Project Hope     home >>stonecroft>> mwongozo >> yesu ni nani somo 3 >> mistari ya biblia
Mistari ya Biblia - Somo #3
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

SOMO LA TATU

YESU ALIFANYA NINI?

Kitabu mwongozo

Mistari ya Biblia

Kujisomea Biblia kwa Juma

Marko 1:16-28
6 Yesu alipokuwa akitembea kando kando ya Ziwa la Galilaya alimwona Simoni na Andrea ndugu yake wakivua samaki kwa kutumia nyavu; ndugu hawa wawili walikuwa wavuvi. 17 Yesu akawaambia, “Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.” 18 Wakaacha nyavu zao mara moja wakamfuata Yesu. 19 Alipokwenda mbele kidogo, akawaona Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo. Wao walikuwa katika mashua wakitengeneza nyavu zao. 20 Mara tu alipowaona akawaita, nao wakamwacha baba yao na wavuvi wa kuajiriwa, wakamfuata Yesu.
21 Wakaenda mpaka Kapernaumu. Ilipofika siku ya sabato, Yesu akaenda katika sinagogi akaanza kufundisha. 22 Watu waliom sikiliza, walishangazwa sana na mafundisho yake. Yeye hakufund isha kama walimu wao wa sheria. Alifundisha kama mtu mwenye mam laka.
23 Wakati huo huo, mtu mmoja aliyekuwa na pepo 24 akapiga kelele humo katika sinagogi akasema, “Mbona unatuingilia, Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Ninafahamu wewe ni nani! Wewe ni Mtakatifu wa Mungu.”25 Lakini Yesu akamkemea akamwambia, “Kaa kimya! Mtoke!” 26 Yule pepo mchafu akamtikisa yule mtu kwa nguvu kisha akamtoka akipiga kelele.
27 Watu wakashangaa, wakaanza kuulizana, “Haya ni mambo gani? Ni mafundisho mapya? Huyu mtu anatoa amri kwa mamlaka na hata pepo wanamtii!” 28 Sifa zake zikaenea upesi kila mahali katika mkoa wote wa

Marko 1:29-39
29 Yesu na wanafunzi wake walipoondoka katika sinagogi, walikwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Simoni na Andrea. Wanafunzi wengine waliokuwepo ni Yakobo na Yohana. 30 Mama mkwe wake Simoni alikuwa kitandani, ana homa. Na mara Yesu alipofika wakamweleza. 31 Yesu akaenda karibu na kitanda, akamshika yule mama mkono, akamwinua; homa ikamtoka, akawahudumia.
32 Jioni ile, baada ya jua kutua, watu wakawaleta wagonjwa wote na wengine waliopagawa na pepo kwa Yesu. 33 Watu wote wa mji huo wakakusanyika mbele ya nyumba hiyo. 34 Yesu akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa ya kila aina. Akawatoa pepo wengi; lakini hakuwaruhusu pepo hao wazungumze, kwa sababu wal ifahamu yeye ni nani. 35 Kesho yake alfajiri, kabla hapajapambazuka, Yesu akaamka akaenda mahali pa faragha, akaomba. 36 Simoni na wenzake wakaenda kumtafuta.37 Walipomwona wakamwambia, “Kila mtu ana kutafuta!”
38 Yesu akawajibu, “Twendeni kwenye vijiji vingine vya jirani nikahubiri huko pia; kwa sababu hicho ndicho kilicho nileta.” 39 Kwa hiyo akazunguka Galilaya nzima akihubiri katika masinagogi na kuponya watu waliopagawa na pepo.

Marko 3:13-19
13 Yesu alipanda mlimani akawaita wale aliowataka, nao wakaja.14 Akawachagua kumi na wawili wafuatane naye na awatume kuhubiri na15 wawe na mamlaka ya kufukuza pepo. 16 Hawa ndio aliowachagua: Simoni, ambaye alimwita Petro, 17 Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo ambao aliwaita Boanerge, yaani wana wa ngurumo; 18 Andrea; Filipo; Bartholomayo; Mathayo; Tomaso; Yakobo, mwana wa Alfayo; Thadayo; Simoni, Mkanaani; na 19 Yuda

Marko 4:35-41
35 Siku hiyo, ilipokaribia jioni, aliwaambia wanafunzi wake, “Tuvuke, twende ng’ambo ya pili.” 36 Wakawaacha wale watu wakaingia katika ile mashua ambamo Yesu alikuwa amekaa. Pia palikuwa na mashua nyingine.
37 Pakatokea dhoruba kali, mawimbi yakaipiga ile mashua waliyokuwa wakivukia, ikaanza kujaa maji. Yesu alikuwa amelala akiegemea mto sehemu ya nyuma kwenye ile mashua.
38 Wanafunzi wake wakamwamsha, wakamwambia, “Mwalimu, hujali kwamba tuna zama?’ 39 Akaamka, akaukemea ule upepo, akaiambia ile bahari, “Kaa kimya! Tulia!” Ule upepo ukatulia, kukawa shwari. 40 Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kwa nini mnaogopa? Je, bado hamna imani?” 41 Lakini wao walikuwa wamejawa na hofu wakaulizana, “Ni nani huyu ambaye hata upepo na mawimbi vinamtii?”

Marko 6:30-44
30 Wale wanafunzi kumi na wawili waliporudi, walimweleza Yesu mambo yote waliyofanya na kufundisha. 31 Kwa kuwa watu wengi mno walikuwa wakija na kutoka, hata wakakosa nafasi ya kula, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Twendeni peke yetu mahali pa faragha, mpate kupumzika.” 32 Basi wakaondoka kwa mashua peke yao wakaenda mahali pasipo na watu.
33 Lakini watu waliowaona wakiondoka, wakawatambua. Wakawa tangulia mbio kwa miguu kutoka miji yote wakielekea kule waliko kuwa wakienda. Wakawahi kufika.
34 Yesu alipofika nchi kavu na kuuona huo umati wa watu, aliwaonea huruma kwa maana walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Kwa hiyo akaanza kuwafundisha mambo mengi.
35 Hata saa za mchana zilipoanza kupita, wanafunzi wake wakamwendea wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na saa zimek wenda. 36 Waruhusu watu waondoke wakajinunulie chakula kwenye mashamba na vijiji vya jirani.”
37 Lakini Yesu akawajibu, “Wapeni ninyi chakula.” Wakam wambia, “Tunahitaji fedha nyingi sana, kununulia mikate ya kutosha kulisha watu wote hawa.”
38 Akawauliza, “Mna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie.” Waliporudi wakamwambia, “Ipo mikate mitano na samaki wawili.”
39 Kisha Yesu akawaamuru wawaketishe watu makundi makundi kwenye nyasi, 40 nao wakaketi kwenye makundi ya watu mia mia na hamsini hamsini. 41 Yesu akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili akatazama mbinguni, akashukuru, kisha akaimega ile mikate akawapa wanafunzi wake wawagawie wale watu. Pia akawagawia wote wale samaki wawili. 42 Watu wote wakala, wakashiba. 43 Wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia wakajaza vikapu kumi na viwili. 44 Idadi ya wanaume waliokula walikuwa elfu tano.

Marko 10:2-16
2 Baadhi ya Mafarisayo wakamjia wakitaka kumtega, wakamwul iza, “Ni halali mtu kumwacha mke wake?”
3 Yesu akawajibu, “Musa aliwaamuruje?” 4 Wakamjibu, “Musa aliruhusu kwamba mume anaweza kumwandikia mkewe hati ya talaka na kumwacha.”
5 Yesu akawaambia, “Musa aliwaandikia sheria hiyo kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. 6 Lakini tangu mwanzo wa uumbaji, ‘Mungu aliwaumba mume na mke. 7 Na kwa sababu hii mume atamwacha baba yake na mama yake na hao wawili, watakuwa mwili mmoja.’ 8 Kwa hiyo hawatakuwa wawili tena bali mwili mmoja. 9 Basi, alichokiun ganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.”
10 Baadaye waliporudi nyumbani , wanafunzi wa Yesu walimwul iza kuhusu jambo hili.
11 Akawajibu, “Mtu ye yote anayempa mkewe talaka na kuoa mke mwingine, anazini kwa yule mke aliyempa talaka. 12 Na mwa namke anayempa mumewe talaka na kuolewa na mume mwingine, anazini pia.”
13 Watu walikuwa wakimletea Yesu watoto wadogo ili awaguse lakini wanafunzi wake wakawakemea. 14 Yesu alipoona yaliyokuwa yakitokea alichukizwa, akawaambia wanafunzi wake, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni wa watu kama hawa! 15 Ninawahakikishieni kwamba, mtu ye yote ambaye hataukubali Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kamwe.”16 Akawakumbatia wale watoto wadogo, akaweka mikono yake juu yao, akawabariki.

Yohana 2:13-22
13 Ilipokaribia sikukuu ya Wayahudi iitwayo Pasaka, Yesu alikwenda Yerusalemu. 14 Alipoingia Hekaluni aliwakuta watu wakiuza ng’ombe, kondoo na njiwa, na wengine wamekaa kwenye meza zao wakifanya biashara ya kubadilishana fedha. 15 Akatengeneza mjeledi wa kamba akawafukuza wote kutoka Hekaluni pamoja na kon doo na ng’ombe; akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilish ana fedha na kuzimwaga fedha zao.
16 Akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, “Watoeni hapa! Mnathubutuje kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa soko?” 17 Wanafunzi wake wakakumbuka kuwa Maan diko yalisema: “Upendo wangu kwa nyumba yako utaniangamiza.”
18 Viongozi wa Wayahudi wakamwuliza, “Unaweza kutuonyesha ishara gani kuthibitisha una mamlaka ya kufanya mambo haya?”
19 Yesu akawajibu, “Livunjeni hili Hekalu, nami nitalijenga tena kwa siku tatu!”
20 Wale Wayahudi wakamjibu, “Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arobaini na sita. Wewe unasema unaweza kulijenga kwa siku tatu?”
21 Lakini yeye aliposema ‘Hekalu’ alikuwa anazungumzia mwili wake. 22 Kwa hiyo alipofufuliwa kutoka kwa wafu, wanafunzi wake walikumbuka maneno haya; wakayaamini Maandiko na yale maneno ali yosema Yesu.

Marko 11: 15-17
15 Walipofika Yerusalemu, Yesu aliingia Hekaluni akaanza kuwafukuza watu waliokuwa wakifanya biashara humo. Akapindua meza za waliokuwa wakibadilisha fedha na viti vya watu waliokuwa wakiuza njiwa.16 Hakuruhusu mtu ye yote kuchukua bidhaa kupi tia ukumbi wa Hekalu.17 Akawafundisha akisema, “Je, haikuan dikwa katika Maandiko kuwa: ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa watu wote’? Mbona ninyi mmeigeuza kuwa pango la wany ang’anyi?”

Luka 1: 29,34
29 Mariamu alifadhaishwa sana na maneno haya, akajiuliza moyoni, maana ya salamu hizi ni nini.
34 Mariamu akamwuliza malaika, “Lakini, nitapataje mimba, na mimi ni bikira?”

Luka 2: 19, 51
19 Lakini Mariamu akayaweka mambo haya yote moyoni mwake, akayafikiria mara kwa mara.
51 Akarudi pamoja na wazazi wake hadi Nazareti. Akawa aki watii, na mama yake akayaweka moyoni mambo haya yote.

Yohana 1: 1-3, 14
Hapo mwanzo, kabla ya kuwapo kitu kingine cho chote, aliku wapo Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye alikuwa Mungu. 2 Tangu mwanzo Neno amekuwa na Mungu. 3 Vitu vyote viliumbwa na yeye, wala hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho hakukiumba.
14 Neno akawa mwanadamu akaishi kati yetu akiwa amejaa utu kufu na kweli. Tuliona utukufu wake, utukufu wa Mwana pekee wa Baba.

1. a. Luke 3:23
23 Yesu alikuwa na umri wa miaka kama thelathini hivi ali poanza kazi ya kuhubiri. Yesu alijulikana kama mtoto wa Yusufu. Yusufu alikuwa mwana wa Eli,

b. 1 Yohana 4:9
9 Na hivi ndivyo Mungu alivyoonyesha upendo wake kwetu: alimtuma Mwana wake wa pekee ulimwenguni ili kwa ajili yake sisi tupate kwa kupitia kwake.

2. a Yohana 5:17
17 Yesu akawaambia, “Baba yangu anafanya mema siku zote. Mimi pia sina budi kufanya mema.”

3. a. Marko 1:21
21 Wakaenda mpaka Kapernaumu. Ilipofika siku ya sabato, Yesu akaenda katika sinagogi akaanza kufundisha.

b. Marko 1:32-34
32 Jioni ile, baada ya jua kutua, watu wakawaleta wagonjwa wote na wengine waliopagawa na pepo kwa Yesu. 33 Watu wote wa mji huo wakakusanyika mbele ya nyumba hiyo. 34 Yesu akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa ya kila aina. Akawatoa pepo wengi; lakini hakuwaruhusu pepo hao wazungumze, kwa sababu wal ifahamu yeye ni nani.

c. Marko 1:35
35 Kesho yake alfajiri, kabla hapajapambazuka, Yesu akaamka akaenda mahali pa faragha, akaomba.

d. Marko 1:38
38 Yesu akawajibu, “Twendeni kwenye vijiji vingine vya jirani nikahubiri huko pia; kwa sababu hicho ndicho kilicho nileta.”

e. Marko 6:7-12
7 Akawaita wale wanafunzi kumi na wawili akaanza kuwatuma wawili wawili na akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu.
8 Akawaagiza wasichukue cho chote safarini isipokuwa fimbo tu. Wasichukue mkate, wala mfuko, wala fedha. 9 Ila wavae viatu lakini wasichukue nguo ya kubadili. 10 Pia akawaambia, “Mkiin gia nyumba yo yote, kaeni hapo hapo hadi mtakapoondoka katika mji huo. 11 Na mahali po pote ambapo hamtakaribishwa wala kusikili zwa, mtakapoondoka hapo, kung’uteni mavumbi yaliyoko miguuni mwenu, kama onyo lenu kwao.”
12 Kwa hiyo wakatoka, wakaenda wakihubiri kwamba watu wat ubu, waache dhambi.

Yohana 21: 25
25 Jesus did many other things as well. If every one of them were written down, I suppose that even the whole world would not have room for the books that would be written.

4. a. Luka 4:33-36
33 Alikuwepo mtu mmoja katika sinagogi aliyekuwa ame pagawa na pepo mchafu, naye alianza kupiga kelele kwa nguvu akisema, 34 “Unataka kutufanya nini, Wewe Yesu wa Nazareti? Ume kuja kutuangamiza? Nakufahamu wewe ni nani. Wewe ni Mtakatifu wa Mungu.” 35 Yesu akamwamuru yule pepo: “Nyamaza! Mtoke!” Yule pepo akamwangusha chini yule mtu mbele yao, akamtoka pasipo kumd huru. 36 Watu wote wakashangaa wakaambiana, “Mafundisho ya mtu huyu ni ya ajabu. Anawaamuru pepo wachafu kwa mamlaka na nguvu, nao wanatoka!

b. Luka 5:4-10
4 Alipokwisha zungumza na watu akamwambia Simoni, “Sasa ipe leke mashua hadi mahali penye kina kirefu, kisha mshushe nyavu zenu nanyi mtapata samaki.”
5 Simoni akamjibu, “Bwana, tumekesha usiku kucha tukivua na hatukuambulia kitu cho chote. Lakini, kwa kuwa wewe umesema, tutazishusha nyavu.” 6 Nao walipofanya kama Yesu alivyowaagiza, nyavu zao zikajaa samaki, zikaanza kuchanika! 7 Wakawaashiria wavuvi wa ile mashua nyingine waje kuwasaidia. Mashua zote mbili zikajaa samaki hata karibu kuzama.
8 Simoni Petro alipoona yaliyotokea alipiga magoti mbele ya Yesu akamwambia, “Bwana,tafadhali uniache kwa maana mimi ni mwe nye dhambi.” 9 Kwa kuwa yeye na wavuvi wenzake walikuwa wamesh angazwa sana na wingi wa samaki waliopata. 10 Hali kadhalika wavuvi wa ile mashua nyingine, Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo walishangazwa pia. Ndipo Yesu akamwambia Simoni, “Usiogope; tangu sasa utakuwa mvuvi wa watu.”

c. Marko 1:40-42
40 Akaja mtu mwenye ukoma, akapiga magoti mbele ya Yesu akamsihi, “Ukitaka, unaweza kunitakasa.” 41 Yesu akamwonea huruma, akanyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Nataka upone, takasika.” 42 Mara ukoma wote ukaisha akapona kabisa.

d. Mathayo 15:1-9
Baadhi ya walimu wa sheria na Mafarisayo kutoka Yerusalemu walikuja kwa Yesu wakamwuliza, 2 “Mbona wanafunzi wako hawafu ati mafundisho ya wazee wetu? Kwa maana wao hawanawi mikono ka bla ya kula!” 3 Yesu akawajibu, “Mbona ninyi mnazivunja amri za Mungu kwa ajili ya mafundisho yenu? 4 Kwa maana Mungu alisema: ‘Waheshimu baba yako na mama yako’ na ‘Ye yote amtukanaye baba yake au mama yake, na auawe.’ 5 Lakini ninyi mnasema kwamba mtu akimwambia baba yake au mama yake, ‘Kile ambacho ningeweza kuku saidia nacho nimekitoa kwa Mungu,’ basi hana wajibu tena wa kum saidia baba yake. 6 Basi kwa ajili ya mafundisho yenu mnavunja amri ya Mungu. 7 Ninyi wanafiki! Isaya alisema sawa juu yenu alipotabiri kwamba: 8 ‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami. 9 Kuniabudu kwao ni bure, na mafundisho yao ni maagizo ya wanadamu.’

e. Luka 7:11-17
11 Baada ya siku hiyo, Yesu alikwenda mji mmoja uitwao Naini. Wanafunzi wake na umati wa watu waliongozana naye. 12 Alipokaribia njia ya kuingia mjini alikutana na watu wal iobeba maiti wakitoka nje ya mji. Marehemu alikuwa mtoto wa kiume wa pekee wa mama mmoja mjane na umati wa watu wa mji ule ulikuwa pamoja na huyo mama. 13 Bwana Yesu alipomwona yule mjane moyo wake ulijaa huruma, akamwambia, “Usilie.” 14 Kisha akalisoge lea lile jeneza akaligusa na wale waliolibeba wakasimama. Ndipo akasema: “Kijana nakuambia, amka!” 15 Yule aliyekuwa marehemu akaamka, akakaa na akaanza kusema! Yesu akamkabidhi kwa mama yake.
16 Watu wote wakajawa na hofu. Wakamtukuza Mungu wakisema, “Nabii mkuu ametokea kati yetu. Mungu amekuja kutuokoa sisi watu wake.”17 Habari hizi za mambo aliyofanya Yesu zikaenea Uyahudi nzima na sehemu za jirani.

Luka 3:21-22
21 Baada ya watu wote kubatizwa, Yesu naye alibatizwa. Na alipokuwa akiomba, mbingu zilifunguka. 22 Roho Mtakatifu akash uka juu yake kama hua; na sauti ikasikika kutoka mbinguni ikisema: “Wewe ni Mwanangu mpendwa, ninapendezwa nawe.”

5. a. Yohana 6:38
38 Kwa maana sikushuka kutoka mbinguni nije kutimiza mapenzi yangu, bali nitimize mapenzi yake yeye aliyenituma.

b. Yohana 7:16-17
16 Yesu akawajibu , “Mafundisho yangu hayatoki kwangu. Yanatoka kwake yeye aliyenituma. 17 Mtu ye yote akipenda kufanya mapenzi ya Mungu, atajua kama mafundisho yangu yanatoka kwa Mungu au ninasema kwa mamlaka yangu mwenyewe.

c. Wafilipi 2:13
13 Kwa maana ni Mungu ambaye anatenda kazi ndani yenu, akiwapa nia ya kutimiza mapenzi yake na kuwawezesha kutenda yale yanayompendeza 1

6. Warumi 12:2
2 Msiige tabia na mien endo ya dunia hii bali mbadilishwe, nia zenu zikifanywa kuwa mpya, ili mpate kuwa na hakika ni nini mapenzi ya Mungu: yaliyo mema, yanayopendeza machoni pake na makamilifu.

Mwanzo 1:27-28
Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimuumba mwanamume na mwanamke alimuumba. Mungu akawabarikia, mungu akawaambia, zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

Mwanzo 2:15
Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya edeni, ailime na kuitunza.

Mwanzo 3:17
Akamwambia adamu, kwa kuwa umesikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti aambao nalikuagiza, nikasema, usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako.

7. a. 2 Wathethalonike 3:10
10 Maana tulipokuwa pamoja nanyi tuliwapa amri hii: “Ikiwa mtu hatafanya kazi, basi asile.”

b. Warumi 12:11
11 Juhudi yenu isipungue, moto wenu wa kiroho uendelee kuwaka mkimtumikia Mungu.

8. Waefeso 6:5-8
5 Watumwa, watiini hao walio mabwana zenu hapa duniani, kwa heshima na kwa kutetemeka na kwa moyo mmoja, kama vile mnamtii Kristo. 6 Watiini, sio tu wakati wakiwaona ili mpate sifa, bali mtumike kama watumishi wa Kristo, mkifanya mapenzi ya Mungu kwa moyo.
7 Toeni huduma yenu kwa moyo wote, kama vile mnamtumikia Bwana na sio watu. 8 Mkumbuke kuwa Bwana atampa kila mmoja tuzo kutegemeana na wema aliotenda, kama yeye ni mtumwa au ni mtu huru.

9. a. 1 Wakorintho 10:31
31 Basi, lo lote mfanyalo, kama ni kula au ni kunywa, fanyeni mambo yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu.

b. 1 Wakorintho 16:14
14 Fanyeni kila kitu katika upendo.

c. Wakolosai 3:23
23 Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo kama watu wanaomtumikia Bwana na siyo wanadamu.

Yohana 13: 34-35
34 Nina waachia amri mpya: pendaneni ninyi kwa ninyi. Kama mimi nilivy owapenda, na ninyi mpendane vivyo hivyo. 35 Kama mkipendana hivyo, watu wote watafahamu ya kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.”

Exodus 31:15
15 For six days work is to be done, but the seventh day is a day of sabbath rest, holy to the Lord. Whoever does any work on the Sabbath day is to be put to death.

Matayo 5: 17
17 “Msidhani kwamba nimekuja kufuta sheria ya Musa na mafundisho ya manabii. kwamba mpaka mbingu na dunia zitaka potoweka, hakuna hata herufi moja ya sheria itakayopotea mpaka shabaha yake ikamilike.

Marko 6: 31
31 Kwa kuwa watu wengi mno walikuwa wakija na kutoka, hata wakakosa nafasi ya kula, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Twendeni peke yetu mahali pa faragha, mpate kupumzika.”

Matayo 11: 28-30
28 “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jifungeni nira yangu; jifunzeni kutoka kwangu; kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu. 30 Kwa maana nira yangu ni rahisi, na mzigo wangu ni mwepesi.”

10. a.Yohana 6:29
29 Yesu akawajibu, “Kazi anayotaka Mungu muifanye ni hii: mumwamini yeye aliyenituma.”

b. Yohana 3:16
16 “Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu kiasi cha kumtoa Mwanae pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele

1 Corinthians 3: 13-15
13 kazi yake itaonekana; kwa kuwa ile siku itaidhihirisha kazi yake. Itadhihirishwa kwa moto, na moto utapima ubora wa kazi ya kila mtu. 14 Kama alichojenga hakitaharibiwa kwa moto, atapokea tuzo. 15 Kama kazi ya mtu itateketea, atapata hasara, ila yeye mwenyewe ataokolewa, lakini kama mtu aliyenusurika kwenye moto.

 

 
 

The Guide has her own Guidebook to help her lead and guide the lesson.

Swahili Lesson #3 Guidebook (to be translated)

Download Swahili Guidebook Bible Verses Swahili Lesson #3

Mistari ya Biblia

 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us