Project Hope     home >> stonecroft>>roho mtakatifu yuko wapi?>>somo la nne>> mistari ya biblia
Roho Mtakatifu yuko wapi? - Somo la Nne #4 - Mistari ya Biblia
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

Somo la 4

Nawezaje kuwa mkristo nizaae matunda?

Kitabu mwongozo

Mistari ya Biblia

Kujisomea biblia katika Juma

1 Wakorintho 13:1-13
Kama ningekuwa na uwezo wa kusema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa kama kelele ya kengele au toazi. 2 Na kama nina uwezo wa unabii, na kuelewa siri zote na maarifa yote; na hata kama nina imani kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu. 3 Kama nikitoa mali yote niliyo nayo, na kama nikitoa mwili wangu uchomwe moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.

4 Upendo huvumilia, upendo hufadhili; upendo hauna wivu au majivuno.
5 Upendo hauna kiburi na haukosi kuwa na adabu. Upendo hau tafuti kujipendeza nafsi; haukasiriki upesi, hauweki orodha ya mabaya. 6 Upendo haufurahii mabaya, bali hufurahia kweli. 7 Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahim ili yote.
8 Upendo hauna mwisho. Lakini penye unabii, utakoma; zikiwepo lugha zitakoma; yakiwepo maarifa yatakwisha. 9 Kwa maana tunafa hamu kwa sehemu na tunafanya unabii kwa sehemu. 10 Lakini uka milifu utakapokuja, yale yasiyo kamili yatakwisha. 11 Nilipokuwa mtoto mdogo, nilisema kama mtoto mdogo, niliwaza kama mtoto mdogo, nilifikiri kama mtoto mdogo. Nilipokuwa mtu mzima niliacha mambo ya kitoto. 12 Kwa maana sasa tunaona sura kama ya kwenye kioo, lakini wakati huo tutaona uso kwa uso. Sasa nafahamu kwa sehemu, wakati huo nitafahamu kikamilifu, kama vile ninavyo faha mika kikamilifu.

13 Basi sasa, mambo matatu yanadumu: imani, tumaini na upendo. Lakini lililo kuu kati ya haya ni upendo.

Warumi 8:1-8
Kwa hiyo basi, sasa hakuna tena hukumu kwa wale walio ndani ya Kristo Yesu. 2 Kwa maana sheria ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu imeniweka huru kutokana na sheria ya dhambi na mauti. 3 Mungu amefanya lile ambalo sheria ilishindwa kufanya kwa sababu ya udhaifu wa mwili wetu wa asili. Mungu aliihukumu dhambi kwa kumtuma Mwana wake wa pekee katika hali ya mwili kama sisi, ili awe sadaka kwa ajili ya dhambi. 4 Kwa kufanya hivyo, Mungu ametutimizia matakwa ya haki ya sheria kwa kuwa sasa maisha yetu yanaongozwa na Roho na wala hatuishi tena kwa kufuata mata kwa ya mwili.

5 Kwa maana wale waishio kwa kuongozwa na asili yao ya dhambi, hukaza mawazo yao kwenye mambo ya mwili; bali wale waishio kwa kuongozwa na Roho hukaza mawazo yao katika mambo ya Roho. 6 Matokeo ya mawazo yaliyotawaliwa na tamaa za mwili ni kifo lakini mawazo yaliyotawaliwa na Roho huleta uzima na amani. 7 Watu wenye mawazo yaliyotawaliwa na mambo ya mwili ni adui wa Mungu. Watu kama hao hawakubali kutii sheria ya Mungu, na kwa kweli hawawezi. 8 Watu wanaotawaliwa na mwili, hawawezi kum pendeza Mungu .

Warumi 8:9-17
9 Lakini ninyi hamuishi kwa kufuata matakwa ya mwili, bali mnaongozwa na Roho; ikiwa kweli Roho wa Mungu anaishi ndani yenu. Mtu ye yote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo. 10 Lakini kama Kristo anaishi ndani yenu, ingawa miili yenu imekufa kwa sababu ya dhambi, roho zenu zinaishi kwa sababu mmek wisha kuhesabiwa haki. 11 Na ikiwa Roho wa Mungu ambaye alimfu fua Yesu kutoka kwa wafu anaishi ndani yenu, Mungu aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataipatia uzima miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya huyo Roho wake ambaye anaishi ndani yenu. 12 Kwa hiyo ndugu zangu, hatuwajibiki tena kuishi kama miili yetu inavyotaka. 13 Kwa maana mkiishi kama mwili unavyotaka mta kufa,lakini kama mkiangamiza matendo ya mwili kwa nguvu ya Roho, mtaishi.

14 Kwa maana wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu ni wana wa Mungu.15 Hamkupewa Roho anayewafanya kuwa tena watumwa wa hofu. Lakini mmepokea Roho anayewafanya kuwa wana. Na kwa Roho huyo tunaweza kumwita Mungu, “Abba! Baba!” 16 Ni Roho mwenyewe anayeshuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi ni wana wa Mungu. 17 Na ikiwa sisi ni wana, basi tu warithi. Sisi ni warithi wa Mungu tutakaorithi pamoja na Kristo iwapo tutateseka pamoja naye ili pia tutukuzwe pamoja naye.

1 Wakorintho 12:1-11
Sasa kuhusu karama za Roho Mtakatifu ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu. 2 Mnajua kwamba mlipokuwa hamumjui Mungu mlivutwa na kupotoshwa na sanamu bubu.

3 Kwa hiyo napenda mfahamu ya kuwa hakuna mtu anayeongozwa na Roho wa Mungu anayeweza kusema, “Yesu alaaniwe.” Pia hakuna mtu awezaye kukiri, “Yesu ni Bwana,” isipokuwa ameongozwa na Roho Mtakatifu. 4 Basi kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni mmoja. 5 Pia kuna huduma za aina mbalimbali, lakini Bwana ni mmoja. 6 Kisha kuna aina tofauti za kutenda kazi, lakini ni Mungu yule yule anayeongoza kazi zote kwa kila mtu.7 Roho Mtakatifu hudhi hirishwa kwa kila mtu kwa faida ya wote. 8 Maana mtu mmoja hupewa neno la hekima na huyo Roho, na mwingine hupewa neno la ufahamu kutoka kwa Roho huyo huyo. 9 Mtu mwingine hupewa imani na huyo Roho na mwingine karama za kuponya. 10 Huyo huyo Roho humpa mwingine uwezo wa kufanya miujiza, mwin gine unabii, mwingine uwezo wa kutofautisha kati ya roho mbalim bali, mwingine aina za lugha na mwingine uwezo wa kutafsiri lugha. 11 Lakini ni Roho huyo huyo mmoja anayefanya haya yote, naye hugawa karama kwa kila mtu, kama yeye mwenyewe apendavyo.

1 Yohana 4:7-21
7 Wapendwa, tupendane, kwa sababu upendo hutoka kwa Mungu. Mtu mwenye upendo amezaliwa na Mungu na anamjua Mungu. 8 Mtu asiye na upendo hamjui Mungu; kwa maana Mungu ni upendo. 9 Na hivi ndivyo Mungu alivyoonyesha upendo wake kwetu: alimtuma Mwana wake wa pekee ulimwenguni ili kwa ajili yake sisi tupate kwa kupitia kwake. 10 Na huu ndio upendo: si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi hata akamtuma Mwanae awe sadaka ya kulipia dhambi zetu.11 Wapendwa, kwa kuwa Mungu ali tupenda kiasi hicho, sisi pia tunapaswa kupendana. 12 Hakuna mtu aliyepata kumwona Mungu; lakini tukipendana, Mungu anaishi ndani yetu, na upendo wake unakamilika ndani yetu. 13 Tunajua ya kwamba tunaishi ndani yake na yeye anaishi ndani yetu kwa sababu ametupatia Roho wake. 14 Na sisi tumeona na kushuhudia kwamba Baba amemtuma Mwanae awe mwokozi wa ulim wengu. 15 Kila mtu anayekiri kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, na yeye hukaa ndani ya Mungu. 16 Kwa hiyo tunajua na kutegemea upendo alio nao Mungu kwetu sisi. Mungu ni upendo, na mtu mwenye upendo hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake. 17 Upendo unakamilishwa ndani yetu ili tuwe na uja siri siku ile ya hukumu; kwa maana hata katika ulimwengu huu sisi tunaishi kama yeye. 18 Katika upendo hakuna woga; upendo ulioka milika hufukuza woga wote, kwa sababu woga hutokana na adhabu. Mtu mwenye woga hajakamilishwa katika upendo. 19 Tunapenda kwa sababu yeye alitupenda kwanza.

20 Mtu akisema, “Nampenda Mungu,” na huku anamchukia ndugu yake, huyo ni mwongo. Kwa maana mtu asipompenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hajamwona. 21 Na Mungu mwenyewe ametupa amri hii kwamba, mtu anayempenda Mungu hana budi kumpenda pia na ndugu yake.

Wagalatia 5:16-26
16 Kwa hiyo nasema, mruhusuni Roho atawale maisha yenu na msitafute kutimiza tamaa za mwili. 17 Kwa maana tamaa za mwili hushindana na Roho; na Roho hushindana na tamaa za mwili. Roho na mwili hupingana, na kwa sababu hiyo ninyi hamwezi kufanya yale mnayotaka. 18 Lakini kama mkiongozwa na Roho, hamko tena chini ya sheria.

19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: uasherati, uchafu, ufisadi,20 kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, mafarakano, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha waonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama haya, hawataurithi Ufalme wa Mungu. 22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumili vu, wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi. Hakuna sheria inayopinga mambo kama haya.

24 Wote walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na tamaa zake.25 Kwa kuwa tunaishi kwa kuongozwa na Roho wa Mungu, basi tufuate uongozi wake. 26 Tusiwe watu wenye maji vuno, tusichokozane na wala tusioneane wivu. Kuchukuliana Mizigo

1 Yohana 1: 9
9 Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwa minifu na wa haki na atatusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote.

1. Wagalatia 5: 22-23
22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumili vu, wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi. Hakuna sheria inayopinga mambo kama haya.

1 Wakorintho 13:13
13 Basi sasa, mambo matatu yanadumu: imani, tumaini na upendo. Lakini lililo kuu kati ya haya ni upendo.

Matayo 22: 34-40
34 Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazi sha Masadukayo, walikutana wakamjia pamoja. 35 Mmoja wao, mtaalamu wa sheria akajaribu kumtega kwa kumwuliza, 36 “Mwali mu, ni amri ipi iliyo kuu kuliko zote?” 37 Yesu akamjibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’ 38 Hii ndio amri kuu, tena ni ya kwanza. 39 Na ya pili inafanana nayo, nayo ni hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ 40 Amri hizi mbili ndio msingi wa sheria zote na Maandiko ya manabii.”

3, Walosai 3:19
19 Ninyi waume, wapendeni wake zenu wala msiwe wakali juu yao.

Luka 6:27-28
27 “Sikieni niwaambie, wapendeni adui zenu. Watendeeni mema wanaowachukia. 28 Wabarikini wanaowalaani, waombeeni mema wanaowaumiza.

Tito 2:3-4
3 Hali kadhalika akina mama wazee wawe na mwenendo wa unyenyekevu. Wasiwe wachonganishi, wala wasiwe watumwa wa pombe; bali waonyeshe mfano mwema. 4 Hivyo wawafundishe akina mama vijana kuwapenda waume zao na watoto wao

Yohana 13:34-35
34 Nina waachia amri mpya: pendaneni ninyi kwa ninyi. Kama mimi nilivy owapenda, na ninyi mpendane vivyo hivyo. 35 Kama mkipendana hivyo, watu wote watafahamu ya kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.”

Mathayo 22:39
39 Na ya pili inafanana nayo, nayo ni hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’

Waefeso 5:2
2 Muishi maisha ya upendo kama Kristo alivyotupenda sisi akajitoa kwa ajili yetu kuwa sadaka yenye harufu nzuri na dhabihu kwa Mungu.

Warumi 12:9-10
9 Upendo wenu uwe wa kweli. Chukieni uovu, mshikilie yaliyo mema.10 Pendaneni ninyi kwa ninyi kwa upendo wa kindugu. Waheshimuni wengine kuliko mnavyojiheshimu wenyewe.

Warumi 5:5
5 Tukiwa na tumaini hatuwezi kukata tamaa kwa sababu Mungu amekwisha kumimina upendo wake mioyoni mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye ni zawadi tuliyopewa na Mungu.

Wafilipi 4:4
4 Furahini katika Bwana siku zote, tena nasema furahini!

Wafilipi 4:6-7
6 Msifadhaike juu ya jambo lo lote; lakini katika kila jambo mjulisheni Mungu haja zenu, kwa kusali na kuomba pamoja na kushu kuru 7 Na amani ya Mungu, ambayo inapita ufahamu wote, italinda mioyo yenu na nia zenu kwa Kristo Yesu.

Yohana 14: 27
27 Ninawaachia amani. Nawapeni amani yangu; amani hii ulimwengu hauwezi kuwapa. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.

4. Warumi 15:5
5 Na Mungu aliye chanzo cha subira na faraja awajalie ninyi moyo wa umoja miongoni mwenu mnapomfuata Kristo Yesu,

5. Wakolosai 3:12
12 Basi, kwa kuwa ninyi ni wateule wa Mungu, wapendwa na watakatifu, vaeni moyo wa huruma, wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.

6. Waefeso 2:10
10 Kwa maana sisi ni matokeo ya kazi ya Mungu tulioumbwa katika Kristo Yesu, ili tuwe na matendo mema ambayo Mungu alikwisha andaa, tuishi katika hayo.

Luka 16:10-12
10 “Mtu ambaye ni mwaminifu katika mambo madogo, atakuwa mwaminifu hata katika mambo makubwa; na mtu ambaye si mwaminifu katika mambo madogo hatakuwa mwaminifu katika mambo makubwa. 11 Na ikiwa hamkuwa waaminifu katika kutunza mali ya dunia hii, ni nani atakayewaamini awakabidhi mali ya kweli? 12 Na kama ham kuwa waaminifu na mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa mali yenu wenyewe?

2 Wathesalonike 3:3
3 Lakini Bwana ni mwaminifu. Ata waimarisheni na kuwalinda kutokana na yule mwovu.

7. Wafilipi 2:3-8
3 Msifanye jambo lo lote kwa ajili ya ubinafsi au kwa kujiona, bali kuweni wanyenyekevu, mkiwahesabu wengine kuwa bora kuliko ninyi.
4 Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu ajishughulishe pia kwa faida ya wengine. 5 Muwe na nia kama ile aliyokuwa nayo Kristo Yesu; 6 yeye kwa asili alikuwa sawa na Mungu, lakini hakuona kwamba kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kush ikilia sana. 7 Bali alikubali kuacha vyote, akachukua hali ya mtumishi, akazaliwa na umbo la wanadamu. 8 Alipochukua umbo la mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii mpaka kufa, tena kifo cha msalaba.

Tito 2:11-12
11 Kwa maana neema ya Mungu iletayo wokovu imedhihirishwa kwa watu wote. 12 Neema hiyo inatufundisha kukataa uovu na tamaa za dhambi, tupate kuishi maisha ya kiasi, ya haki na ya kumcha Mungu, katika ulimwengu huu. Wakati huo huo.

1 Wakorintho 12:11
11 Lakini ni Roho huyo huyo mmoja anayefanya haya yote, naye hugawa karama kwa kila mtu, kama yeye mwenyewe apendavyo.

1 Wakorintho 12:11
11 Lakini ni Roho huyo huyo mmoja anayefanya haya yote, naye hugawa karama kwa kila mtu, kama yeye mwenyewe apendavyo.

8. 1 Petro 4:10
10 Kila mmoja na atumie kipawa alichopewa kuwahudumia wengine, kama mawakili waaminifu wa neema mbalimbali za Mungu.

9. 1 Wakorintho 12:8-10
8 Maana mtu mmoja hupewa neno la hekima na huyo Roho, na mwingine hupewa neno la ufahamu kutoka kwa Roho huyo huyo. 9 Mtu mwingine hupewa imani na huyo Roho na mwingine karama za kuponya. 10 Huyo huyo Roho humpa mwingine uwezo wa kufanya miujiza, mwin gine unabii, mwingine uwezo wa kutofautisha kati ya roho mbalim bali, mwingine aina za lugha na mwingine uwezo wa kutafsiri lugha.

Wafilipi 1:11
11 Maisha yenu yawe na matunda ya haki yatokayo kwa Yesu Kristo, ili Mungu apewe utukufu na sifa.

Warumi 12: 6-8
6 Tumepewa vipawa tofauti kulingana na neema tuliy opokea kutoka kwa Mungu. Kama mtu ana kipawa cha kutoa unabii basi akitumie kulingana na imani yake. 7 Kama kipawa chake ni kuwahudumia wengine, basi awahudumie. Kama ni kufundisha, basi na afundishe. 8 Kama kipawa chake ni kuwatia moyo wengine, na afanye hivyo. Kama ni ukarimu, basi na atoe kwa moyo. Mwenye kipawa cha uongozi na afanye hivyo kwa bidii. Mwenye kipawa cha huruma na aonyeshe huruma yake kwa furaha.

 

 
 

The Guide has her own Guidebook to help her lead and guide the lesson.

Download Swahili Lesson #4 Guidebook

Download Swahili Guidebook Bible Verses Lesson #4

Download Swahili Lesson #4 Student Study Book

Mistari ya Biblia

 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us