utanijulisha njia za uzima;
Mbele za uso wako ziko fuiraha tele;
Na katika mkono wako wa kume mna mema ya milele.

Zaburi 21:6
Maana umemfanya kuwa Baraka za milele;
Maana wamfurahisha kwa furaha za uso wako.

Zaburi 31:20
Utawasitili na fitina za watu
Katika sitara ya kuwapo kwako;
Utawaficha katikia hema
na mashindano ya ndimi.

Zaburi 46:1
Mungu kwetu sisi ni kimbilia la karibu,
Msaada utakao onekana tele wakati wa mateso.

Zaburi 89:15
Heri watu wale waijuao sauti ya shange,
Ee BWANA huenenda katika sauti ya uso wako.

Zaburi 139:7-12
NIende wapi nijiepushe na roho yako?
Niende wapi niukimbie uso wako?
Kama ningepanda mbinguni wewe upo huko;
Ningefanya kitanda change kuzimu wewe upo.
Ningezitwaaa mbawa za asubihi,
Na kukaa pande za mwisho wa bahari,
Huko nako mkono wako utaniongoza.
Na mkono wako wa kuume utanishika.
Kama nikisema "Hakika giza litanifunika"
Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku;
Giza nalo halikufichi kitu,
Bali usiku huangaza kama mchana;
Giza na mwanga kwako ni sawa sawa.

Yohana 14:3
Baada ya kwenda na kuandaa makao kwa ajili yenu,
Nitakuja tena kuwachukua, ili jilipo mimi nanyi muwepo.

Zaburi 34:18
BWANA yu karibu nao waliovunjiaka mioyo,
Na walio pondeka roho huwaokoa.

Zaburi 103:19
BWANA ameweka kiti chake cha enzi mbingu,
Na ufalme wake umevitawala vitu vyote.

Isaya 57:15
Maana yeye aliye juu aliye tukuka akaaye milele,ambaye jina lake ni mtakatifu asema hivi, naka mimi mahali palipo inuka palipo patakatifu, tena pamoja nay eye aliye na roho iliyo tubu an kunyeyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.

Yeremia 23:24
“…….Je sizijazi nchi mbingu na nchi? Asema BWANA.

Mwanzo 2:7
BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai mtu akawa nafsi hai.

Kumbukumbu la torati 30:19
Nazishuhudia Mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea Mbele yako uzima na mauti Baraka na laana, basi chagua uzima ili uwe hai wewe na uzao wako.

1 Yohana 2:24-25
24 Mnapaswa kuendelea kuyafuata mafundisho mliyoyasikia tangu mwanzo. Kama mkifanya hivyo, mtakuwa siku zote katika Mwana na katika Baba. 25 Na hili ndilo ambalo Mwana ameliahidi kwetu sisi, uzima wa milele.

 

 
 

 

The Guide has her own Guidebook to help her lead and guide the lesson.

Download Swahili Lesson #3 Guidebook

Download Swahili Lesson #3 Bible Verses Handbook

JE MUNGU YUKOJE?

Mistari ya Biblia

 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us