Project Hope     home >>stonecroft>> mwongozo >> yesu ni nani somo 6 >> mistari ya biblia
Mistari ya Biblia - Somo #6
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

SOMO LA SITA

JE NITAMWONA YESU TENA?

Kitabu mwongozo

Mistari ya Biblia

Kujisomea Biblia kwa Juma

Yohana 1:14-18
14 Neno akawa mwanadamu akaishi kati yetu akiwa amejaa utu kufu na kweli. Tuliona utukufu wake, utukufu wa Mwana pekee wa Baba. 15 Yohana alishuhudia habari zake, akatangaza: “Huyu ndiye yule niliyewaambia kuwa, ‘Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi kwa kuwa alikuwapo kabla sijazaliwa.”’ 16 Na kutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema tele. 17 Musa alitule tea sheria kutoka kwa Mungu, lakini Yesu Kristo ametuletea neema na kweli. 18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Lakini Mwanae pekee, ambaye ana uhusiano wa karibu sana na Baba yake, amemdhihirisha Mungu kwetu.

Yohana 14:1-11
Yesu akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia. 2 Katika nyumba ya baba yangu mna nafasi nyingi. Kama sivyo, nisingeliwaambia kwamba nakwenda kuwaandalia makao. 3 Na nikishawaandalia, nitarudi kuwachukua mkae pamoja nami; ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo. 4 Ninyi mnajua njia ya kufikia ninakokwenda.” 5 Tomaso akamwuliza, “Bwana, hatujui unakokwenda; tutaijuaje njia?”6 Yesu akawaam bia, “Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu. 7 Kama mngekuwa mnajua mimi ni nani, mngemfahamu na Baba yangu. Tangu sasa mnamfahamu Baba yangu na mmemwona.” 8 Filipo akamwambia Yesu, “Bwana, tuonyeshe Baba yako nasi tutaridhika.”9 Yesu akamjibu, “Filipo, imekuwaje hunifahamu baada ya mimi kuwa pamoja nanyi muda wote huu? Mtu ye yote ambaye ameniona mimi, amemwona Baba. Sasa inakuwaje unasema, ‘Tuonyeshe Baba’? 10 Je, huamini ya kuwa mimi niko ndani ya Baba yangu, na Baba yangu yuko ndani yangu? Mambo ninayowaambia siyasemi kwa mamlaka yangu mwenyewe, bali yanatoka kwa Baba yangu ambaye anaishi ndani yangu, na ndiye anayetenda haya yote. 11 Niaminini ninapowaambia ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu na Baba yangu yu ndani yangu. La sivyo, niaminini kwa sababu ya haya mambo ninayotenda.

1 Yohana 5:10-12
10 Kwa hiyo Wayahudi wakamwambia yule mtu aliyeponywa, “Leo ni sabato. Huruhusiwi kubeba mkeka wako.”

11 Yeye akawajibu, “Yule mtu aliyeniponya aliniambia, ‘Chu kua mkeka wako utembee.”’
12 Wakamwuliza, “Ni mtu gani huyo aliyekuambia uchukue mkeka wako utembee?”

Mathayo 16:24-27
24 Ndipo Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Mtu akitaka kuni fuata, ni lazima ajikane mwenyewe na achukue msalaba wake, anifu ate. 25 Kwa maana mtu akitaka kuokoa nafsi yake, ataipoteza; lakini mtu atakayeipoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataipata tena.
26 “Kwa maana mtu atapata faida gani akiupata ulimwengu wote lakini akaipoteza nafsi yake? Au mtu atabadilisha nini na nafsi yake? 27 Kwa maana mimi Mwana wa Adamu nitakuja katika utukufu wa Baba yangu pamoja na malaika wangu na nitamlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

Wafilipi 2:5-11
5 Muwe na nia kama ile aliyokuwa nayo Kristo Yesu; 6 yeye kwa asili alikuwa sawa na Mungu, lakini hakuona kwamba kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kush ikilia sana. 7 Bali alikubali kuacha vyote, akachukua hali ya mtumishi, akazaliwa na umbo la wanadamu. 8 Alipochukua umbo la mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii mpaka kufa, tena kifo cha msalaba. 9 Kwa sababu hiyo, Mungu alimwinua juu kabisa, akampa jina ambalo ni kuu kuliko majina yote; 10 ili kwa jina la Yesu, kila goti lipigwe, mbinguni na duniani na kuzimu; 11 na kila ulimi ukiri kwamba Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu.

1 Wathethalonike 4:15-18
15 Kama alivyosema Bwana mwenyewe, tunawaambieni kuwa sisi ambao tuko hai bado, tutakaokuwa hai mpaka Bwana arudi, kwa hakika hatutawatangulia wale waliokwisha kufa.
16 Kwa maana Bwana mwenyewe atashuka toka mbinguni, akitoa amri kwa sauti kuu pamoja na sauti ya malaika mkuu na sauti ya tarumbeta ya Mungu; na wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuka kwanza.17 Kisha sisi tulio hai bado, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu tukutane na Bwana angani. Na hivyo tutakuwa na Bwana milele.18 Kwa hiyo farijianeni kwa maneno haya.

Yohana 5:24-29
24 Ninawaambia hakika, ye yote anayesikiliza maneno yangu na kumwamini yule aliyenituma, anao uzima wa milele na hatahukumiwa. Amevuka kutoka kwenye mauti, na kuingia katika uzima.25 Nina waambia hakika, wakati utafika, tena umekwisha timia, ambapo wafu wataisikia sauti ya Mwana wa Mungu; na wote watakaoisikia wata kuwa hai.26 Kama vile Baba alivyo chanzo cha uzima, hali kad halika amemwezesha Mwanae kuwa chanzo cha uzima. 27 Na amempa Mwanae mamlaka ya kuhukumu kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu.

28 “Msishangae kusikia haya. Wakati unakuja ambapo wafu wataisikia sauti yake, 29 nao watatoka makaburini; wale waliot enda mema watafufuka na kuwa hai, na wale waliotenda maovu, wata fufuka na kuhukumiwa.

1. b.Mathayo 22:36-40
26 Ikatokea hivyo hivyo kwa yule ndugu wa pili hadi wote saba wakamwoa huyo mjane bila kupata watoto.27 Baadaye, yule mjane naye akafariki. 28 Sasa tuambie, siku ile ya ufufuo, ata hesabiwa kuwa ni mke wa nani? Maana aliolewa na wote saba!”

29 Yesu akawajibu, “Mnakosea kwa sababu hamjui Maandiko wala uwezo wa Mungu. 30 Wakati wa ufufuo, watu hawataoa wala kuolewa; kwa maana watakuwa kama malaika wa mbinguni. 31 Na kuhusu ufufuo wa wafu, hamjasoma Mungu alivyowaambia kwamba, 32 ‘Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo’? Yeye si Mungu wa wafu bali ni Mungu wa walio hai.”

33 Ule umati wa watu waliposikia hayo, walishangazwa sana na mafund isho yake.
34 Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazi sha Masadukayo, walikutana wakamjia pamoja. 35 Mmoja wao, mtaalamu wa sheria akajaribu kumtega kwa kumwuliza, 36 “Mwali mu, ni amri ipi iliyo kuu kuliko zote?”

37 Yesu akamjibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’ 38 Hii ndio amri kuu, tena ni ya kwanza. 39 Na ya pili inafanana nayo, nayo ni hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ 40 Amri hizi mbili ndio msingi wa sheria zote na Maandiko ya manabii.”

c. Marko 10:45
45 Kwa maana hata mimi Mwana wa Adamu sikuja ili nitumikiwe, bali nilikuja ili niwe mtumishi na kutoa maisha yangu yawe fidia kwa ajili ya watu wengi.”

3. Ufunuo 1:7
7 Tazama! Anakuja katika mawingu! Na kila jicho litamwona. Hata na wale waliomchoma mkuki na makabila yote ulimwenguni wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.

Yohana 19: 32-34
32 Kwa hiyo askari wakaenda wakavunja miguu ya mtu wa kwanza aliyesulubiwa na Yesu na wa pili pia. 34 Ila askari mmoja akamchoma mkuki ubavuni, na mara pakatoka damu na maji.

4. a. Mathayo 24:21-31
21 Kwa maana kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu mwanzo wa dunia mpaka sasa na ambayo haitatokea tena. 22 Kama siku hizo zisingepunguzwa, hakuna hata mtu mmoja ambaye angesalimika, lakini kwa ajili ya wale walioteu liwa na Mungu, siku hizo zitapunguzwa. 23 Wakati huo mtu aki waambia, ‘Tazama! Kristo yuko hapa!’ au ‘Kristo yule pale!’ msi sadiki. 24 Kwa maana watatokea makristo na manabii wa uongo na watafanya ishara za ajabu na miujiza mingi ili kuwadanganya, hata ikiwezekana, wateule wa Mungu. 25 Angalieni, nawatahadharisha mapema.

26 “Kwa hiyo wakiwaambia, ‘Yule kule nyikani,’ msitoke. Au wakisema, ‘Yuko chumbani 27 Kwa maana kama vile umeme unavyotokea mashariki na kuangaza mpaka magharibi, ndivyo itakavyokuwa kuja kwangu mimi Mwana wa Adamu. 28 Kwa maana po pote ulipo mzoga, ndipo wakusanyikapo tai.

29 “Mara baada ya dhiki ya wakati huo, jua litatiwa giza, mwezi hautatoa mwanga wake tena, na nyota zitaanguka kutoka mbin guni; nguvu za anga zitatikisika. 30 Ndipo itaonekana ishara ya Mwana wa Adamu angani na watu wote ulimwenguni wataomboleza. Nao wataniona mimi Mwana wa Adamu nikija juu ya mawingu ya angani, katika uwezo na utukufu mkuu. 31 Na nitawatuma malaika zangu kwa sauti kuu ya tarumbeta na watawakusanya wateule wangu kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho mmoja wa mbingu hadi mwisho mwingine.

b. Marko 13:32-37
32 “Hakuna ajuaye siku hiyo itakuwa lini au saa ngapi; hata malaika mbinguni hawajui wala mimi Mwana sijui, isipokuwa Mungu Baba peke yake.33 “Jiandaeni, muwe macho. Kwa maana hamjui wakati mambo haya yatakapotokea. 34 Ni kama mtu anayesafiri na kuwaachia wat umishi wake madaraka, kila mtu na wajibu wake; kisha akamwambia mlinzi wa mlango awe macho. 35 Kesheni basi, kwa sababu hamjui ni lini bwana mwenye nyumba atarudi.

Anaweza akaja jioni, au usiku wa manane au alfajiri au mapambazuko. 36 Kama akija gha fla, pasipo ninyi kumtazamia, asije awakute mmelala. 37 Na haya ninayowaambia ninyi nawaambia watu wote: Kesheni!”

c. Luka 21:25-28, 34-36
25 “Kutakuwa na matukio ya ajabu kwenye jua, mwezi na nyota. Hapa ulimwenguni, mataifa yatakuwa katika dhiki na wasi wasi kutokana na ngurumo na dhoruba za kutisha zitakazotokea baharini. 26 Watu watakufa moyo kwa hofu na wasiwasi kuhusu yale wanayoogopa kuwa yataukumba ulimwengu; kwani nguvu za anga zita tikisika. 27 Ndipo wataniona mimi Mwana wa Adamu nikija katika wingu kwa uwezo na utukufu mkuu.28 Mambo haya yakianza kutokea, simameni imara, mjipe moyo, kwa kuwa ukombozi wenu unakaribia.”

34 Jihadharini msije mkatawaliwa na ulafi, ulevi na wasiwasi wa maisha haya. Kisha siku ikafika pasipo ninyi kutazamia mka naswa! 35 Kwa maana siku hiyo itawakumba watu wote waishio duniani. 36 Kaeni macho na ombeni ili Mungu awawezeshe kuepuka yale yote yatakayotokea na mweze kusimama mbele yangu mimi Mwana wa Adamu.”

5. Ebrania 9:27
27 Na kama ambavyo mwanadamu ameandikiwa kufa mara moja tu, na baada ya hapo kukabili hukumu;

6. a. 2 Korintho 5:10
10 Kwa kuwa sisi sote inatubidi kusimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo. Na kila mmoja atapokea mema au mabaya, kulingana na matendo yake alipokuwa katika mwili.

b. Matendo 17:30-31
30 Mungu alisamehe ujinga huo wa zamani, lakini sasa anaamuru watu wote watubu, waachane na miungu ya sanamu.31 Kwa kuwa amepanga siku ambayo atahukumu ulimwengu kwa haki akimtumia mtu aliyemchagua, ambaye amemhakikisha kwa watu wote kwa kumfufua kutoka kwa wafu.”

c. Ufunuo 20:11-15
11 Kisha nikaona kiti kikubwa cha enzi cheupe, pamoja na huyo aliyeketi juu yake. Dunia na anga zilikimbia kutoka machoni pake zikatoweka wala hazikuonekana tena. 12 Nikaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya kiti cha enzi, na vitabu vikafunguliwa. Pia kitabu kingine ambacho ni kitabu cha uzima kikafunguliwa. Na hao wafu wakahukumiwa kutokana na yale yaliy oandikwa ndani ya vitabu hivyo, kuhusu matendo yao.

13 Bahari zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake, na kifo na kuzimu nazo zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake, na wote wakahukumiwa kwa matendo yao.14 Kisha mauti na kuzimu zikatupwa katika ziwa la moto. Hiki ndicho kifo cha pili, yaani ziwa la moto. 15 Na kama jina la mtu halikukutwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.

1 Timotheo 2:3-4
3 Jambo hili ni jema na linampendeza Mungu Mwokozi wetu 4 ambaye anapenda watu wote waokolewe na wapate kuijua kweli.

Matayo 25: 41
41 “Kisha atawaambia wale walio kushoto kwake, ‘Ondokeni kwangu ninyi mliolaaniwa, nendeni katika moto wa milele alioan daliwa shetani na malaika zake.

Wafilipi 2: 10-11
10 ili kwa jina la Yesu, kila goti lipigwe, mbinguni na duniani na kuzimu; 11 na kila ulimi ukiri kwamba Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu

1 Yohana 2: 15-17
15 Msiipende dunia wala mambo yaliyomo duniani. Kama mtu akiipenda dunia, hawezi kumpenda Baba. 16 Maana vitu vyote vil ivyomo duniani, yaani, tamaa za mwili, tamaa ya vitu vinavyoone kana kwa macho, na kiburi kiletwacho na mali, vyote hivi havitoki kwa Baba bali hutoka ulimwenguni.17 Nayo dunia inapita na tamaa zake zote zinapita, lakini mtu anayetimiza mapenzi ya Mungu huishi milele.

2 Wakorintho 5: 17
17 Kwa hiyo mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama, mapya yamekuja.

1 Yohana 1: 8-10
8 Tukisema kwamba hatuna dhambi tunajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani yetu. 9 Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwa minifu na wa haki na atatusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote.10 Tukisema hatujatenda dhambi tunamfanya yeye kuwa mwongo, na neno lake halimo ndani yetu.

1 Yohana 4: 7-11
7 Wapendwa, tupendane, kwa sababu upendo hutoka kwa Mungu. Mtu mwenye upendo amezaliwa na Mungu na anamjua Mungu. 8 Mtu asiye na upendo hamjui Mungu; kwa maana Mungu ni upendo. 9 Na hivi ndivyo Mungu alivyoonyesha upendo wake kwetu: alimtuma Mwana wake wa pekee ulimwenguni ili kwa ajili yake sisi tupate kwa kupitia kwake. 10 Na huu ndio upendo: si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi hata akamtuma Mwanae awe sadaka ya kulipia dhambi zetu.11 Wapendwa, kwa kuwa Mungu ali tupenda kiasi hicho, sisi pia tunapaswa kupendana. 12 Hakuna mtu aliyepata kumwona Mungu; lakini tukipendana, Mungu anaishi ndani yetu, na upendo wake unakamilika ndani yetu.

7. a. 2 Wakorintho 7:1
Kwa kuwa tumepewa ahadi hizi wapendwa, basi tujitakase kutokana na kila aina ya uchafu wa mwili na roho, na tufanye bidii kufikia ukamilifu kwa kuwa tunamcha Mungu.

b. Matayo 6:19-21
19 “Msijiwekee mali nyingi duniani ambapo wadudu na kutu huharibu na wezi huvunja na kuiba. 20 Lakini jiwekeeni mali mbinguni ambapo wadudu na kutu hawaharibu na wezi hawavunji na kuiba.21 Kwa sababu pale akiba yako ilipo ndipo moyo wako uta kapokuwa.”

c. Yakobo 1: 2-4
2 Ndugu wapendwa, mnapopatwa na majaribu mbalimbali, yahesab uni kuwa ni furaha tupu. 3 Kwa maana mnafahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu hujenga ustahimilivu. 4 Na ustahimilivu ukimaliza kazi yake mtakuwa wakamilifu pasipo kupungukiwa na cho chote.

d. 2 Timotheo 4:1-5
Ninakuamuru mbele za Mungu na mbele za Kristo Yesu ambaye atawahukumu walio hai na wafu; na kwa kuja kwake na ufalme wake:2 hubiri Neno; lisisitize wakati ufaao na wakati usiofaa; sadik isha, kemea, na kuonya kwa uvumilivu mkuu na mafundisho thabiti.

3 Maana wakati unakuja ambapo watu hawatavumilia kusikia mafund isho yenye uzima; bali kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajilundi kia walimu tele watakaowaambia yale ambayo masikio yao yanatamani sana kuyasikia. 4 Watakataa kabisa kusikia kweli na watageukia hadithi za uongo. 5 Bali wewe uwe imara, katika mambo yote, vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiza wajibu wote wa huduma yako.

e. 1 Korintho 15:58
58 Kwa hiyo ndugu zangu, simameni imara. Msitikisike. Mzidi sana kujitoa kwa ajili ya kazi ya Bwana, kwa maana mnajua ya kuwa, juhudi yenu si bure katika Bwana.

Psalm 16:11
11 You make known to me the path of life; you will fill me with joy in your presence, with eternal pleasures at your right hand.

 
 

The Guide has her own Guidebook to help her lead and guide the lesson.

Swahili Lesson #6 Guidebook (to be translated)

Download Swahili Guidebook Bible Verses Swahili Lesson #6

Mistari ya Biblia

 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us