Project Hope     home >> stonecroft>>roho mtakatifu yuko wapi?>>somo la kwanza 1>> mistari ya biblia
Roho Mtakatifu yuko wapi? - Somo la kwanza #1 - Mistari ya Biblia
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

Somo la 1

Kutambua uwepio wa Roho Mtakatifu

Kitabu mwongozo

Mistari ya Biblia

1. Yohana 14:26
26 Lakini yule Msaidizi, yaani Roho Mtakatifu, ambaye Baba yangu atamtuma kwenu kwa jina langu, atawafundisha mambo yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

Yohana 4: 24
24 Mungu ni roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”

2. Yohana 15:26
26 Lakini atakapokuja yule Msaidizi nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, yaani yule Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia mimi.

Matendo 13:2
2 Umati mkubwa mno wa watu wakasongamana hata ikabidi aingie katika mashua akaketi humo; na wale watu wakakaa ukingoni mwa bahari.

Warumi 8:14
14 Kwa maana wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu ni wana wa Mungu.

Warumi 8:26
26 Hali kadhalika Roho hutusaidia katika udhaifu wetu. Kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu usioelezeka kwa maneno.

3. 2 Wakorintho 1:21-22
21 Ni Mungu mwenyewe ambaye anatuwezesha sisi na ninyi kusimama imara katika Kristo. Ametuweka wakfu; 22 ametutia mhuri wake juu yetu, akatupa Roho wake mioyoni mwetu kama uthibitisho.

4. Yohana 16:7-11
7 Lakini nawaambia kweli kwamba kuondoka kwangu ni kwa faida yenu kwa maana nisipoondoka, yule Msaidizi hatakuja kwenu. Lakini nikienda nitamtuma aje kwenu. 8 Naye akija atauthibitishia ulim wengu kuhusu dhambi, haki na hukumu. 9 Kuhusu dhambi kwa sababu hawaniamini; 10 kuhusu haki kwa sababu ninakwenda kwa Baba na hamtaniona tena; 11 na kuhusu hukumu kwa sababu mtawala wa ulim wengu huu amekwisha kuhukumiwa.

Yuda 1: 14-16
14 Henoki, ambaye alikuwa wa kizazi cha saba baada ya Adamu, alitoa unabii kuhusu watu hawa akasema, “Sikilizeni! Nilimwona Bwana akija na watakatifu wake maelfu kwa maelfu 15 kutoa hukumu kwa wote na kuwaadhibu wasiomcha Mungu, kwa ajili ya matendo yao maovu waliyoyatenda na kwa ajili ya maneno makali ambayo hao waovu wasiomcha Mungu walisema juu yake.”

16 Watu hawa ni wanung’unikaji, wakaidi, wenye kufuata tamaa zao, wenye majivuno, wenye kujigamba na ambao huwasifu watu wen gine ili mambo yao yafanikiwe.

Warumi 6: 23
23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

5. Yohana 3:5-7
5 Yesu akamwambia, “Ninakuambia hakika, kama mtu hakuzaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia katika Ufalme wa Mungu. 6 Mtu huzaliwa kimwili na wazazi wake, lakini mtu huzaliwa kiroho na Roho wa Mungu. 7 Kwa hiyo usishangae ninapokuambia kwamba huna budi kuzaliwa mara ya pili.

Tito 3:4-7
4 Lakini wakati wema na upendo wa Mungu Mkombozi wetu ulipodhihirishwa, 5 ali tuokoa, si kwa sababu ya matendo mema ya haki tuliyotenda, bali kwa sababu ya huruma yake. Alituokoa kwa kuoshwa na kuzaliwa mara ya pili na kufanywa wapya kwa njia ya Roho Mtakatifu, 6 ambaye Mungu alitumiminia kwa wingi kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu. 7 Na tukishahesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele tunaoutumainia.

Yohana 3:16
16 “Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu kiasi cha kumtoa Mwanae pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

6. Ufunuo 22:17
17 Roho na bibi harusi wanasema, “Njoo!” Na kila mtu asi kiaye na aseme, “Njoo!” Na mtu ye yote mwenye kiu na aje, na kila anayetaka na apokee zawadi ya maji ya uzima bure.

Yohana 10:30
30 Mimi na Baba yangu tu mmoja.

7. I Wakorintho 2:11
11 Kwa maana ni nani anajua mawazo ya mtu isipo kuwa roho aliye ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo hakuna mtu anayeelewa mawazo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.

Waebrania 9:14
14 damu ya Kristo ambaye kwa njia ya Roho wa milele alijitoa mwenyewe kwa Mungu kama sadaka isiyokuwa na doa, itazisafisha dhamiri zetu zaidi sana kutokana na matendo yaletayo kifo, na kutuwezesha kumtumikia Mungu aliye hai.

Warumi 8:2, 10
2 Kwa maana sheria ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu imeniweka huru kutokana na sheria ya dhambi na mauti.

10 Lakini kama Kristo anaishi ndani yenu, ingawa miili yenu imekufa kwa sababu ya dhambi, roho zenu zinaishi kwa sababu mmek wisha kuhesabiwa haki.

 

 
 

The Guide has her own Guidebook to help her lead and guide the lesson.

Download Full Swahili Guidebook

Download Swahili Guidebook Introduction

Download Swahili Lesson #1 Guidebook

Download Swahili Guidebook Front and Back page of folder

Download Swahili Guidebook Bible Verses Lesson #1

Download Swahili Lesson #1 Student Study Book

Mistari ya Biblia

 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us