Project Hope     home >>stonecroft>> mwongozo >> yesu ni nani somo 5 >> mistari ya biblia
Mistari ya Biblia - Somo #5
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

SOMO LA TANO

YESU YUKO WAPI KWA SASA

Kitabu mwongozo

Mistari ya Biblia


Kujisomea Biblia kwa Juma

Matendo 1:6-11
Mpendwa Teofilo, Katika Kitabu changu cha kwanza nilikuan dikia kuhusu mambo yote aliyotenda Yesu, 2 hadi wakati alipopaa mbinguni. Kabla hajachukuliwa juu, aliwapa mitume wake maagizo kwa njia ya Roho Mtakatifu. 3 Alijionyesha kwao akiwa hai muda wa siku arobaini baada ya kufufuka kwake. Akawahakikishia kwa njia nyingi ya kuwa ni yeye na akaongea nao kuhusu Ufalme wa Mungu.
4 Wakati mmoja alipokuwa nao, aliwapa amri hii, “Msiondoke Yerusalemu, mpaka mtakapopokea ahadi aliyotoa Baba, ambayo mmeni sikia nikiizungumzia. 5 Kwa maana Yohana aliwabatiza kwa maji lakini baada ya siku chache mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”
6 Mitume walipokutana na Yesu walimwuliza, “Bwana, wakati huu ndipo utawarudishia Waisraeli ufalme ?” 7 Yesu akawaambia, “Si juu yenu kufahamu wakati na majira ambayo yamewekwa na Baba kwa mamlaka yake. 8 Lakini mtapokea nguvu akishawajilia Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu na Yudea yote na Samaria, hadi mwisho wa dunia.”
9 Baada ya kusema haya, wakiwa wanatazama, alichukuliwa juu, na wingu likamficha wasimwone tena. 10 Walikuwa bado wakikaza macho yao mawinguni alipokuwa akienda, ndipo ghafla, wanaume wawili waliovaa mavazi meupe walisimama karibu nao, 11 wakasema, “Ninyi watu wa Galilaya, mbona mnasimama hapa mkitazama mbin guni? Yesu huyu huyu aliyechukuliwa mbinguni atarudi tena kama mlivyomwona akienda mbinguni.”

Matendo 2:32-35
32 Huyu Yesu, Mungu alimfufua, na sisi ni mash ahidi wa tukio hilo.
33 “Basi akiwa ametukuzwa na kukaa upande wa kulia wa Mungu, alipokea Roho Mtakatifu aliyeahidiwa na Baba yake. Huyo Roho Mtakatifu ndiye aliyetumiminia haya mnayoyaona na kuyasikia.
34 Daudi hakupaa kwenda mbinguni, lakini alisema, ‘Bwana alim wambia Bwana wangu: kaa upande wangu wa kulia, 35 mpaka nitaka powafanya maadui zako kiegemezo cha miguu yako.’

Waebrania 4:14-16
14 Hivyo basi, kwa kuwa tunaye kuhani mkuu aliyepitia mbingu, Yesu Mwana wa Mungu, tushikilie kwa uthabiti imani yetu tunayoikiri. 15 Kwa maana huyu kuhani wetu mkuu si kuhani ambaye hawezi kutuhurumia katika udhaifu wetu, bali ni kuhani ambaye kwa kila hali amejaribiwa kama sisi, lakini pasipo kutenda dhambi. 16 Kwa hiyo basi, tusogelee kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupokee rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa shida.

Wagalatia 2:15-20
15 Sisi tulio Wayahudi wa kuzaliwa na sio watu wa mataifa ‘wenye dhambi,’16 tunafahamu kwamba mtu hawezi kuhesabiwa haki kwa kutii sheria bali kwa kumwamini Yesu Kristo. Kwa hiyo sisi pia tumemwamini Yesu Kristo ili tupate kuhesabiwa haki kwa kumwa mini Kristo, na wala si kwa kuitii sheria. Maana hakuna mtu ata kayehesabiwa haki kwa kutii sheria. 17 Lakini ikiwa sisi katika jitihada ya kuhesabiwa haki katika Kristo, bado tunaonekana tun gali wenye dhambi, je, hii ina maana kwamba Kristo amekuwa mwene zaji wa dhambi? La hasha! 18 Lakini ikiwa mimi nina jenga tena kile ambacho nimekwisha bomoa, basi ninadhihirisha kwamba mimi ni mvunja sheria.19 Kwa maana mimi kwa njia ya sheria, nimeifia sheria, ili nipate kuishi kwa ajili ya Mungu.
20 Nimesulubiwa pamoja na Kristo; si mimi tena ninayeishi bali ni Kristo anayeishi ndani yangu. Maisha ninayoishi sasa naishi kwa kumwa mini Mwana wa Mungu, aliyenipenda hata akatoa maisha yake kwa ajili yangu.

Waefeso 3:14-21
14 Kwa sababu hii napiga magoti mbele ya Mungu Baba, 15 aliye baba wa familia ya waamini wote, mbinguni na duniani. 16 Namwomba Mungu awaimarishe kwa kuwatia nguvu mioyoni mwenu kwa njia ya Roho wake kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake. 17 Na naomba kwamba, kwa imani, Kristo aendelee kuishi ndani ya mioyo yenu, ili mkiwa mmesimama imara na kujengwa katika upendo, 18 mpate uwezo wa kuelewa, pamoja na watu wote wa Mungu, upana na urefu na kimo na kina cha upendo wa Kristo;19 na mpate kufa hamu upendo huu, ingawa unapita upeo wa maarifa, na hivyo mpate kujazwa kabisa na ukamilifu wa Mungu mwenyewe.
20 Utukufu ni wake yeye, ambaye ana uwezo wa kutenda zaidi ya yale tunayoyaomba na kuyawazia, kwa kadiri ya nguvu yake inayofanya kazi ndani yetu.21 Utukufu ni wake katika kanisa na katika Kristo Yesu kwa vizazi vyote, milele na milele. Amina.

Wakolosai 1:27-29
27 Kwao, Mungu amependa kudhihirisha kati ya mataifa utukufu wa utajiri wa siri hii, yaani, Kristo ndani yenu ndiye tumaini pekee la utu kufu.
28 Kwa sababu hii tunamtangaza Kristo, tukiwaonya na kuwa fundisha watu wote kwa hekima yote ili tuweze kumleta kila mmoja mbele ya Mungu akiwa amekamilika katika Kristo. 29 Kwa shabaha hii nina fanya kazi, nikijitahidi kwa nguvu kuu ya Kristo inay ofanya kazi kwa uwezo mkuu ndani yangu.

1 Petro 3:22
22 Yeye amekwenda mbinguni, na amekaa upande wa kulia wa Mungu pamoja na malaika, mamlaka na nguvu zote zikiwa chini yake.

Marko 6:31
31 Kisha Yesu akawaambia, “Njooni mnifuate peke yenu hadi mahali patulivu na palipo mbali na watu wengine ili mpumzike kidogo”, kwani pale walikuwepo watu wengi wakija na kutoka, nao hawakuwa na nafasi ya kula.

2 Wathesalonike 3:10
10 Tulipokuwa nanyi, tuliwapa kanuni hii: “Yeyote asiyefanya kazi asile.”

Mwanzo 3:15
Name nitaweka uadui kati yako na huyu mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.

Matayo 28:11-15
11 Wakati wale wanawake walipokuwa wanakwenda, baadhi ya wale askari waliokuwa wanalinda kaburi, wakaenda mjini kuwaeleza makuhani wakuu yote yaliyotokea. 12 Baada ya kufanya mkutano na wazee na kushauriana, waliwapa wale askari kiasi fulani cha fedha na 13 kuwaambia, “Semeni, ‘Wanafunzi wake walikuja wakamwiba usiku sisi tukiwa tumelala.’ 14 Kama habari hizi zikimfikia gavana, sisi tutamridhisha na hamtapata shida yo yote.” 15 Kwa hiyo wale askari wakazipokea hizo fedha wakafanya kama walivy oagizwa. Na habari hii imeenea kwa Wayahudi mpaka leo.

1. Matendo 1:1-11
Mpendwa Teofilo, Katika Kitabu changu cha kwanza nilikuan dikia kuhusu mambo yote aliyotenda Yesu, 2 hadi wakati alipopaa mbinguni. Kabla hajachukuliwa juu, aliwapa mitume wake maagizo kwa njia ya Roho Mtakatifu. 3 Alijionyesha kwao akiwa hai muda wa siku arobaini baada ya kufufuka kwake. Akawahakikishia kwa njia nyingi ya kuwa ni yeye na akaongea nao kuhusu Ufalme wa Mungu.
4 Wakati mmoja alipokuwa nao, aliwapa amri hii, “Msiondoke Yerusalemu, mpaka mtakapopokea ahadi aliyotoa Baba, ambayo mmeni sikia nikiizungumzia. 5 Kwa maana Yohana aliwabatiza kwa maji lakini baada ya siku chache mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”
6 Mitume walipokutana na Yesu walimwuliza, “Bwana, wakati huu ndipo utawarudishia Waisraeli ufalme ?”
7 Yesu akawaambia, “Si juu yenu kufahamu wakati na majira ambayo yamewekwa na Baba kwa mamlaka yake. 8 Lakini mtapokea nguvu akishawajilia Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu na Yudea yote na Samaria, hadi mwisho wa dunia.”
9 Baada ya kusema haya, wakiwa wanatazama, alichukuliwa juu, na wingu likamficha wasimwone tena. 10 Walikuwa bado wakikaza macho yao mawinguni alipokuwa akienda, ndipo ghafla, wanaume wawili waliovaa mavazi meupe walisimama karibu nao, 11 wakasema, “Ninyi watu wa Galilaya, mbona mnasimama hapa mkitazama mbin guni?
Yesu huyu huyu aliyechukuliwa mbinguni atarudi tena kama mlivyomwona akienda mbinguni.”

Luke 24:36-44
36 Wakati walipokuwa wanazungumza hayo, Yesu mwenyewe akasi mama katikati yao akawasalimu, “Amani iwe nanyi.”
37 Wakashtuka na kuogopa wakidhani wameona mzimu. 38 Lakini akawauliza, “Kwa nini mnaogopa? Kwa nini mna mashaka mioyoni mwenu?39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu mwone kuwa ni mimi. Niguseni mwone. Mzimu hana nyama na mifupa kama mnion avyo.” 40 Aliposema haya aliwaonyesha mikono yake na miguu yake. 41 Wakashindwa kuamini kwa ajili ya furaha na mshangao waliokuwa nao. Akawauliza, “Mna chakula cho chote hapa?” 42 Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa,43 akakichukua akakila mbele yao.
44 Akawaambia, “Haya ndiyo mambo niliyowaambia nilipokuwa pamoja nanyi; kwamba yote yaliyoandikwa kunihusu mimi katika she ria ya Musa, katika Maandiko ya manabii na Zaburi hayana budi kutimizwa.”

2. a. Yohana 20:14-18
14 Alipokuwa akisema haya akageuka, akamwona Yesu amesimama nyuma yake, lakini hakumtambua! 15 Yesu akamwambia, “Mama, mbona unalia? Unamta futa nani?” Mariamu alidhani aliyekuwa anaongea naye ni mtunza bustani, kwa hiyo akajibu, “Kama ni wewe umemchukua tafadhali nionyeshe ulipomweka ili nimchukue.” 16 Yesu akamwita, “Mar iamu.” Ndipo Mariamu akamgeukia Yesu, akamwambia kwa Kiebrania, “Rabboni!’ 17 Yesu akamwambia, “Usin ishike kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ninakwenda kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu.” 18 Kwa hiyo Mariamu Magdalena akaenda akawakuta wanafunzi akawaambia, “Nimemwona Bwana!”

b. Luka 24:13-15
13 Siku hiyo hiyo, wanafunzi wawili wa Yesu walikuwa wanak wenda kijiji cha Emau, yapata maili saba kutoka Yerusalemu, 14 nao walikuwa wakizungumzia mambo yote yaliyotokea. 15 Wali pokuwa wakizungumza, Yesu mwenyewe alikuja akatembea pamoja nao,

c. Yohana 20:26-29
26 Wakashindwa kumkamata kwa maneno aliyosema mbele ya watu. Jibu lake liliwashangaza mno, wakakosa la kusema. Yesu Afundisha Kuhusu Ufufuo
27 Baadhi ya Masadukayo , wale wanaosema kwamba hakuna ufu fuo wa wafu, wakamjia Yesu wakamwuliza, 28 “Mwalimu, katika sheria ya Musa , tunasoma kwamba kama mtu akifariki akamwacha mkewe bila mtoto, basi kaka yake amwoe huyo mjane ili amzalie marehemu watoto. 29 Walikuwepo ndugu saba. Wa kwanza akafa bila kuzaa mtoto.

d. 1 Wakorintho 15:5
5 Na kwamba alimto kea Kefa, kisha akawatokea wale kumi na wawili.

e. Yohana 21:1
Baada ya haya Yesu alijitambulisha tena kwa wanafunzi wake kando ya bahari ya Tiberia. Ilitokea hivi:

f.1 Wakorintho 15:6
6 Baadaye akawa tokea ndugu waamini zaidi ya mia tano kwa pamoja, na wengi wao wangali hai, ingawa wengine wameshakufa.

g. 1 Wakorintho 15:7
7 Kisha akamtokea Yakobo, na ndipo akawatokea mitume wote.

3. Waebrania 12:2
2 Tumtazame Yesu aliyeanzisha na anayekamilisha imani yetu. Yeye, kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake, alivumilia kifo cha msalaba bila kujali aibu, na sasa ameketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.

4. Waebrania 7:24-25
24 Lakini yeye anaendelea na ukuhani wake daima kwa maana anaishi milele. 25 Kwa hiyo anaweza kwa wakati wote kuwaokoa wale wanaomkaribia Mungu kupitia kwake, kwa sababu yeye anaishi daima ili kuwaombea.

Yohana 14:16-20
16 Nami nitam womba Baba, naye atawapeni Msaidizi mwingine akae nanyi siku zote. 17 Huyo ndiye Roho wa Kweli ambaye watu wasioamini hawawezi kumpokea. Watu kama hao hawamwoni wala hawamfahamu. Ninyi mnamfahamu kwa kuwa anakaa ndani yenu na ataendelea kuwa nanyi. 18 Sitawaacha kama yatima. Nitarudi kwenu.
19 Baada ya muda mfupi watu wa ulimwengu hawataniona tena, ila ninyi mta niona; na kwa kuwa mimi ni hai, ninyi pia mtakuwa hai. 20 Wakati huo utakapofika mtajua ya kuwa mimi niko ndani ya Baba yangu na ninyi mko ndani yangu.

Tito 3: 4-7
4 Lakini wakati wema na upendo wa Mungu Mkombozi wetu ulipodhihirishwa, 5 ali tuokoa, si kwa sababu ya matendo mema ya haki tuliyotenda, bali kwa sababu ya huruma yake. Alituokoa kwa kuoshwa na kuzaliwa mara ya pili na kufanywa wapya kwa njia ya Roho Mtakatifu, 6 ambaye Mungu alitumiminia kwa wingi kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu. 7 Na tukishahesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele tunaoutumainia .

5. Warumi 5:8-9
8 Lakini Mungu anaudhihirisha upendo wake kwetu kwamba: tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo ali kufa kwa ajili yetu.
9 Basi, kwa kuwa tumekwisha kuhesabiwa haki kwa damu yake, bila shaka atatuokoa kutoka katika ghadhabu ya Mungu.

Warumi 5:10
10 Kwa kuwa kama tulipokuwa maadui wa Mungu tulipatanishwa kwa kifo cha Mwanae, bila shaka sasa kwa kuwa tumepatanishwa, tutaokolewa kwa uzima wake.

Yohana 6:37
37 Wale wote ambao Baba amenipa watakuja kwangu na ye yote ajaye kwangu, sitamtupa nje kamwe.

Matayo 11:28
28 “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

7. a. Wagalatia 2:20
20 Nimesulubiwa pamoja na Kristo; si mimi tena ninayeishi bali ni Kristo anayeishi ndani yangu. Maisha ninayoishi sasa naishi kwa kumwa mini Mwana wa Mungu, aliyenipenda hata akatoa maisha yake kwa ajili yangu.

b.1 Korintho 3:16-17
16 Je, hamjui kwamba ninyi ni Hekalu la Mungu, na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? 17 Kama mtu ye yote akiliharibu Hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa sababu Hekalu la Mungu ni takatifu, na ninyi ni Hekalu hilo.

1 Korintho 6:19
16 Hamjui kwamba mtu aushirikishaye mwili wake na kahaba ana kuwa mmoja naye kimwili? Maandiko yanasema, “Hao wawili watakuwa mwili mmoja.”

c. Warumi 8:9-11
9 Lakini ninyi hamuishi kwa kufuata matakwa ya mwili, bali mnaongozwa na Roho; ikiwa kweli Roho wa Mungu anaishi ndani yenu. Mtu ye yote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo. 10 Lakini kama Kristo anaishi ndani yenu, ingawa miili yenu imekufa kwa sababu ya dhambi, roho zenu zinaishi kwa sababu mmek wisha kuhesabiwa haki. 11 Na ikiwa Roho wa Mungu ambaye alimfu fua Yesu kutoka kwa wafu anaishi ndani yenu, Mungu aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataipatia uzima miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya huyo Roho wake ambaye anaishi ndani yenu.

Isaya 57:15
Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele, ambaye jina lake ni mtakatifu; asema hivi; nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja nay eye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufu roho za wanyenyekevu, na kuifufu mioyo yao waliotubu.

Matendo 4:12
Yesu peke yake ndiye anayeweza kuokoa watu. Jina lake ndiyo nguvu pekee iliyotolewa kumwokoa mtu yeyote ulimwenguni. Ni lazima tuokoke kupitia yeye!”


 
 

The Guide has her own Guidebook to help her lead and guide the lesson.

Swahili Lesson #5 Guidebook (to be translated)

Download Swahili Guidebook Bible Verses Swahili Lesson #5

Mistari ya Biblia

 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us