Project Hope     home >>stonecroft>> mwongozo >> yesu ni nani somo 4 >> mistari ya biblia
Mistari ya Biblia - Somo #4
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

SOMO LA NNE

KWA NINI YESU ALIKUJA?

Kitabu mwongozo

Mistari ya Biblia

Kujisomea Biblia kwa Juma

Mathayo 5:1-2, 17-20
Yesu alipoona umati wa watu, alipanda mlimani akaketi chini. Wanafunzi wake wakamjia, 2 naye akaanza kuwafundisha akisema: 17 “Msidhani kwamba nimekuja kufuta sheria ya Musa na mafundisho ya manabii. kwamba mpaka mbingu na dunia zitaka potoweka, hakuna hata herufi moja ya sheria itakayopotea mpaka shabaha yake ikamilike. 19 Kwa hiyo ye yote atakayelegeza hata mojawapo ya amri ndogo kuliko amri zote na akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa mbinguni. Sikuja kuzifuta bali kuzitimiza. 18 Kwa maana ninawaambia hakika Lakini atakayetii amri hizi na kuwafundisha wengine kuzitii a taitwa mkuu katika Ufalme wa mbinguni. 20 Kwa maana nawaambieni, ikiwa haki yenu haitazidi haki ya waandishi wa sheria na Mafari sayo, hamtaingia katika Ufalme wa mbinguni kamwe.”

Yohana 6:35-38
35 Yesu akawaambia, “Mimi ndiye mkate wa uzima. Ye yote ajaye kwangu hataona njaa kamwe, na ye yote aniaminiye, hataona kiu kamwe. 36 Lakini kama nilivyokwisha waambia, mnaniona lakini bado hamtaki kuamini. 37 Wale wote ambao Baba amenipa watakuja kwangu na ye yote ajaye kwangu, sitamtupa nje kamwe. 38 Kwa maana sikushuka kutoka mbinguni nije kutimiza mapenzi yangu, bali nitimize mapenzi yake yeye aliyenituma.

Matendo 2:23-24
23 Huyu Yesu ali tiwa mikononi mwenu kwa mpango na makusudi ya Mungu aliyoyafahamu tangu awali. Nanyi mlimwua kwa kumtundika na kumpigilia misumari msalabani, mkisaidiwa na watu waovu. 24 Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu akamwondolea uchungu wa mauti, kwa sababu hata kifo kisingaliweza kumzuia.

1 Yohana 3:5-6
5 Yesu akamwambia, “Ninakuambia hakika, kama mtu hakuzaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia katika Ufalme wa Mungu. 6 Mtu huzaliwa kimwili na wazazi wake, lakini mtu huzaliwa kiroho na Roho wa Mungu.

Waebrania 2:14-15
14 Basi, kwa kuwa watoto hao wana mwili na damu, yeye pia alishiriki katika ubinadamu wao, ili kwa kufa kwake apate kumwan gamiza yule mwenye mamlaka juu ya kifo, yaani shetani; 15 na hivyo awaweke huru wale ambao walikuwa utumwani maisha yao yote kwa sababu ya kuogopa kifo.

Ufunuo 3:20-21
20 Tazama, nasimama mlangoni napiga hodi. Mtu ye yote akisikia sauti yangu na kufun gua mlango, nitaingia ndani na kula pamoja naye, naye pamoja nami. 21 Atakayeshinda nitampa haki ya kuketi pamoja nami kwenye kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu kwenye kiti chake cha enzi.

Ufunuo 5:9-10
9 Nao wakaimba wimbo mpya: “Wewe unastahili kuichukua hati na kuifungua mihuri yake. Kwa sababu wewe uliuawa na kwa damu yako ukamnunulia Mungu watu kutoka katika kila kabila na kila lugha; watu wa kila jamaa na kila taifa. 10 Umewafanya hawa wawe ufalme na makuhani wa kumtumikia Mungu wetu, na watata wala ulimwenguni.”

Isaya 9:6
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume; na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; naye ataitwa jina lake, Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.

Isaya 35:4-6
….jipeni moyo, msiogope; tazama, mung wenu atakuja na kisasi, na malipo ya mungu; atakuja na kuwaokoa ninyi.
Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuliwa.
Ndipo mtu aliye kilema ataruka ruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba; maana katika nyika maji yatabubujika; na vijito jangwani.

1.a. Mathayo 5:17
17 “Msidhani kwamba nimekuja kufuta sheria ya Musa na mafundisho ya manabii. kwamba mpaka mbingu na dunia zitaka potoweka, hakuna hata herufi moja ya sheria itakayopotea mpaka shabaha yake ikamilike.

b. Yohana 1:18
18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Lakini Mwanae pekee, ambaye ana uhusiano wa karibu sana na Baba yake, amemdhihirisha Mungu kwetu.

c. Mathayo 20:28
28 kama vile ambavyo mimi Mwana wa Adamu sikuja ili nitumikiwe bali kutumika na kutoa maisha yangu kuwa fidia kwa ajili ya watu wengi.”

d. Luka 4:42-43
42 Kesho yake, kulipopambazuka, Yesu alikwenda mahali pa faragha. Watu wengi wakawa wanamtafuta kila mahali, na walipom wona wakajaribu kumzuia asiondoke. 43 Lakini yeye akawaambia, “Ninao wajibu wa kuhubiri Habari Njema za Ufalme wa Mungu sehemu nyingine pia. Hii ndio sababu nilitumwa.”

e. Luka 19:10
10 Kwa maana mimi Mwana wa Adamu nimekuja kutafuta na kuokoa waliopotea.”

f. Yohana 3:17
17 Maana Mungu hakumtuma Mwanae kuuhukumu ulimwengu bali auokoe ulimwengu.

g. Yohana 10:7-10
7 Kwa hiyo Yesu akasema nao tena akawaambia, “Mimi ni mlango wa kupitia kondoo. 8 Wote walionitangulia ni wezi na wany ang’anyi. Hata hivyo kondoo hawakuwafuata. 9 Mimi ni mlango; mtu ye yote anayeingia zizini kwa kupitia kwangu atakuwa salama, naye ataingia na kutoka na kupata malisho. 10 Mwizi huja kwa nia ya kuiba, kuua na kuharibu. Nimekuja ili watu wapate uzima; uzima ulio kamili.

h. 1 Timotheo 1:15
15 Neno hili ni la hakika tena linastahili kukubalika kabisa, kwamba Kristo Yesu alikuja duniani kuokoa wenye dhambi, ambao kati yao, mimi ni mwenye dhambi kuliko wote.

Isaya 14:12-14
Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi, jinsi ulivyokatwa kabisa, ewe uliyewaangusha mataifa.
Nawe ulisema moyoni mwako, nitapanda mpaka mbiguni, nitakiinua kiti change juu, kuliko nyota za mungu; name nitaketi juu yam lima wa mkutano, katika pande za mwisho za kaskazini.
Nitapaa kupita vimo vya mawingu, nitafanana nay eye aliye juu.

Warumi 5:12
12 Kwa hiyo kama vile ambavyo dhambi iliingia ulimwenguni kupitia kwa mtu mmoja, na dhambi ikaleta kifo, na kwa njia hiyo kifo kikawajia watu wote kwa kuwa wote walitenda dhambi -

Matendo Ya Mitume 4:11-12
11 Huyu Yesu ndiye ‘lile jiwe ambalo ninyi wajenzi mlilikataa, ambalo limekuwa jiwe kuu la pembeni.’ 12 Wokovu unapatikana kwake tu; kwa maana hakuna jina jingine duniani ambalo wamepewa wanadamu kuwaokoa ila jina la Yesu, na ni kwa jina hilo peke yake tunaweza kuokolewa!”

Mark1:11
11 Na sauti kutoka mbinguni ikasema, “Wewe ni mwanangu mpendwa; nimependezwa nawe.”

2. a. Luka 18:29-33
29 Yesu akajibu, “Nawaam bia hakika, hakuna hata mmoja aliyeacha nyumba yake, au mke, ndugu, wazazi au watoto kwa ajili ya Ufalme wa Mungu,
30 ambaye hatapewa na Mungu mara nyingi zaidi ya hivyo katika maisha haya na kupata uzima wa milele katika maisha yajayo.” 32 Nitatiwa mikononi mwa watawala wa Kirumi. Watu watanizomea, watanitukana na kunitemea mate. 33 Watanipiga na kuniua, lakini siku ya tatu nitafufuka.”

b. Mathayo 12:38-40
38 Kisha baadhi ya waandishi wa sheria na Mafarisayo wakam wambia, “Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.” 39 Lakini yeye akawajibu, “Kizazi cha watu waovu na wasiowaami nifu hutafuta ishara; lakini hawatapewa ishara yo yote isipokuwa ile ya nabii Yona. 40 Kwa maana kama vile Yona alivyokaa katika tumbo la nyangumi kwa muda wa siku tatu mchana na usiku, vivyo hivyo mimi Mwana wa Adamu nitakaa siku tatu, mchana na usiku ndani ya ardhi.

c. Marko 8:31-32a
31 Akaanza kuwafundisha wanafunzi wake kuwa yeye, Mwana wa Adamu, atapata mateso mengi na kukataliwa na wazee, na makuhani wakuu na walimu wa sheria; na kwamba atauawa na baada ya siku tatu atafufuka.32 Aliyasema haya wazi wazi.

3. Luka 23:4
4 Pilato akawaambia maku hani wakuu na watu wote waliokuwapo, “Sioni sababu ya kutosha kumshtaki huyu mtu!”

4. Marko 14:61-64
61 Lakini Yesu alikaa kimya; hakusema neno lo lote. Kuhani Mkuu akamwuliza, “Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu Mtu kufu?” 62 Yesu akajibu, “Mimi ndiye, na mtaniona mimi Mwana wa Adamu nimeketi upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi, na nikija na mawingu ya mbinguni.”
63 Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akasema, “Tuna haja gani tena ya mashahidi? 64 Ninyi wote mmemsikia akikufuru! Mna toa hukumu gani?” Wote wakamhukumu kwamba ana hatia na auawe.

Isaya 53:3-6
Alidharauliwa na kukataliwa na watu; mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, alidharauliwa na wala hatukumhesabu kuwa kitu.
Hakika ameyachukua masikitiko yetu, amejitwika huzuni zetu; lakini tulimzania ya kuwa amepigwa,amepigwa na mungu na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu alichubuliwa kwa maovu yetu, adhabu ya amani yetu ilikua juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Sisi sote kama kondoo tumepotea; kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; na Bwana ameweka juu yake maovu yetu sisi sote.

5. Marko 14:43-15:47
43 Yesu alipokuwa bado anazungumza, Yuda, mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili, akafika pamoja na umati wa watu wenye mapanga na marungu. Watu hao walikuwa wametumwa na makuhani wakuu, waandishi, na wazee. 44 Yuda, yule msaliti, alikuwa amewapa ishara wale watu kuwa, “Yule nitakayembusu, ndiye mnayemtaka, mkamateni na kumchukua akiwa chini ya ulinzi.”
45 Kwa hiyo Yuda alipofika, alimwendea Yesu akamwambia, “Mwalimu,” akambusu. 46 Wakamkamata Yesu, wakamweka chini ya ulinzi. 47 Lakini mmoja wa wale waliokuwa wamesimama hapo aka chukua upanga akampiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio. 48 Kisha Yesu akasema, “Mbona mmekuja kunikamata kwa mapanga na marungu? Kwani mimi ni jambazi?49 Siku zote nilikuwa pamoja nanyi nikifundisha Hekaluni wala hamkunikamata. Lakini Maandiko lazima yatimie. ” 50 Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha, wakakimbia. 51 Kijana mmoja aliyekuwa amevaa shuka tu alikuwa akimfuata Yesu. Walipomkamata, 52 alikimbia uchi, akaacha shuka lake.
53 Kisha wakampeleka Yesu nyumbani kwa kuhani mkuu ambapo makuhani wakuu, wazee, na walimu wa sheria walikuwa wamekuta nika. 54 Petro aliwafuata kwa mbali, akaingia barazani kwa kuhani mkuu, akaketi pamoja na walinzi akiota moto. 55 Makuhani wakuu na wajumbe wote wa Baraza walijaribu kutafuta ushahidi wa kumshtaki Yesu ili wapate kumwua, lakini hawakupata. 56 Wengi walitoa ushahidi wa uongo, lakini ushahidi wao haukupatana.
57 Ndipo watu fulani wakasimama wakatoa ushahidi wa uongo wakisema,58 “Sisi tulimsikia akisema, ‘Mimi nitabomoa Hekalu hili lililojengwa na wanadamu, na katika siku tatu nitajenga lin gine ambalo halikujengwa na wanadamu.’ ” 59 Lakini hata hawa, ushahidi wao ulipingana.
60 Kuhani Mkuu akasimama mbele ya Baraza akamwuliza Yesu, “Huwezi kujibu mashtaka haya ambayo watu hawa wameleta juu yako?” 61 Lakini Yesu alikaa kimya; hakusema neno lo lote. Kuhani Mkuu akamwuliza, “Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu Mtu kufu?” 62 Yesu akajibu, “Mimi ndiye, na mtaniona mimi Mwana wa Adamu nimeketi upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi, na nikija na mawingu ya mbinguni.”
63 Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akasema, “Tuna haja gani tena ya mashahidi? 64 Ninyi wote mmemsikia akikufuru! Mna toa hukumu gani?” Wote wakamhukumu kwamba ana hatia na auawe.
65 Kisha baadhi ya watu wakaanza kumtemea mate; wakamfunga kitambaa usoni wakampiga na kumwambia, “Toa unabii, utuambie nani amekupiga!” Maaskari wakampokea kwa mapigo.
66 Petro alikuwa bado yuko barazani. Kisha akaja mtumishi mmoja wa kike wa kuhani mkuu. 67 Alipomwona Petro akiota moto, alimtazama sana, akamwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu Mnazareti.” 68 Lakini Petro akakataa, akasema, “Sijui wala sielewi unalosema,” akaondoka akaenda mlangoni. 69 Yule mtumi shi wa kike akamwona, akawaambia tena wale waliokuwa wamesimama pale, “Huyu mtu ni mmoja wao.” 70 Lakini Petro akakana tena. Baada ya muda kidogo wale waliokuwa wamesimama hapo pamoja naye wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana wewe pia ni Mgalilaya!” 71 Petro akaanza kulaani na kuapa, akawaambia, “Simjui huyo mtu mnayemsema.”
72 Hapo hapo jogoo akawika mara ya pili. Petro akakumbuka lile neno ambalo Yesu alikuwa amemwambia, “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Akalia kwa uchungu. Pilato Anamhoji Yesu

Kulipopambazuka, makuhani wakuu walifanya mkutano pamoja na wazee na walimu wa sheria, na Baraza zima likafanya mashauri. Wakamfunga Yesu, wakamchukua na kumkabidhi kwa Pilato. 2 Pilato akamwuliza, “Wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Wewe ndiye uliyesema maneno hayo.” 3 Makuhani wakuu wakamsh taki kwa mambo mengi. 4 Pilato akamwuliza tena, “Huna la kujibu?
5 Yesu hakusema neno. Pilato akashangaa.
6 Ilikuwa desturi wakati wa sherehe za Pasaka kumfungulia mfungwa ye yote ambaye watu walimtaka . 7 Wakati huo, mtu mmoja aitwaye Baraba alikuwa amefungwa gerezani pamoja na wahalifu wen gine kwa makosa ya kusababisha uasi ambapo mauaji yalitokea. 8 Basi watu waliokusanyika walimjia Pilato wakamwomba awafanyie kama ilivyokuwa desturi wakati wa Pasaka. 9 Pilato akawauliza, “Mnataka nimfungue huyu mfalme wa Wayahudi?” 10 Alikuwa ana fahamu kwamba wakuu wa makuhani walikuwa wanamwonea Yesu wivu ndio sababu wakamshtaki kwake. 11 Lakini makuhani wakuu wakawa chochea watu wamwombe awafungulie Baraba.
12 Pilato akawauliza tena watu, “Nimfanye nini huyu mtu mnayemwita mfalme wa Wayahudi?” 13 Wakapiga kelele, “Msulub ishe!” 14 Akawauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakapiga kelele kwa nguvu zaidi, “Msulubishe!”
15 Pilato alitaka kuwaridhisha watu, kwa hiyo akamfungulia Baraba; na baada ya kuamuru Yesu apigwe mijeledi, akamtoa asulub ishwe.
16 Maaskari wakampeleka Yesu hadi kwenye ukumbi wa ndani ya Ikulu iliyoitwa Praitoria, wakakusanya kikosi kizima cha askari. 17 Wakamvika Yesu vazi la zambarau, wakatengeneza taji ya miiba, wakamvika.
18 Wakaanza kumsalimu kwa dhihaka, “Salamu, Mfalme wa Wayahudi!” 19 Wakampiga kwa fimbo kichwani, wakamte mea mate. Wakamdhihaki kwa kupiga magoti kama vile wanamheshimu mfalme. 20 Walipokwisha kumdhihaki, walimvua lile vazi la zam barau, wakamvika nguo zake. Kisha wakamtoa nje wakamsulubishe.
21 Walipokuwa wakienda kumsulubisha, njiani walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni, raia wa Kirene. Yeye alikuwa baba yao Aleksanda na Rufas. Alikuwa anakuja mjini kutoka shamba. Wakamla zimisha abebe msalaba wa Yesu. 22 Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahali palipoitwa Golgota, -yaani Mahali pa Fuvu la Kichwa.
23 Wakampa divai iliyochanganywa na manemane, lakini akaikataa. 24 Basi wakamsulubisha, wakagawana nguo zake kwa kuzipigia kura kuamua kila mtu achukue nini.
25 Ilikuwa yapata saa tatu asubuhi walipomsulubisha. 26 Tangazo la mashtaka yake liliandikwa maneno haya: “MFALME WA WAYAHUDI.”27 Majambazi wawili walisulubiwa pamoja naye, mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wa kushoto. [ 28 Na kwa njia hii yale Maandiko yasemayo, “Alihesabiwa pamoja na wenye hatia,” yalitimia.] 29 Watu waliokuwa wakipita, walimtukana na kutikisa vichwa vyao kwa mzaha wakasema, “Si ulikuwa ukisema kwamba unaweza kulivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu? 30 Shuka msalabani basi, ujiokoe mwenyewe!”31 Hali kadhalika makuhani wakuu na walimu wa sheria walimdhihaki wakisema, “Ali waokoa wengine lakini anashindwa kujiokoa mwenyewe.32 Kristo mfalme wa Wayahudi ashuke basi msalabani ili tupate kuona na kuamini!” Na wale waliosulubiwa pamoja naye pia walimtukana.
33 Ilipofika saa sita, giza lilikumba nchi nzima kwa muda wa saa tatu.34 Ilipofika saa tisa, Yesu akalia kwa sauti kuu “Eloi, Eloi lama Sabaktani?” Yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” 35 Baadhi ya watu waliokuwa wanasimama karibu waliposikia maneno hayo, walisema, “Mnamsikia? Anamwita
36 Mtu mmoja akaenda mbio, akachovya sponji kwenye divai na siki, akaiweka kwenye ufito akamwinulia Yesu ili anywe huku akisema, “Hebu tuone kama Eliya atakuja kumshusha kutoka msala bani!”
37 Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho. 38 Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili kuanzia juu hadi chini.
39 Yule askari aliyekuwa amesimama mbele ya msalaba alipoona jinsi alivyokata roho, akasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”
40 Walikuwapo pia wanawake walio kuwa wakiangalia mambo haya kwa mbali. Kati yao walikuwapo Mariamu Magdalena, na Mariamu mama yao Yakobo mdogo na Yose, na pia Salome . 41 Hawa walifuatana na Yesu alipokuwa Galilaya na kumhudumia. Pia walikuwapo wanawake wengine wengi waliokuwa wamekuja naye Yerusalemu.
42 Ilipofika jioni, kwa kuwa ilikuwa siku ya Maandalizi, siku moja kabla ya Pasaka, 43 Yusufu wa Arimathea alijikaza akamwendea Pilato akamwomba auchukue mwili wa Yesu. Yeye alikuwa ni mjumbe wa Baraza aliyeheshimika, ambaye alikuwa anatazamia kuja kwa Ufalme wa Mungu. 44 Pilato alishangaa kusikia kwamba Yesu amekwisha kufa. Kwa hiyo akamwita askari amhakikishie kuwa kweli amekufa. 45 Baada ya kuhakikishiwa na yule askari kwamba kweli amekufa, Pilato alimpa Yusufu ruhusa ya kuuchukua mwili wa Yesu. 46 Basi Yusufu alinunua sanda ya kitani, akautoa mwili wa Yesu msalabani; akamzungushia sanda, akamweka ndani ya kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kisha akaviringisha jiwe akaufunika mlango wa kaburi.47 Mariamu Magdalena na Mariamu mama wa Yose walipaona mahali alipozikwa Yesu.

Mathayo 27:27-28:15
27 Kisha askari wa gavana wakampeleka Yesu kwenye makao makuu ya gavana wakakusanya kikosi cha askari, wakamzunguka Yesu.
28 Wakamvua nguo zake, wakamvika kanzu ya rangi nyekundu.29 Wakasokota taji ya miiba wakamvika kichwani. Wakamwekea fimbo mkono wake wa kulia, wakapiga magoti mbele zake wakamdhihaki wakisema, “Uishi maisha marefu, mfalme wa Wayahudi!” 30 Wakamtemea mate, wakachukua ile fimbo wakampiga nayo kich wani. 31 Baada ya kumdhihaki, walimvua ile kanzu, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakampeleka kumsulubisha.
32 Walipokuwa wakienda, walikutana na mtu mmoja wa Kirene aitwaye Simoni, wakambebesha ule msalaba kwa nguvu. 33 Na wali pofika sehemu iitwayo Golgotha, maana yake mahali pa Fuvu la Kichwa, 34 wakampa divai iliyochanganywa na nyongo ili anywe; lakini baada ya kuionja, akaikataa.
35 Walipokwisha kumsulubisha wakagawana nguo zake kwa kuzi pigia kura.36 Kisha wakaketi, wakamchunga. 37 Juu ya kichwa chake, kwenye msalaba, wakaandika shtaka lake: ‘HUYU NI YESU, MFALME WA WAYAHUDI.’38 Wanyang’anyi wawili walisulubiwa pamoja naye, mmoja kulia kwake na mwingine kushoto kwake.
39 Watu waliokuwa wakipita njiani walimtukana, wakatikisa vichwa vyao 40 na kusema, “Si ulisema ungevunja Hekalu na kulijenga kwa muda wa siku tatu? Jiokoe basi! Kama wewe ni Mwana wa Mungu shuka msalabani.” 41 Hali kadhalika, makuhani wakuu, walimu wa sheria na wazee walimdhihaki, wakisema, 42 “Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe. Yeye si Mfalme wa Israeli? Ashuke kutoka msalabani nasi tutamwamini.
43 Anamwamini Mungu; basi Mungu na amwokoe sasa kama anamtaka. Kwa maana alisema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu.’ ” 44 Hata wale wanyang’anyi waliosulubiwa naye walimtukana kwa njia hiyo hiyo.
45 Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa, nchi nzima ilikuwa giza. 46 Mnamo saa tisa Yesu akalia kwa sauti kuu, “Eli, Eli lama sabakthani?” Yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona ume niacha?”
47 Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama hapo waliposikia haya walisema, “Anamwita Eliya!” 48 Mmoja wao akaenda mbio akaleta sponji akaichovya kwenye siki akaiinua kwa mwanzi akamwekea mdo moni. 49 Lakini wengine wakasema, “Hebu tuone kama Eliya ata kuja kumwokoa.” [Na mwingine akachukua mkuki akamchoma ubavuni, pakatoka maji na damu].
50 Yesu akalia tena kwa sauti kuu, kisha akakata roho. 51 Wakati huo huo pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili, kuanzia juu hadi chini. Dunia ikatetemeka na miamba ikapasuka. 52 Makaburi yakafunguka na miili ya watakatifu waliofariki ili fufuka. 53 Walitoka makaburini na Yesu alipofufuka walikwenda Mji Mtakatifu wakawatokea watu wengi. 54 Basi yule jemadari na wale waliokuwa naye wakimlinda Yesu walipoona lile tetemeko na yote yaliyotokea, waliogopa wakasema, “Hakika, huyu alikuwa
55 Wanawake wengi walio kuwa wamefuatana na Yesu tangu Gali laya wakimhudumia, nao walikuwapo wakitazama kwa mbali yote yali yotokea.56 Kati yao walikuwapo Mariamu Magdalena, Mariamu mama yake Yakobo na Yusufu na mama yao wana wa Zebedayo.
57 Ilipofika jioni, alifika tajiri mmoja kutoka Arimathea aitwaye Yusufu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu. 58 Akaenda kwa Pilato akaomba mwili wa Yesu. Pilato akaamuru apewe. 59-60 Yusufu alichukua mwili wa Yesu akauweka katika sanda safi akauzika katika kaburi lake jipya ambalo lilikuwa limechongwa kwenye mwamba. Kisha akaviringisha jiwe kubwa akafu nika mlango wa kaburi, akaondoka. 61 Mariamu Magdalena na yule Mariamu mwingine walikuwa wamekaa mbele ya kaburi.
62 Siku iliyofuata, yaani siku iliyofuata ile siku ya Maan dalizi ya sabato, makuhani wakuu na Mafarisayo walimwendea Pilato 63 wakamwambia, “Tunakumbuka kwamba yule mwongo alisema, ‘Baada ya siku tatu nitafufuka.’ 64 Tunaomba uamuru kwamba kabu ri liwekewe ulinzi hadi siku ya tatu. Vinginevyo wanafunzi wake wanaweza wakaja wakauiba mwili wake na kuwaambia watu kwamba amefufuka. Jambo hili likitokea uongo huu wa mwisho utakuwa mbaya zaidi ya ule wa kwanza.” 65 Pilato akawaambia, “Ninyi mnao askari. Nendeni mkaweke ulinzi, mhakikishe pamekuwa salama kama mpendavyo.” 66 Wakaenda wakaweka ulinzi kaburini, wakaliwekea lile jiwe mhuri na kuwaweka askari walinzi.

Baada ya Sabato, alfajiri mapema siku ile ya Jumapili, Mari amu Magdalena na yule Mariamu mwingine walikwenda kuliangalia kaburi. 2 Ghafla pakatokea tetemeko kubwa la ardhi; kwa sababu Malaika wa Bwana alikuja kutoka mbinguni akalisogeza lile jiwe, akalikalia. 3 Malaika huyo alifanana kama umeme na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji. 4 Wale walinzi wa kaburi walipomwona walitetemeka kwa hofu, wakawa kama wamekufa.
5 Lakini yule malaika akawaambia wale wanawake, “Msiogope. Ninajua kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa. 6 Hayupo hapa. Amefu fuka kama alivyosema. Njooni muone pale alipokuwa amelazwa. 7 Kisha nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake hivi, amefufuka kutoka kwa wafu naye amewatangulia kwenda Galilaya, mtamwona huko. Sasa nimekwisha waambia.” 8 Wakiwa wamejawa na hofu na furaha nyingi, wale wanawake waliondoka upesi pale kaburini, wakaenda mbio kuwaeleza wanafunzi habari hizo.
9 Mara, Yesu akawatokea, akawasalimia, “Salamu!” Wale wana wake wakamwendea wakajitupa chini wakaishika miguu yake, wakam wabudu.10 Ndipo Yesu akawaambia, “Msiogope. Nendeni mkawaambie ndugu zangu waende Galilaya, wataniona huko.”
11 Wakati wale wanawake walipokuwa wanakwenda, baadhi ya wale askari waliokuwa wanalinda kaburi, wakaenda mjini kuwaeleza makuhani wakuu yote yaliyotokea. 12 Baada ya kufanya mkutano na wazee na kushauriana, waliwapa wale askari kiasi fulani cha fedha na 13 kuwaambia, “Semeni, ‘Wanafunzi wake walikuja wakamwiba usiku sisi tukiwa tumelala.’ 14 Kama habari hizi zikimfikia gavana, sisi tutamridhisha na hamtapata shida yo yote.” 15 Kwa hiyo wale askari wakazipokea hizo fedha wakafanya kama walivy oagizwa. Na habari hii imeenea kwa Wayahudi mpaka leo.

Yohana 19:16-21:25
16 Ndipo Pilato akawaka bidhi Yesu wamsulubishe.
17 Kwa hiyo wakamchukua Yesu, naye akatoka akiwa amebeba msalaba wake kuelekea mahali palipoitwa, ‘Fuvu la kichwa,’ au kwa Kiebrania, Golgotha. 18 Hapo ndipo walipomsulubisha. Pamoja naye walisulubishwa watu wengine wawili, mmoja upande wa kushoto na mwingine upande wa kulia wa Yesu. 19 Pilato aliandika maneno yafuatayo kwenye kibao, kikawekwa juu kwenye msalaba wa Yesu: “YESU WA NAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI”
20 Kwa kuwa mahali hapo palikuwa karibu na mjini, Wayahudi wengi walisoma maneno haya ambayo yalikuwa yameandikwa kwa lugha za Kiebrania, Kilatini na Kigiriki. 21 Makuhani wakuu wakamwambia Pilato, “Usiandike, ‘Mfalme wa Wayahudi,’ bali ‘Mtu huyu alisema, Mimi ni Mfalme wa Wayahudi.”’ 22 Pilato akawajibu, “ Nilichokwisha andika, nimeandika.”
23 Maaskari walipokwisha msulubisha Yesu, walichukua mavazi yake wakayagawa mafungu manne; kila askari akapata moja. Ila wal ikubaliana wasipasue ile kanzu yake kwa maana ilikuwa imefumwa tangu juu hadi chini na haikukatwa mahali po pote. 24 Wakaam biana, “Tusiipasue ila tupige kura tuone ni nani aichukue.” Hii ilitimiza yale Maandiko yaliyosema, “Waligawana mavazi yangu, na kanzu yangu wakaipigia kura.” 25 Kwa hiyo wakapiga kura. Karibu na msalaba wa Yesu walikuwa wamesimama: Mariamu mama yake, shan gazi yake, Mariamu mke wa Klopa na Mariamu Magdalena.26 Yesu alipomwona mama yake na yule mwanafunzi aliyempenda wamesimama karibu, alimwambia mama yake, “Mama, huyo ni mwanao!”27 Kisha akamwambia yule mwanafunzi, “Na huyo ni mama yako.” Tangu wakati huo yule mwanafunzi akamchukua mama yake Yesu nyumbani kwake.
28 Baada ya haya Yesu alifahamu ya kuwa mambo yote yameka milika, kwa hiyo, ili kutimiza Maandiko, akasema, “Naona kiu.” 29 Hapo palikuwa na bakuli lililojaa siki. Kwa hiyo wakachukua sponji iliyolowanishwa kwenye hiyo siki wakaichomeka kwenye ufito wa hisopo wakampandishia mdomoni.30 Baada ya kuipokea hiyo siki, Yesu akasema, “Imekwisha.” Akainamisha kichwa, akakata roho.
31 Kwa kuwa ilikuwa siku ya Maandalizi ya Pasaka Wayahudi hawakutaka miili yao ibaki msalabani siku ya sabato. Hii ingekuwa sabato ya pekee kwa kuwa iliangukia wakati wa Pasaka. Wakamwomba Pilato aamuru miguu ya wale waliosulubiwa ivunjwe ili wafe upesi waondolewe msalabani. 32 Kwa hiyo askari wakaenda wakavunja miguu ya mtu wa kwanza aliyesulubiwa na Yesu na wa pili pia. 34 Ila askari mmoja akamchoma mkuki ubavuni, na mara pakatoka damu na maji. 35 Mambo haya yamehakikishwa na mtu aliyeyaona, na ushahidi wake ni wa kuaminika. Yeye anajua ya kuwa aliyosema ni kweli, naye ametoa ushuhuda huu ili nanyi mpate kuamini. 36 Kwa maana mambo haya yalitokea ili kutimiza Maandiko yaliyosema, “Hakuna hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa.” 37 Na pia Maandiko mengine yanasema, “Watamtazama yeye waliyemchoma kwa mkuki.” 38 Baada ya haya, Yusufu wa Arimathea aliyekuwa mfuasi wa siri wa Yesu, maana aliwaogopa Wayahudi, akamwomba Pilato auchukue mwili wa Yesu; naye akamruhusu. Kwa hiyo akaja, akauchukua mwili wa Yesu. 39 Naye Nikodemo, yule ambaye alimwen dea Yesu kwa siri usiku, alikuja na mchanganyiko wa manukato zaidi ya kilo thelathini. 40 Wakauchukua mwili wa Yesu, wakau vika sanda iliyokuwa na manukato, kama ilivyokuwa desturi ya Way ahudi. 41 Karibu na pale walipomsulubisha palikuwa na bustani yenye kaburi ambalo lilikuwa halijatumika. 42 Kwa hiyo ili kuka milisha mazis
Jumapili asubuhi na mapema, kukiwa bado giza, Mariamu Mag dalena alifika kaburini akakuta lile jiwe lililokuwa limeziba mlango wa kaburi limeondolewa. 2 Kwa hiyo akaenda mbio kwa Simoni Petro na yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akawaambia, “Wameu chukua mwili wa Bwana kutoka mle kaburini na hatujui wameuweka wapi!” 3 Petro na yule mwanafunzi wakaondoka mara kuelekea kabu rini. 4 Wote wawili walikuwa wanakimbia lakini yule mwanafunzi akakimbia mbio zaidi kuliko Petro, akawahi kufika kaburini. 5 Alipofika akainama na kuchungulia mle kaburini akaona ile sanda, lakini hakuingia ndani. 6 Ndipo Petro akaja akimfuata nyuma akaenda moja kwa moja hadi ndani ya kaburi. Naye akaona ile sanda 7 na kile kitambaa kilichokuwa kichwani mwa Yesu kimekunjwa na kuwekwa kando ya ile sanda. 8 Kisha yule mwanafunzi aliyewahi kufika kaburini naye akaingia ndani; akaona, akaamini. 9 Kwa maana mpaka wakati huo walikuwa bado hawajaelewa yale Maandiko yaliyotabiri kuwa angefufuka kutoka kwa wafu. 10 Wale wanafunzi wakaondoka wakarudi nyumbani kwao.
11 Lakini Mariamu akakaa nje ya kaburi akilia. Na alipokuwa akilia akainama kutazama mle kaburini. 12 Akaona malaika wawili wamevaa nguo nyeupe, wamekaa pale mwili wa Yesu ulipokuwa, mmoja upande wa miguuni na mwingine upande wa kichwani! 13 Wakamwuliza Mariamu, “Mama, mbona unalia?” Akawaambia, “Nalia kwa kuwa wamemchukua Bwana wangu na sijui wamemweka wapi.” 14 Alipokuwa akisema haya akageuka, akamwona Yesu amesimama nyuma yake, lakini hakumtambua! 15 Yesu akamwambia, “Mama, mbona unalia? Unamta futa nani?” Mariamu alidhani aliyekuwa anaongea naye ni mtunza bustani, kwa hiyo akajibu, “Kama ni wewe umemchukua tafadhali nionyeshe ulipomweka ili nimchukue.” 16 Yesu akamwita, “Mar iamu.” Ndipo Mariamu akamgeukia Yesu, akamwambia kwa Kiebrania, “Rabboni!’ 17 Yesu akamwambia, “Usin ishike kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ninakwenda kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu.” 18 Kwa hiyo Mariamu Magdalena akaenda akawakuta wanafunzi akawaambia, “Nimemwona Bwana!”
19 Jumapili hiyo jioni, wakati wanafunzi walikuwa pamoja huku milango ikiwa imefungwa kwa kuwaogopa Wayahudi, Yesu aliwato kea! Akasimama kati yao akasema, “Amani iwe nanyi.” 20 Baada ya kusema haya, aliwaonyesha mikono yake na ubavu wake. Wanafunzi walifurahi sana walipomwona Bwana! 21 Yesu akawaambia tena, “Amani iwe nanyi. Kama Baba alivyonituma, mimi pia nawatuma ninyi.”
22 Na alipokwisha kusema haya akawavuvia pumzi yake akawaambia, “Pokeeni Roho Mtakatifu.23 Mkimsamehe mtu ye yote dhambi zake, atakuwa amesamehewa. Msipomsamehe, atakuwa hajasame hewa.”
24 Tomaso, aliyeitwa Pacha, hakuwepo wakati Yesu aliwatokea wanafunzi wenzake. 25 Kwa hiyo wakamwambia, “Tumemwona Bwana.” Lakini yeye akawaambia, “Sitaamini mpaka nione alama za misumari katika mikono yake na niguse kwa vidole vyangu makovu ya misumari na kuweka mkono wangu ubavuni mwake.”
26 Siku nane baada ya haya, wanafunzi walikuwa pamoja tena katika chumba kimoja na Tomaso pia alikuwepo. Milango ilikuwa imefungwa, lakini Yesu akawatokea akasimama kati yao akawaambia, “Amani iwe nanyi.”27 Ndipo akamwambia Tomaso, “Weka kidole chako hapa; tazama mikono yangu halafu nyoosha mkono wako uguse ubavu wangu. Usiwe na mashaka bali uamini.” 28 Tomaso akasema, “Bwana wangu na Mungu wangu!” 29 Yesu akamwambia, “Umeamini kwa kuwa umeniona? Wamebarikiwa wale ambao hawajaona lakini wameamini.”
30 Yesu alifanya ishara nyingine nyingi mbele za wanafunzi wake ambazo hazikuandikwa katika kitabu hiki. 31 Lakini hizi zimeandikwa ili muweze kuamini ya kuwa Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake.

Baada ya haya Yesu alijitambulisha tena kwa wanafunzi wake kando ya bahari ya Tiberia. Ilitokea hivi: 2 Simoni Petro, Tomaso aitwaye Pacha, Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi wengine wawili walikuwa pamoja. 3 Simoni Petro aka waambia wenzake, “Mimi nakwenda kuvua samaki.” Nao wakamwambia, “Tutakwenda pamoja nawe.” Wakatoka, wakaingia ndani ya mashua. Lakini usiku ule hawakupata cho chote. 4 Kulipopambazuka, Yesu alisimama ufukoni, lakini wale wana funzi hawakumtambua. 5 Yesu akawaambia, “Wanangu, mmepata samaki wo wote?” Wakamjibu, “La.” 6 Akawaambia, “Shusheni wavu upande wa kulia wa mashua yenu nanyi mtapata samaki.” Walivyofa nya hivyo walipata samaki wengi mno hata wakashindwa kuingiza ule wavu uliojaa samaki katika mashua! 7 Kisha yule mwanafunzi ali yependwa na Yesu akamwambia Petro, “Ni Bwana!” Petro aliposikia haya akajifunga nguo yake, kwa kuwa alikuwa amevua wakati wakifa nya kazi, akajitosa baharini, akaogelea kuelekea ufukoni. 8 Wale wanafunzi wengine wakaja kwa ile mashua huku wakivuta ule wavu uliojaa samaki. Hapo walipokuwa wakivua hapakuwa mbali na nchi kavu; ilikuwa kama hatua mia moja hivi.
9 Walipowasili nchi kavu, wakaona moto wa mkaa na samaki wakiokwa juu yake, na mikate. 10 Yesu akawaambia, “Leteni baadhi ya samaki mliovua.”11 Simoni Petro akaenda akauvuta ule wavu ambao ulikuwa umejaa samaki wakubwa mia moja hamsini na tatu, akauleta ufukoni. Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika. 12 Yesu akawaambia, “Njooni mle.” Hakuna hata mmoja wao aliyethubutu kumwuliza, “Wewe ni nani?” Walijua hakika ya kuwa ni Bwana. 13 Yesu akaenda akachu kua ile mikate na baadaye samaki, akawagawia. 14 Hii ilikuwa ni mara ya tatu Yesu kujitambulisha kwa wanafunzi wake tangu afufuke kutoka kwa wafu.
15 Walipokwisha kula, Yesu akamwuliza Simoni Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?” Yeye akamjibu, “Ndio Bwana, wewe unajua ya kuwa nakupenda.” Yesu akamwambia, “Lisha wana kondoo wangu.” 16 Kwa mara nyingine Yesu akamwul iza Simoni Petro, “Simoni, mwana wa Yohana, unanipenda?” Petro akajibu, “Ndio Bwana, wewe unajua ya kuwa nakupenda.” Akamwam bia, “Chunga kondoo wangu.” 17 Kwa mara ya tatu Yesu akamwul iza Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda?” Petro akahuzu nika sana kwa kuwa Yesu alimwuliza mara ya tatu, ‘Unanipenda?’ Akamjibu, “Bwana, wewe unajua kila kitu. Unajua ya kuwa naku penda.” Yesu akamwambia, “Lisha kondoo wangu. 18 Nakuambia wazi, ulipokuwa kijana ulivaa na kwenda unakotaka; lakini ukiwa mzee utanyoosha mikono yako na mtu mwingine atakuvika nguo na kukupeleka usipotaka kwenda.” 19 Alisema haya ili kumfahamisha Petro jinsi atakavyokufa, na kwa kifo hicho Mungu atukuzwe. Kisha Yesu akamwambia Petro, “Nifuate.” 20 Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akiwafuata. Huyu mwanafunzi ndiye yule aliyekaa karibu kabisa na Yesu alipokula naye chakula cha mwisho akauliza, ‘Bwana, ni nani atakayekusaliti?’ 21 Petro alipomwona huyo mwanafunzi akamwuliza Yesu, “Bwana, na huyu je?” 22 Yesu akamjibu, “ Ikiwa nataka aishi mpaka nitakapo rudi, inakuhusu nini? Wewe nifuate!” 23 Kwa sababu ya maneno haya ya Yesu, uvumi ukaenea kati ya ndugu kwamba huyu mwanafunzi hangekufa. Lakini Yesu hakusema kuwa hangekufa. Yeye alisema tu kwamba, “Ikiwa nataka aishi mpaka nitakaporudi, inakuhusu nini?”
24 Huyu ndiye yule mwanafunzi ambaye anashuhudia mambo haya na ndiye ambaye ameandika habari hizi. Nasi tunajua ya kuwa ushu huda wake ni wa kweli.

Luka 23:26-24:52
26 Na walipokuwa wakienda naye, wakamkamata mtu mmoja ait waye Simoni wa Kirene aliyekuwa anatoka mashambani. Wakambebesha msalaba, wakamlazimisha atembee nyuma ya Yesu.
27 Umati mkubwa wa watu wakamfuata Yesu ikiwa ni pamoja na wanawake waliokuwa wakimlilia na kuomboleza. 28 Lakini Yesu akawageukia, akawaam bia, “Enyi akina mama wa Yerusalemu, msinililie mimi bali jilil ieni ninyi wenyewe na watoto wenu.
29 Kwa maana wakati utafika ambapo mtasema, ‘Wamebarikiwa akina mama tasa, ambao hawakuzaa na matiti yao hayakunyonyesha.’ 30 Na watu wataiambia milima, ‘Tuangukieni’ na vilima, ‘Tufunikeni’. 31 Kwa maana kama watu wanafanya mambo haya wakati mti ni mbichi, itakuwaje utakapo kauka?”
32 Wahalifu wengine wawili pia walipelekwa wakasulubiwe pamoja na Yesu.33 Walipofika mahali paitwapo “Fuvu la kichwa,” wakamsulubisha Yesu hapo pamoja na hao wahalifu; mmoja upande wa kulia na mwingine upande wa kushoto.
34 Yesu akasema, “Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui wali tendalo!” Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura. 35 Watu wakasi mama pale wakimwangalia. Viongozi wa Wayahudi wakamdhihaki wakisema, “Si aliokoa wengine! Ajiokoe mwenyewe basi, kama kweli yeye ndiye Kristo wa Mungu, Mteule wake.” 36 Askari nao wakam wendea, wakamdhihaki. Wakamletea siki anywe, 37 wakamwambia, “Kama wewe ni mfalme wa Wayahudi, jiokoe tuone.”
38 Na maandishi haya yaliwekwa kwenye msalaba juu ya kichwa chake: “HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI.” 39 Mmoja kati ya wale wahalifu waliosulubiwa naye akamtu kana, akasema: “Wewe si ndiye Kristo? Jiokoe na utuokoe na sisi.”
40 Yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake, akisema, “Wewe humwogopi hata Mungu! Wote tumehukumiwa adhabu sawa. 41 Adhabu yetu ni ya haki kwa sababu tunaadhibiwa kwa makosa tuliyofanya. Lakini huyu hakufanya kosa lo lote.” 42 Kisha akasema, “Bwana Yesu unikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.” 43 Yesu akam jibu, “Nakuambia kweli, leo hii utakuwa pamoja nami peponi.”
44 Ilikuwa kama saa sita mchana. Kukawa na giza nchi nzima mpaka saa tisa, 45 kwa maana jua liliacha kutoa nuru. Pazia la Hekalu likapasuka katikati kukawa na vipande viwili. 46 Yesu akapaza sauti akasema, “Baba, mikononi mwako ninaikabidhi roho yangu.” Baada ya kusema haya, akakata roho.
47 Mkuu wa maaskari alipoona yaliyotokea, akamsifu Mungu akasema, “Hakika, mtu huyu alikuwa mwenye haki.” 48 Na watu wote waliokuwa wamekusanyika hapo kushuhudia tukio hilo walipoy aona hayo, walirudi makwao wakijipiga vifua kwa huzuni.
49 Lakini wale wote waliomfahamu, pamoja na wanawake wal iokuwa wamemfuata kutoka Galilaya, walisimama kwa mbali wakiyata zama mambo haya. Yesu Azikwa Kaburini
50 Kulikuwa na mtu mmoja jina lake Yusufu mwenyeji wa mji wa Arimathaya, ambaye alikuwa anautazamia Ufalme wa Mungu. Yeye ali kuwa mjumbe wa Baraza na pia alikuwa mtu mwema na mwenye kuheshi mika.51 Lakini yeye hakukubaliana na wajumbe wenzake katika uamuzi wao na kitendo cha kumsulubisha Yesu. 52 Basi, Yusufu alikwenda kwa Pilato akaomba apewe mwili wa Yesu. 53 Akaushusha kutoka msalabani, akauzungushia sanda, akauhifadhi katika kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kaburi hilo lilikuwa halijatumika bado. 54 Siku hiyo ilikuwa Ijumaa, Siku ya Maandalizi, na sabato ilikuwa karibu ianze. 55 Wale wanawake waliokuwa wamefuatana na Yesu kutoka Galilaya wakamfuata Yusufu, wakaliona kaburi na jinsi mwili wa Yesu ulivyolazwa humo. 56 Kisha wakarudi nyumbani wakaandaa marashi na manukato ya kuupaka huo mwili. Lakini waka pumzika siku ya sabato kama ilivyoamriwa.

Siku ya Jumapili, alfajiri na mapema, wale wanawake wali chukua yale manukato waliyokuwa wameyaandaa wakaenda kaburini. 2 Wakakuta jiwe limeondolewa kwenye mlango wa kaburi. 3 Lakini walipoingia ndani, hawakuona mwili wa Bwana Yesu. 4 Walipokuwa wanashangaa juu ya jambo hilo, ghafla, watu wawili waliokuwa wamevaa mavazi yanayong’aa sana, wakasimama karibu nao. 5 Wale wanawake, kwa hofu, wakainamisha nyuso zao chini. Lakini wale watu wakawaambia, “Kwa nini mnamtafuta aliye hai mahali pa wafu? 6 Hayuko hapa; amefufuka. Kumbukeni alivyowaambia alipokuwa Gali laya, 7 kwamba ilikuwa lazima Mwana wa Adamu awekwe mikononi mwa watu waovu, asulubiwe na siku ya tatu afufuke.”8 Wakayakumbuka maneno ya Yesu. 9 Waliporudi kutoka huko kaburini wakaeleza mambo haya kwa wale wanafunzi kumi na mmoja pamoja na wengine wote. 10 Hao wanawake walikuwa ni Mariamu Magdalene, Yoana na Mariamu mama yake Yakobo pamoja na wengine waliofuatana nao.11 Maelezo yao yalionekana kama upuuzi kwa hiyo hawakuwaamini. 12 Bali Petro akaondoka mbio, akaenda kaburini. Alipoinama, akaiona ile sanda, ila hakuona kitu kingine zaidi. Akarudi nyumbani akis taajabia yaliyotokea.
13 Siku hiyo hiyo, wanafunzi wawili wa Yesu walikuwa wanak wenda kijiji cha Emau, yapata maili saba kutoka Yerusalemu, 14 nao walikuwa wakizungumzia mambo yote yaliyotokea. 15 Wali pokuwa wakizungumza, Yesu mwenyewe alikuja akatembea pamoja nao, 16 lakini wao hawakumtambua. 17 Akawauliza, “Ni mambo gani haya mnayozungumzia wakati mnatembea?” Wakasimama , nyuso zao zikionyesha huzuni.18 Mmoja wao, aliyeitwa Kleopa, akamwambia, “Nadhani ni wewe tu katika watu wote wanaoishi Yerusalemu ambaye hufahamu mambo yaliyotokea siku hizi chache zilizopita.”
19 Akawauliza, “Mambo gani?” Wakamjibu “Mambo yaliyompata Yesu Mnazareti. Yeye alikuwa nabii mwenye uwezo mkuu katika maneno yake na matendo yake, mbele za Mungu na mbele za wanadamu. 20 Makuhani wakuu na viongozi wetu walimtoa ahukumiwe kufa na wakamsulubisha.
21 Na sisi tulikuwa tumetegemea kwamba yeye ndiye angeliikomboa Israeli. Zaidi ya hayo leo ni siku ya tatu tangu mambo haya yatokee. 22 Isitoshe, baadhi ya wanawake katika kundi letu wametushtua; walikwenda kaburini leo alfajiri23 lakini hawakuukuta mwili wake. Waliporudi walisema wamewaona malaika ambao waliwaambia kwamba Yesu yu hai. 24 Baadhi yetu walikwenda kaburini wakakuta mambo ni kama walivyoelezea wale wanawake, ila yeye mwenyewe hawakumwona.”
25 Kisha Yesu akawaambia, “Ninyi ni watu wajinga. Mbona mnaona ugumu kuamini mambo yote yaliyosemwa na Manabii? 26 Je, haikumpasa Kristo kuteswa na kwa njia hiyo aingie katika utukufu wake?” 27 Akawafafanulia maandiko yalivyosema kumhusu yeye, akianzia na maandiko ya Musa na kupitia maandiko yote ya manabii.
28 Walipokaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, Yesu akawa kama anaendelea na safari. 29 Lakini wakamsihi akae nao wakisema, “Kaa hapa nasi kwa maana sasa ni jioni na usiku unain gia.” Basi akaingia ndani kukaa nao. 30 Alipokuwa nao mezani, akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akaanza kuwagawia. 31 Ndipo macho yao yakafumbuliwa, wakamtambua! Lakini akatoweka, hawakumwona tena.
32 Wakaulizana, “Je, mioyo yetu haikuchangamka kwa furaha alipokuwa anazungumza nasi njiani na kutufafanulia Maandiko?” 33 Wakaondoka mara moja, wakarudi Yerusalemu. Wakawakuta wale wanafunzi kumi na mmoja na wale waliokuwa pamoja nao, wamekusany ika 34 wakisema, “Ni kweli Bwana amefufuka! Amemtokea Simoni.” 35 Kisha wale wanafunzi wawili wakaeleza yaliyotokea njiani na jinsi walivyomtambua Yesu alipoumega mkate. Yesu Awatokea Wanafunzi Wake
36 Wakati walipokuwa wanazungumza hayo, Yesu mwenyewe akasi mama katikati yao akawasalimu, “Amani iwe nanyi.”
37 Wakashtuka na kuogopa wakidhani wameona mzimu. 38 Lakini akawauliza, “Kwa nini mnaogopa? Kwa nini mna mashaka mioyoni mwenu?39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu mwone kuwa ni mimi. Niguseni mwone. Mzimu hana nyama na mifupa kama mnion avyo.” 40 Aliposema haya aliwaonyesha mikono yake na miguu yake. 41 Wakashindwa kuamini kwa ajili ya furaha na mshangao waliokuwa nao. Akawauliza, “Mna chakula cho chote hapa?” 42 Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa,43 akakichukua akakila mbele yao.
44 Akawaambia, “Haya ndiyo mambo niliyowaambia nilipokuwa pamoja nanyi; kwamba yote yaliyoandikwa kunihusu mimi katika she ria ya Musa, katika Maandiko ya manabii na Zaburi hayana budi kutimizwa.” 45 Akawapa uwezo wa kuyaelewa Maandiko, 46 aka waambia, “Haya ndiyo yaliyoandikwa: Kristo atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka kwa wafu. 47 Habari hii ya wokovu itatan gazwa kwanza Yerusalemu hadi kwa mataifa yote, kwamba: kuna msa maha wa dhambi kwa wote watakaotubu na kunigeukia mimi.48 Ninyi ni mashahidi wa mambo haya. 49 Na sasa nitawapelekea Roho Mtaka tifu kama alivyoahidi Baba yangu; lakini kaeni humu Yerusalemu mpaka mtakapopewa nguvu ya Roho Mtakatifu kutoka mbinguni.”
50 Kisha akawaongoza nje ya mji mpaka Bethania, akainua mikono yake, akawabariki. 51 Alipokuwa anawabariki, akawaacha; akachukuliwa mbinguni.52 Wakamwabudu na kisha wakarudi Yerus alemu wamejawa na furaha;

Matendo Ya Mitume1: 1-11
Mpendwa Teofilo, Katika Kitabu changu cha kwanza nilikuan dikia kuhusu mambo yote aliyotenda Yesu, 2 hadi wakati alipopaa mbinguni. Kabla hajachukuliwa juu, aliwapa mitume wake maagizo kwa njia ya Roho Mtakatifu. 3 Alijionyesha kwao akiwa hai muda wa siku arobaini baada ya kufufuka kwake. Akawahakikishia kwa njia nyingi ya kuwa ni yeye na akaongea nao kuhusu Ufalme wa Mungu.
4 Wakati mmoja alipokuwa nao, aliwapa amri hii, “Msiondoke Yerusalemu, mpaka mtakapopokea ahadi aliyotoa Baba, ambayo mmeni sikia nikiizungumzia. 5 Kwa maana Yohana aliwabatiza kwa maji lakini baada ya siku chache mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”
6 Mitume walipokutana na Yesu walimwuliza, “Bwana, wakati huu ndipo utawarudishia Waisraeli ufalme ?”
7 Yesu akawaambia, “Si juu yenu kufahamu wakati na majira ambayo yamewekwa na Baba kwa mamlaka yake. 8 Lakini mtapokea nguvu akishawajilia Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu na Yudea yote na Samaria, hadi mwisho wa dunia.”
9 Baada ya kusema haya, wakiwa wanatazama, alichukuliwa juu, na wingu likamficha wasimwone tena. 10 Walikuwa bado wakikaza macho yao mawinguni alipokuwa akienda, ndipo ghafla, wanaume wawili waliovaa mavazi meupe walisimama karibu nao, 11 wakasema, “Ninyi watu wa Galilaya, mbona mnasimama hapa mkitazama mbin guni? Yesu huyu huyu aliyechukuliwa mbinguni atarudi tena kama mlivyomwona akienda mbinguni.”

2 Wakorintho 5: 21
21 Mungu alimfanya yeye ambaye hakujua dhambi, awe dhambi kwa ajili yetu ili ndani yake tupate kuwa haki ya Mungu.

1 Yohana 3: 8-10
8 Kila atendaye dhambi ni wa shetani; kwa maana shetani ametenda dhambi tangu mwanzo. Mwana wa Mungu alikuja ili aziangamize kazi za shetani.
9 Mtu aliyezaliwa na Mungu haendelei na tabia ya kutenda dhambi, kwa maana ana asili ya Mungu; hawezi kuendelea kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mungu.
10 Na hivi ndivyo tunavyoweza kutambua wazi kati ya walio watoto wa Mungu na walio watoto wa shetani. Mtu ye yote asiyet enda lililo haki si wa Mungu; wala asiyempenda ndugu yake si wa Mungu.

Waefeso 1: 18-22
18 Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yaangaziwe ili mpate kujua tumaini mliloitiwa, na mtambue utajiri wa urithi wa utukufu wake kwa watu wa Mungu; 19 na muu fahamu uweza wake usiopimika ambao ametupa sisi tunaoamini. Uweza huo ni sawa na ile nguvu kuu 20 ambayo aliitumia alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, akamweka akae mkono wake wa kulia katika enzi yake mbinguni. 21 Hapo alipo ni juu sana, kupita tawala na mamlaka zote na nguvu zote na milki, na kupita cheo cho chote kinachoweza kutolewa, si tu katika nyakati hizi, bali pia katika nyakati zijazo. 22 Na Mungu ameweka vitu vyote viwe chini ya mamlaka yake na akamteuwa awe mkuu wa vitu vyote kwa ajili ya kanisa.

Ufunua wa Yohana 20:1-3, 7-10
Kisha nikaona malaika akija kutoka mbinguni akiwa ameshika ufunguo wa lile shimo la kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi. 2 Akalishika lile joka, yule nyoka wa kale ambaye ni Ibilisi au Shetani, akamfunga kwa muda wa miaka elfu moja. 3 Akamtupa kuzi muni; akamfungia huko na kumzibia kabisa, asipate nafasi ya kudanganya mataifa tena mpaka hiyo miaka elfu moja iishe. Baada ya hapo ataachiliwa kwa muda mfupi.
7 Miaka hiyo elfu moja itakapokwisha, shetani atafunguliwa kutoka kifungoni mwake, 8 naye atakuja kuyadanganya mataifa yali yopo katika pembe nne za dunia, yaani, Gog na Magog na kuwakusa nya tayari kwa vita. Idadi yao ni kama mchanga wa bahari. 9 Nao walitembea juu ya eneo lote la dunia, wakaizunguka kambi ya wata katifu na ule mji mwema, lakini moto ulishuka kutoka mbinguni, ukawateketeza. 10 Na yule Ibilisi aliyewadanganya alitupwa katika ziwa la moto na kiberiti walipokuwa yule mnyama na yule nabii wa uwongo. Nao watateseka huko usiku na mchana, milele na milele.

7. Matendo 4:12
12 Wokovu unapatikana kwake tu; kwa maana hakuna jina jingine duniani ambalo wamepewa wanadamu kuwaokoa ila jina la Yesu, na ni kwa jina hilo peke yake tunaweza kuokolewa!”

 

 
 

The Guide has her own Guidebook to help her lead and guide the lesson.

Swahili Lesson #4 Guidebook (to be translated)

Download Swahili Guidebook Bible Verses Swahili Lesson #4

Mistari ya Biblia

 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us