Project Hope     home >> stonecroft>>roho mtakatifu yuko wapi?>>somo la pili>> mistari ya biblia
Roho Mtakatifu yuko wapi? - Somo la Pili #2 - Mistari ya Biblia
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

Somo la 2

Roho mtakatifu ana kazi gani?

Kitabu mwongozo

Mistari ya Biblia

Kujisomea Biblia kwa Juma

Yohana 3:1-13
Kiongozi mmoja wa Wayahudi wa kundi la Mafarisayo aitwaye Nikodemo,2 alimjia Yesu usiku akamwambia, “Rabi, tunafahamu kuwa wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kufanya miujiza hii uifanyayo, kama Mungu hayupo pamoja naye.”

3 Yesu akamjibu, “Ninakwambia hakika, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona Ufalme wa Mungu.”

4 Nikodemo akasema, “Inawezekanaje mtu mzima azaliwe? Anaweza kuingia tena katika tumbo la mama yake na kuzaliwa mara ya pili?”

5 Yesu akamwambia, “Ninakuambia hakika, kama mtu hakuzaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia katika Ufalme wa Mungu. 6 Mtu huzaliwa kimwili na wazazi wake, lakini mtu huzaliwa kiroho na Roho wa Mungu. 7 Kwa hiyo usishangae ninapokuambia kwamba huna budi kuzaliwa mara ya pili.8 Upepo huvuma po pote upendapo. Mvumo wake unausikia lakini huwezi ukafahamu utokako wala uen dako. Ndivyo ilivyo kwa kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.” 9 Nikodemo akamwuliza, “Mambo haya yanawezekanaje?”10 Yesu akamwambia, “Wewe ni mwalimu mashuhuri wa Waisraeli na huyaelewi mambo haya? 11 Ninakwambia kweli, sisi tunazungumza lile tunalo lijua na tunawashuhudia lile tuliloliona, lakini hamtaki kutu amini! 12 Ikiwa hamuniamini ninapowaambia mambo ya duniani, mtaniaminije nitakapowaambia habari za mbinguni? 13 Hakuna mtu ye yote ambaye amewahi kwenda juu mbinguni isipokuwa mimi Mwana wa Adamu niliyeshuka kutoka mbinguni.

Yohana 3:14-21
14 Na kama Musa alivyomwi nua yule nyoka kule jangwani, vivyo hivyo mimi Mwana wa Adamu sina budi kuinuliwa juu15 ili kila mtu aniaminiye awe na uzima wa milele . 16 “Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu kiasi cha kumtoa Mwanae pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 17 Maana Mungu hakumtuma Mwanae kuuhukumu ulimwengu bali auokoe ulimwengu.18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakumwamini Mwana pekee wa Mungu. 19 Na hukumu yenyewe ni kwamba: Nuru imekuja ulimwenguni lakini watu wakapenda giza kuliko nuru kwa sababu matendo yao ni maovu.20 Kwa kuwa kila mtu atendaye maovu huchu kia nuru, wala hapendi kuja kwenye nuru ili matendo yake maovu yasifichuliwe. 21 Lakini kila mtu anayeishi maisha ya uaminifu huja kwenye nuru, kusudi iwe wazi kwamba matendo yake yanatokana na utii kwa Mungu.”

Matendo 1:1-11
Mpendwa Teofilo, Katika Kitabu changu cha kwanza nilikuan dikia kuhusu mambo yote aliyotenda Yesu, 2 hadi wakati alipopaa mbinguni. Kabla hajachukuliwa juu, aliwapa mitume wake maagizo kwa njia ya Roho Mtakatifu. 3 Alijionyesha kwao akiwa hai muda wa siku arobaini baada ya kufufuka kwake. Akawahakikishia kwa njia nyingi ya kuwa ni yeye na akaongea nao kuhusu Ufalme wa Mungu.

4 Wakati mmoja alipokuwa nao, aliwapa amri hii, “Msiondoke Yerusalemu, mpaka mtakapopokea ahadi aliyotoa Baba, ambayo mmeni sikia nikiizungumzia. 5 Kwa maana Yohana aliwabatiza kwa maji lakini baada ya siku chache mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”
6 Mitume walipokutana na Yesu walimwuliza, “Bwana, wakati huu ndipo utawarudishia Waisraeli ufalme ?”

7 Yesu akawaambia, “Si juu yenu kufahamu wakati na majira ambayo yamewekwa na Baba kwa mamlaka yake. 8 Lakini mtapokea nguvu akishawajilia Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu na Yudea yote na Samaria, hadi mwisho wa dunia.”
9 Baada ya kusema haya, wakiwa wanatazama, alichukuliwa juu, na wingu likamficha wasimwone tena. 10 Walikuwa bado wakikaza macho yao mawinguni alipokuwa akienda, ndipo ghafla, wanaume wawili waliovaa mavazi meupe walisimama karibu nao, 11 wakasema, “Ninyi watu wa Galilaya, mbona mnasimama hapa mkitazama mbin guni? Yesu huyu huyu aliyechukuliwa mbinguni atarudi tena kama mlivyomwona akienda mbinguni.”

Matendo 2:1-13
Ilipofika siku ya Pentekoste, waamini wote walikuwa wameku tana mahali pamoja. 2 Ghafla, sauti kama mvumo mkubwa wa upepo uliwashukia kutoka mbinguni, ukaijaza nyumba yote walimokuwa wamekaa.

3 Pakatokea kitu kama ndimi za moto ambao uligawanyika ukakaa juu ya kila mmoja wao.4 Wote walijazwa Roho Mtakatifu wakaamza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kusema.

5 Wakati huo walikuwepo Yerusalemu Wayahudi wanaomcha Mungu kutoka nchi zote za dunia.

6 Waliposikia kelele hizi, walikusany ika kwa wingi. Wote walishangaa kwa sababu waliwasikia waamini wakiongea lugha ya kila mmoja wao.

7 Wakastaajabu sana, wakasema, “Hawa wote wanaozungumza ni Wagalilaya. 8 Imekuwaje basi tunawasikia wakinena lugha ya kila mmoja wetu? 9 Hapa kuna Waparthi, Wamedi, Waelami, wakazi wa Mesopotamia, Yudea Kapadokia, Ponto na Asia, 10 Frigia, Pom filia, Misri na pande za Libya karibu na Kirene; na wageni kutoka Rumi, Wayahudi na watu walioingia dini ya Kiyahudi. 11 Watu wen gine wametoka Krete na Uarabuni. Sisi sote tunasikia watu hawa wakisema katika lugha zetu wenyewe mambo makuu ya ajabu aliyofa nya Mungu.” 12 Wakiwa wameshangaa wakaulizana, “Ni nini maana ya mambo haya?” 13 Lakini wengine waliwadhihaki wakasema, “Hawa wamelewa divai mpya!”

Matendo 2:14-21
14 Ndipo Petro akasimama na wale mitume kumi na mmoja, aka hutubia ule umati wa watu kwa sauti kuu akasema, “Wayahudi wen zangu na ninyi nyote mkaao Yerusalemu. Nisikilizeni kwa makini niwaambie jambo hili maana yake ni nini! 15 Hawa watu hawakulewa kama mnavyodhania, kwa maana sasa ni mapema mno, saa tatu asu buhi. 16 La, jambo hili lilitabiriwa na Nabii Yoeli aliposema, 17 ‘Mungu alisema, siku za mwisho nitawamiminia binadamu wote Roho yangu: wavulana wenu na binti zenu watatabiri, vijana wenu wataona maono na wazee wataota ndoto. 18 Ndio, hata watumishi wangu wa kiume na wa kike nitawamiminia Roho yangu, nao watata biri. 19 Nami nitafanya maajabu angani, na duniani nitaonyesha ishara, damu na moto na moshi mnene. 20 Jua litageuka kuwa giza na mwezi utakuwa mwekundu kama damu, kabla ya siku ya Bwana kuwa dia, siku ambayo itakuwa ya kutisha. 21 Lakini ye yote ata kayetubu na kukiri jina la Bwana, ataokoka.’

Matendo 2:36-42
36 “Basi nataka niwahakikishie Waisraeli wote ya kuwa, Mungu amemfanya huyu Yesu ambaye ninyi mlimsulubisha, kuwa ndiye
37 Watu waliposikia maneno haya yaliwachoma moyoni, wakawau liza Petro na wale mitume wengine, “Tufanye nini ndugu zetu?”

38 Petro aliwajibu, “Tubuni, muache dhambi na kila mmoja wenu abatizwe katika jina la Yesu Kristo, ili msamehewe dhambi zenu; nanyi mtapokea zawadi ya Roho Mtakatifu. 39 Kwa maana ahadi hii ilitolewa na Mungu kwa ajili yenu na watoto wenu, na wale wote walio nchi za mbali, na kila mtu ambaye Bwana Mungu wetu anamwita kwake.”

40 Petro aliwasihi kwa maneno mengine mengi na kuwaonya akisema, “Jiepusheni na kizazi hiki kiovu.” 41 Wote waliopokea ujumbe wa Petro walibatizwa na zaidi ya watu elfu tatu wal iongezeka katika kundi la waamini siku hiyo.

42 Waamini hawa walitumia muda wao wakifundishwa na mitume, wakiishi pamoja katika ushirika, wakila pamoja na kusali. 43 Watu wote wakajawa na hofu kwa maana miujiza mingi na maajabu yalifanywa na mitume.

Warumi 8:16
16 Ni Roho mwenyewe anayeshuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi ni wana wa Mungu.

1. Mwanzo 1:2
Nayo nchi ilikuwa ukiwa nayo tupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, Roho wa Mungu akatulia juu ya uso wa maji

Isaya 40:12-14
Ni nani aliye yapima maji kwa konzi ya mkono wake? Na kuzikadiri mbingu kwa shubiri? Na kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi,na kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani, ni nani aliye mwongoza Roho wa Bwana na kumfundisha kwa kuwa mshauri wake? Alifanya shauri na nani ni nani aliye mwelimisha na kumfunza njia ya hukumu na kumfunza maarifa.

2. a. Ayubu 33:4
Roho wa Mungu ameniumba, na Pumzi ya mwenyezi hunipa uhai.

b. Ezekiel 36:27
Nami nitatia Roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu na kuzitenda.

c. Mika 3:8
Bali mimi hakika nimejaa nguvu kwa Roho ya Bwana, nimejaa hukumu na uwezo nimhukumu yakobo kosa lake, na Izraeli dhambi zake.

d. 2 Samweli 23:2
Roho wa Bwana alinena ndani yangu na neno lake likawa ulimini mwangu.

Isaya 11:2
Roho wa Bwana atakaa juu yake, Roho wa hekima na ufahamu, Roho wa ushauri na uweza, Roho wa maarifa na kumcha Bwana.

Kutoka 31:3
Nami nimemjaza Roho wa Mungu katika hekima na maarifa na ujuzi na mambo ya kazi ya kila aina.

Zaburi 51:11
Usinitenge na uso wako,
Wala Roho wako Mtakatifu usiniondolee.
Roho Mtakatifu katika agano jipya

Roho Mtakatifu katika agano jipya

Yohana 14:16
16 Nami nitam womba Baba, naye atawapeni Msaidizi mwingine akae nanyi siku zote

Luka 4:16-19
16 Baadaye Yesu akaenda Nazareti, mahali alipokulia. Siku ya sabato alikwenda katika sinagogi kama kawaida yake. Akasimama ili asome Maandiko. 17 Akapewa kitabu cha nabii Isaya, akakifun gua mahali palipoandikwa: 18-19 “Roho wa Bwana yu juu yangu. Amenichagua kuwahubiria maskini Habari Njema. Amenituma kuwatan gazia wafungwa kuwa wako huru, kuwaambia vipofu kuwa wanaweza kuona tena; na kuwaweka huru wanaoonewa, na nitangaze mwaka ambao Bwana atawabariki watu wake.”

Luka 4:1-2a
Kisha Yesu, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akarudi kutoka Yordani akaongozwa hadi jangwani. Alikaa huko jangwani siku arobaini 2 akijaribiwa na shetani.

Warumi 8:11
11 Na ikiwa Roho wa Mungu ambaye alimfu fua Yesu kutoka kwa wafu anaishi ndani yenu, Mungu aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataipatia uzima miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya huyo Roho wake ambaye anaishi ndani yenu.

Matendo 1:1-2
Mpendwa Teofilo, Katika Kitabu changu cha kwanza nilikuan dikia kuhusu mambo yote aliyotenda Yesu, 2 hadi wakati alipopaa mbinguni. Kabla hajachukuliwa juu, aliwapa mitume wake maagizo kwa njia ya Roho Mtakatifu.

Mathayo 1:18-20
18 Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi: Maria mama yake, alikuwa ameposwa na Yosefu. Lakini kabla ya ndoa yao, Mar ia akiwa bado bikira, alipata mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 19 Kwa kuwa Yosefu alikuwa mtu mwema hakutaka kumwaibisha mchumba wake Maria hadharani. Kwa hiyo aliamua kuvunja uchumba wao kwa siri. 20 Lakini alipokuwa bado anawaza juu ya jambo hili, malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto akasema, “Yosefu mwana wa Daudi, usisite kumwoa Maria mchumba wako kwa maana mimba aliyo nayo ameipata kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

4. 2 Petro 1:21
21 Kwa sababu hakuna unabii uliokuja kwa matakwa ya binadamu, bali watu walinena ujumbe kutoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

1 Wakorintho 2: 13
13 Haya ndio tunayozungumzia, lakini si kwa maneno tuliyofundishwa na hekima ya wanadamu bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, nasi tunafa fanua mambo ya kiroho kwa watu wa kiroho.

Roho Mtakatifu katika maisha yetu

5. Wagalatia 3:27
27 Kwa maana nyote mliobatizwa katika Kristo, mmemvaa Kristo.

Warumi 8:15
15 Hamkupewa Roho anayewafanya kuwa tena watumwa wa hofu. Lakini mmepokea Roho anayewafanya kuwa wana. Na kwa Roho huyo tunaweza kumwita Mungu, “Abba! Baba!”

2 Wakorintho 3:18
18 Na sisi sote ambao nyuso zetu hazikufunikwa tunaonyesha, kama kwenye kioo, utukufu wa Bwana. Nasi tunabadilishwa tufanane naye, kutoka utukufu hadi utukufu wa juu zaidi, ambao unatoka kwa Bwana ambaye ni Roho.

1 Wakorintho 3:16-17
16 Je, hamjui kwamba ninyi ni Hekalu la Mungu, na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? 17 Kama mtu ye yote akiliharibu Hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa sababu Hekalu la Mungu ni takatifu, na ninyi ni Hekalu hilo.

Yohana 6:63
63Roho wa Mungu ndiye anayetoa uzima, uwezo wa mwanadamu haufai kitu. Maneno haya ni Roho na ni uzima.

 

 
 

 

The Guide has her own Guidebook to help her lead and guide the lesson.

Download Swahili Lesson #2 Swahili Guidebook

Download Swahili Guidebook Bible Verses Lesson #2

Download Swahili Lesson #2 Student Study Book

Mistari ya Biblia

 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us