Project Hope     home >>stonecroft>> mwongozo >> yesu ni nani somo 1 >> mistari ya biblia
Mistari ya Biblia - Somo #1
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

SOMO LA KWANZA

BIBLIA INASEMAJE KUHUSU YESU?

Kitabu mwongozo

Mistari ya Biblia

Matendo 9:5
5 Sauli akasema, “Wewe ni nani, Bwana?”
Sauti ikajibu, “Mimi ni Yesu, unayemtesa.

Marko 4:41
41 Lakini wao walikuwa wamejawa na hofu wakaulizana, “Ni nani huyu ambaye hata upepo na mawimbi vinamtii?”

Matayo 16:13-16
13 Basi Yesu alipofika katika wilaya ya Kaisaria Filipi, aliwauliza wanafunzi wake, “Watu husema mimi Mwana wa Adamu kuwa ni nani?” 14 Wakamjibu, “Baadhi husema ni Yohana Mbatizaji, wengine husema ni Eliya; na wengine husema kwamba ni Yeremia au mmo jawapo wa manabii.” 15 Akawauliza, “Na ninyi je, mnasema mimi ni nani? 16 Simoni Petro akamjibu, “Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.”

Marko 6:14-16
14 Mfalme Herode akapata habari hizi, kwa maana jina la Yesu lilikuwa limefahamika kila mahali. Watu wengine walikuwa wakisema, “Yohana Mbatizaji amefufuka kutoka kwa wafu ndiyo maana uwezo wa kutenda miujiza unafanya kazi ndani yake!” 15 Wengine walisema, “Huyo ni Eliya!” Na wengine wakasema, “Ni nabii kama wale manabii wa zamani.” 16 Lakini Herode ali posikia habari hizi alisema, “Huyo ni Yohana Mbatizaji niliyem kata kichwa; amefufuka!”

2 Kings 2:11
11 As they were walking along and talking together, suddenly a chariot of fire and horses of fire appeared and separated the two of them, and Elijah went up to heaven in a whirlwind.

Exodus 3:14
14 God said to Moses, “I am who I am.[c] This is what you are to say to the Israelites: ‘I am has sent me to you.’”

Yohana 5:18
18 Maneno haya yaliwaudhi sana viongozi wa Wayahudi. Wakajaribu kila njia wapate kumwua, kwa sababu, zaidi ya kuvunja sheria za sabato, alikuwa akijifanya sawa na Mungu kwa kujiita Mwana wa Mungu.

1. Yohana 21:25
25 Jesus did many other things as well. If every one of them were written down, I suppose that even the whole world would not have room for the books that would be written.

2. a. Mathayo 1:21
21 Naye atamzaa mtoto wa kiume, nawe utamwita jina lake Yesu; kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka katika dhambi zao.”

b. Mathayo 1:23
23 “Tazama bikira atachukua mimba, naye atamzaa mtoto wa kiume nao watamwita Imanueli,” maana yake, “Mungu pamoja nasi”.

c. Mathayo 3:17
17 Na sauti kutoka mbinguni ikasema, “Huyu ndiye

d. Mathayo 12:8
8 kwa maana Mwana wa Adamu ni Bwana wa sabato.”

e. Mathayo 16:16
16 Simoni Petro akamjibu, “Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.”

f. Mathayo 19:16
16 Mtu mmoja alikuja kwa Yesu akamwuliza, “Mwalimu, nifanye jambo gani jema ili nipate uzima wa milele?”

3. a. Marko 5:6-7
6 Alipomwona Yesu kwa mbali, alimkimbilia akapiga magoti mbele yake,7 akapiga kelele kwa nguvu akasema, “Unataka nini kwangu, Yesu, Mwana wa Mungu Mkuu? Ninakusihi kwa jina la Mungu, usinitese!”

b. Luka 5:5
5 Simoni akamjibu, “Bwana, tumekesha usiku kucha tukivua na hatukuambulia kitu cho chote. Lakini, kwa kuwa wewe umesema, tutazishusha nyavu.”

c. Yohana 1: 35-36
35 Kesho yake, Yohana alikuwapo pale pamoja na wanafunzi wake wawili.36 Alipomwona Yesu akipita, alisema, “Tazameni! Mwana-Kondoo wa Mungu!”

d. Yohana 1:49
49 Nathanaeli akamwambia, “Mwalimu, wewe ni Mwana wa Mungu! Wewe ni Mfalme wa Israeli!”

e. 1 Korintho 1:6-7
6 kama ushuhuda wetu kumhusu Yesu ulivyothibitishwa ndani yenu. 7 Kwa hiyo hamjapungukiwa na karama yo yote ya kiroho wakati mnangoja kudhihirishwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

4. Mathayo 1:1-17
1 Kumbukumbu ya vizazi vya ukoo wa Yesu Kristo mwana wa Daudi na wa Abrahamu: 2 Abrahamu alikuwa baba yake Isaka; Isaka alikuwa baba yake Yakobo; na Yakobo alikuwa baba yake Yuda na ndugu zake. 3 Yuda alikuwa baba yake Peresi na Zera ambao mama yao alikuwa Tamari; Peresi alikuwa baba yake Esroni; Esroni alikuwa baba yake Aramu; 4 Aramu alikuwa baba yake Aminadabu; Aminadabu alikuwa baba yake Nashoni; Nashoni alikuwa baba yake Salmoni; 5 Salmoni alikuwa baba yake Boazi na mama yake Salmoni alikuwa Rahabu. Boazi alikuwa baba yake Obedi, ambaye mama yake alikuwa Ruti; Obedi alikuwa baba yake Yese; 6 Yese alikuwa baba yake Daudi ambaye alikuwa mfalme. Daudi alikuwa baba yake Solomoni ambaye mama yake ni yule aliyekuwa mke wa Uria; 7 Solomoni alikuwa baba yake Rehoboamu; Rehoboamu alikuwa baba yake Abiya; Abiya alikuwa baba yake Asa; 8 Asa alikuwa baba yake Yehoshafati; Yehoshafati alikuwa baba yake Yoramu; Yoramu alikuwa baba yake Uzia; 9 Uzia alikuwa baba yake Yothamu; Yothamu alikuwa baba yake Ahazi; Ahazi alikuwa baba yake Hezekia; 10 Hezekia alikuwa baba yake Manase; Manase alikuwa baba yake Amoni; Amoni alikuwa baba yake Yosia; 11 wakati wa uhamisho wa Babiloni, Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake; 12 na baada ya uhamisho wa Babiloni Yekonia alimzaa Shealtieli; Shealtieli alikuwa baba yake Zerubabeli; 13 Zeru babeli alikuwa baba yake Abihudi; Abihudi alikuwa baba yake Eliakimu ; Eliakimu alikuwa baba yake Azori; 14 Azori alikuwa baba yake Zadoki; Zadoki alikuwa baba yake Akimu; Akimu alikuwa baba yake Eliudi; 15 Eliudi alikuwa baba yake Elieza; Elieza alikuwa baba yake Matani; Matani alikuwa baba yake Yakobo; 16 Yakobo alikuwa baba yake Yosefu ambaye alikuwa mumewe Mar ia, aliyemzaa Yesu anayeitwa Kristo. 17 Basi, kulikuwepo vizazi kumi na vinne tangu Abrahamu mpaka wakati wa mfalme Daudi; na vizazi kumi na vinne tangu mfalme Daudi hadi wakati wa uhamisho wa Babiloni na vizazi kumi na vinne tangu wakati wa uhamisho hadi Kristo.

Yohana 2:1-11
1 Siku ya tatu kulikuwa na harusi katika mji wa Kana ulioko Galilaya. Mama yake Yesu alikuwapo 2 na Yesu pamoja na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa pia. 3 Divai ilipowaishia, mama yake Yesu alimwambia, “Hawana divai.” 4 Yesu akamjibu, “Mama, mbona unanihusisha kwenye jambo hili? Wakati wangu bado haujafika.” 5 Mama yake akawaambia watumishi, “Lo lote atakalowaambia, fanyeni. ” 6 Basi ilikuwapo hapo mitungi sita ya kuwekea maji ya kunawa, kufuatana na desturi ya Wayahudi ya kutawadha. Kila mtungi ungeweza kujazwa kwa madebe sita au saba ya maji. 7 Yesu akawaambia wale watumishi, “Ijazeni mitungi hiyo maji.” Wakaijaza mpaka juu.
8 Kisha akawaambia, “Sasa choteni maji kidogo mumpelekee mkuu wa sherehe.” Wakachota, wakampelekea. 9 Yule mkuu wa sherehe akayaonja yale maji ambayo yalikuwa yame geuka kuwa divai. Hakujua divai hiyo imetoka wapi ingawa wale watumishi waliochota yale maji walifahamu.
Basi akamwita bwana harusi kando 10 akamwambia, “Watu wote huwapa wageni divai nzuri kwanza kisha wakianza kutosheka huwaletea divai hafifu. 11 Hii ilikuwa ishara ya kwanza aliyofanya Yesu. Muujiza huu ulifanyika katika mji wa Kana huko Galilaya, ambako Yesu alidhi hirisha utukufu wake, na wanafunzi wake wakamwamini.

Marko 1:9-11
9 Baadaye Yesu akaja kutoka Nazareti katika sehemu ya Gali laya, akabatizwa na Yohana katika mto wa Yordani. 10 Yesu alipo toka kwenye maji aliona mbingu zikifunuka na Roho wa Mungu anam shukia kama njiwa.11 Na sauti kutoka mbinguni ikasema, “Wewe ni mwanangu mpendwa; nimependezwa nawe.”

Isaya 9:6
Maana kwa ajili yatu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume; na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; naye ataitwa jina lake, mshauri wa ajabu, mungu mwenye nguvu, baba wa milele, mfalme wa amani.

Wakolosai 1:15-20
15 Kristo anafanana kabisa na Mungu asiyeonekana. Yeye ali kuwepo kabla Mungu hajaumba kitu cho chote. 16 Yeye ndiye ali yeumba vitu vyote mbinguni na duniani; vitu vinavyoonekana na visivyoonekana; kama ni viti vya enzi au nguvu, au watawala au milki na mamlaka: vyote viliumbwa na yeye kwa ajili yake. 17 Yeye alikuwapo kabla ya vitu vingine vyote na kwa uwezo wake vitu vyote vinahusiana kwa mpango. 18 Yeye ni kichwa cha mwili, yaani kanisa lake; naye ni wa kwanza na mzaliwa wa kwanza wa wale wote wanaofufuka kutoka kwa wafu, ili yeye peke yake awe mkuu katika vitu vyote. 19 Kwa kuwa ilimpendeza Mungu kwamba ukamil ifu wake wote wa kimungu uwe ndani ya Mwanae; 20 na kwamba kwa njia ya mwanae vitu vyote vilivyoko duniani na vilivyoko mbinguni vipatanishwe na Mungu, kwa ajili ya damu yake iliyomwagwa msala bani kuleta amani.

15 Kristo anafanana kabisa na Mungu asiyeonekana.
Yeye ali kuwepo kabla Mungu hajaumba kitu cho chote.

Wakolosai 1:15-20

 
 

The Guide has her own Guidebook to help her lead and guide the lesson to be translated

Download Swahili Lesson #1 Guidebook Introduction

Swahili Lesson #1 Guidebook (to be translated)

Download Swahili Guidebook Bible Verses Swahili Lesson #1

Mistari ya Biblia

 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us