Project Hope     home >> stonecroft>>roho mtakatifu yuko wapi?>>somo la sita>> mistari ya biblia
Roho Mtakatifu yuko wapi? - Somo la Sita #6 - Mistari ya Biblia
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

Somo 6

Kufurahia uwepo wa Mungu

Kitabu mwongozo

Mistari ya Biblia

Kujisomea Biblia kwa Juma

Warumi 7:14 – 25
14 Tunafahamu kwamba sheria ni ya kiroho. Lakini mimi si wa kiroho; mimi nimeuzwa utumwani, ni mtumwa wa dhambi. 15 Sielewi nitendalo: kwa maana lile ninalotaka kulifanya, sifanyi; badala yake, ninafanya lile ambalo nachukia kulifanya. 16 Kwa hiyo kama ninafanya lile nisilopenda kufanya, hii ina maana kwamba nakubali kuwa sheria ni njema. 17 Basi, kwa kweli si mimi hasa nitendaye lile nisilolipenda bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. 18 Kwa maana ninafahamu kwamba hakuna wema wo wote ndani yangu mimi, yaani katika mwili wangu wa asili. Ingawa nina nia ya kutenda lililo jema, lakini ninashindwa kulitenda. 19 Sitendi lile jema nipendalo bali lile ovu nisilopenda, ndilo nitendalo. 20 Basi kama ninafanya lile nisilopenda kufanya, si mimi tena nifanyaye hivyo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
21 Kwa hiyo imekuwa kama ni sheria: kila ninapotaka kufanya jambo jema, jambo ovu hujitokeza. 22 Kwa maana ndani yangu ninaifurahia sheria ya Mungu. 23 Lakini ninaona kuna sheria nyin gine mwilini mwangu inayopingana na ile sheria ninayoikubali akilini mwangu. Sheria hii inanifanya kuwa mateka wa sheria ya dhambi ambayo inafanya kazi mwilini mwangu.

24 Ole wangu, mimi mnyonge! Ni nani atakayeniokoa na huu mwili wa kifo?

25 Ninamshukuru Mungu kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo! Kwa hiyo basi, mimi kwa moyo wangu, ninaitumikia sheria ya Mungu, lakini kwa mwili wangu wa asili ninaitumikia sheria ya dhambi.

Warumi 8:1-17
1Kwa hiyo basi, sasa hakuna tena hukumu kwa wale walio ndani ya Kristo Yesu. 2 Kwa maana sheria ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu imeniweka huru kutokana na sheria ya dhambi na mauti. 3 Mungu amefanya lile ambalo sheria ilishindwa kufanya kwa sababu ya udhaifu wa mwili wetu wa asili. Mungu aliihukumu dhambi kwa kumtuma Mwana wake wa pekee katika hali ya mwili kama sisi, ili awe sadaka kwa ajili ya dhambi. 4 Kwa kufanya hivyo, Mungu ametutimizia matakwa ya haki ya sheria kwa kuwa sasa maisha yetu yanaongozwa na Roho na wala hatuishi tena kwa kufuata mata kwa ya mwili.

5 Kwa maana wale waishio kwa kuongozwa na asili yao ya dhambi, hukaza mawazo yao kwenye mambo ya mwili; bali wale waishio kwa kuongozwa na Roho hukaza mawazo yao katika mambo ya Roho. 6 Matokeo ya mawazo yaliyotawaliwa na tamaa za mwili ni kifo lakini mawazo yaliyotawaliwa na Roho huleta uzima na amani. 7 Watu wenye mawazo yaliyotawaliwa na mambo ya mwili ni adui wa Mungu. Watu kama hao hawakubali kutii sheria ya Mungu, na kwa kweli hawawezi. 8 Watu wanaotawaliwa na mwili, hawawezi kum pendeza Mungu .

9 Lakini ninyi hamuishi kwa kufuata matakwa ya mwili, bali mnaongozwa na Roho; ikiwa kweli Roho wa Mungu anaishi ndani yenu. Mtu ye yote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo. 10 Lakini kama Kristo anaishi ndani yenu, ingawa miili yenu imekufa kwa sababu ya dhambi, roho zenu zinaishi kwa sababu mmek wisha kuhesabiwa haki. 11 Na ikiwa Roho wa Mungu ambaye alimfu fua Yesu kutoka kwa wafu anaishi ndani yenu, Mungu aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataipatia uzima miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya huyo Roho wake ambaye anaishi ndani yenu. 12 Kwa hiyo ndugu zangu, hatuwajibiki tena kuishi kama miili yetu inavyotaka. 13 Kwa maana mkiishi kama mwili unavyotaka mta kufa,lakini kama mkiangamiza matendo ya mwili kwa nguvu ya Roho, mtaishi.

14 Kwa maana wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu ni wana wa Mungu.15 Hamkupewa Roho anayewafanya kuwa tena watumwa wa hofu. Lakini mmepokea Roho anayewafanya kuwa wana. Na kwa Roho huyo tunaweza kumwita Mungu, “Abba! Baba!” 16 Ni Roho mwenyewe anayeshuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi ni wana wa Mungu. 17 Na ikiwa sisi ni wana, basi tu warithi. Sisi ni warithi wa Mungu tutakaorithi pamoja na Kristo iwapo tutateseka pamoja naye ili pia tutukuzwe pamoja naye.

Wakolosai 3:1-17
1 Basi, kwa kuwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, elekezeni mioyo yenu kwenye mambo ya juu, alikokaa Kristo, upande wa kulia wa Mungu.2 Yafikirini mambo ya juu na siyo mambo ya hapa duniani. 3 Kwa maana ninyi mlikufa, na uzima wenu umefichwa pamoja na Kristo kwa Mungu.4 Wakati Kristo ambaye ni uzima wetu ataonekana, ndipo na ninyi mtakapoonekana pamoja naye katika utu kufu.

5 Basi, yaangamizeni kabisa mambo yote yanayotokana na asili yenu ya kidunia: uasherati, mawazo machafu, tamaa mbaya, nia mbaya na choyo ambayo ni ibada ya sanamu.

6 Kwa sababu ya mambo haya, ghadhabu ya Mungu inakuja. 7 Ninyi mlikuwa mkitenda mambo haya katika maisha yenu ya zamani. 8 Lakini sasa ni lazima mwa chane kabisa na mambo kama haya: hasira, ghadhabu, nia mbaya, matukano na maneno machafu kutoka vinywani mwenu.

9 Msiambiane uongo kwa maana mmekwisha vua utu wenu wa zamani pamoja na matendo yake 10 na kuvaa utu upya ambao unaendelea kufanywa upya katika ufahamu ili ufanane na Muumba wake.11 Katika hali hii hakuna tena tofauti kati ya Mgiriki na Myahudi, aliyetahiriwa na asiyetahiriwa, mtu aliyesoma na asiyesoma, mtumwa na mtu huru. Bali Kristo ni yote na yumo ndani ya wote. 12 Basi, kwa kuwa ninyi ni wateule wa Mungu, wapendwa na watakatifu, vaeni moyo wa huruma, wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu. 13 Vumilianeni na kusameheana kama mtu ana malalamiko kuhusu mwenzake. Sameheni kama Bwana alivyokwisha kuwasamehe. 14 Juu ya haya yote, vaeni upendo ambao unaunganisha mambo haya kuwa kitu kimoja kilicho kikamilifu. 15 Ruhusuni amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena muwe na shukrani. 16 Neno la Kristo lidumu ndani yenu kwa wingi, mki fundisha na na kuonyana katika hekima yote; na huku mkiimba zab uri, nyimbo na tenzi za rohoni na mkiwa na shukrani kwa Mungu mioyoni mwenu. 17 Na lo lote mtakalofanya, ikiwa kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kupitia kwake.

Warumi 12:1-8
1 Kwa hiyo ndugu zangu nawasihi kwa sababu ya huruma zake Mungu, jitoeni kwake muwe sadaka hai, takatifu na inayompendeza Mungu, ambayo ndio ibada yenu ya kiroho. 2 Msiige tabia na mien endo ya dunia hii bali mbadilishwe, nia zenu zikifanywa kuwa mpya, ili mpate kuwa na hakika ni nini mapenzi ya Mungu: yaliyo mema, yanayopendeza machoni pake na makamilifu.

3 Kwa sababu ya neema niliyopewa nawaambia kila mmoja wenu: Msijifikirie kuwa watu wa juu kuliko mlivyo. Badala yake, muwe na kiasi katika mawazo yenu, kila mmoja wenu ajipime kutokana na kiasi cha imani aliyopewa na Mungu. 4 Kama vile ambavyo kila mmoja wenu ana mwili mmoja wenye viungo vingi, na kila kiungo kina kazi yake, 5 hali kadhalika, ndani ya Kristo sisi tulio wengi tunakuwa mwili mmoja na kila mmoja wetu ni sehemu ya we ngine wote. 6 Tumepewa vipawa tofauti kulingana na neema tuliy opokea kutoka kwa Mungu.

Warumi 12:9-21
9 Upendo wenu uwe wa kweli. Chukieni uovu, mshikilie yaliyo mema.10 Pendaneni ninyi kwa ninyi kwa upendo wa kindugu. Waheshimuni wengine kuliko mnavyojiheshimu wenyewe. 11 Juhudi yenu isipungue, moto wenu wa kiroho uendelee kuwaka mkimtumikia Mungu. 12 Muwe na furaha katika tumaini lenu, na katika dhiki muwe na subira. Ombeni wakati wote.13 Wasaidieni watu wa Mungu walio na shida. Muwe wakarimu kwa matendo.
14 Waombeeni baraka za Mungu wanaowatesa. Wabarikini wala msiwalaani.15 Furahini pamoja na wenye furaha; huzunikeni pamoja na wenye huzuni.16 Muishi kwa amani ninyi kwa ninyi. Msitake makuu bali muwe tayari kushirikiana na wanyonge. Kamwe msiwe watu wenye majivuno.

17 Msimlipe mtu uovu kwa uovu. Jitahidini kutenda yaliyo mema machoni pa watu wote. 18 Kama ikiwezekana, kaeni kwa amani na watu wote.19 Wapendwa, msijilipizie kisasi, bali mtoe nafasi kwa ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa:“Kisasi ni juu yangu; Mimi nitalipa, asema Bwana.20 Badala yake, adui yakoakiwa na njaa, mpe chakula; akiwa na kiu, mpe kitu anywe. Maana ukifanya hivyo, utampalia mkaa wa moto kichwani pake.21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

Warumi 15:1-13
1 Sisi tulio imara katika imani, hatuna budi kuchukuliana na udhaifu wa wale ambao si imara. Tusitafute kujipendeza wenyewe. 2 Kila mmoja wetu anapaswa kumpendeza jirani yake ili kumjenga katika imani. 3 Kwa maana hata Kristo hakujipendeza mwenyewe bali alikuwa kama ilivyoandikwa: “Matusi yote waliyoku tukana wewe yalinipata mimi.” 4 Kwa maana mambo hayo yaliyoan dikwa zamani, yaliandikwa kutufundisha, ili tukiwa na subira na faraja tunayopata katika Maandiko tuwe na tumaini.

5 Na Mungu aliye chanzo cha subira na faraja awajalie ninyi moyo wa umoja miongoni mwenu mnapomfuata Kristo Yesu, 6 ili kwa pamoja na kwa sauti moja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.

7 Mpokeane ninyi kwa ninyi kama Kristo alivyowapokea, ili Mungu apate kutukuzwa. 8 Maana nawaambia kwamba, Kristo alikuwa mtumishi kwa Waisraeli ili kuonyesha kuwa Mungu ni mwaminifu,na kuthibitisha ahadi alizowapa baba zetu. 9 Na pia ili watu wa mataifa mengine wamtukuze Mungu kwa huruma yake. Kama yasemavyo Maandiko: “Kwa sababu hii nitakutukuza kati ya watu wa mataifa, nitaimba nyimbo za kulisifu jina lako.” 10 Na tena yanasema, “Ninyi watu wa mataifa, furahini pamoja na watu wa Mungu.”

11 Na tena: “Msifuni Bwana enyi watu wote wa mataifa, watu wote wamsifu.” 12 Na tena Isaya anasema:“Shina la Yese lita chipuka, atatoka huko atakayetawala mataifa yote; na watu wa ma taifa watamtumaini.”

13 Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha na amani katika kumwamini, ili kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, mpate kuwa na tumaini tele.

3. Yohana 15:1 – 8
‘Mimi ni mzabibu wa kweli na Baba yangu ndiye mkulima. 2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda, Baba yangu hulikata; na kila tawi lizaalo, yeye hulisafisha ili lipate kuzaa matunda zaidi. 3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya mafundisho nili yowapa. 4 Kaeni ndani yangu nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa matunda pasipo kuwa sehemu ya mzabibu, vivyo hivyo, ninyi msipokaa ndani yangu hamwezi kufanya lo lote. 5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi; anayekaa ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa matunda mengi sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya lo lote. 6 Mtu asipokaa ndani yangu hutupwa nje kama tawi na kunyauka. Matawi hayo hukusanywa na kutupwa motoni, yakateketea. 7 Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lo lote mtakalo nanyi mtatendewa. 8 Mnapozaa matunda kwa wingi Baba yangu anatukuzwa, na hivyo mnadhihirisha kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.

Kumzuia Roho Mtakatifu

5. Matendo 7:51
51 “Ninyi watu wenye shingo ngumu! Wenye mioyo ya kipagani! Mmekuwa viziwi kwa neno la Mungu wala hamchoki kumpinga Roho Mta katifu! Kama walivyofanya baba zetu nanyi leo mnafanya vivyo hivyo.

I Watessalonike 5:19-20
19 Msiuzime moto wa Roho Mtakatifu; 20 msidharau unabii.

Isaya 63:10
Lakini waliasi na kumhuzunisha Roho Mtakatifu
Na akageuka kuwa adui yao, na akapigana nao.
Angalizo-Eneo hili linatueleza Mungu alivyokuwa akihusika na Israeli ambapo hawakutambua namna Mungu livyo wajali na kuwalea.

Matendo Ya Mitume 5:3
3 Petro akamwambia, “Anania, mbona shetani ametawala moyo wako kiasi cha kukubali kumdanganya Roho Mtakatifu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata?

6. Wafilipi 4:6-7
6 Msifadhaike juu ya jambo lo lote; lakini katika kila jambo mjulisheni Mungu haja zenu, kwa kusali na kuomba pamoja na kushu kuru 7 Na amani ya Mungu, ambayo inapita ufahamu wote, italinda mioyo yenu na nia zenu kwa Kristo Yesu.

Warumi 2:15
15 Kwa jinsi hii matendo yao yanaonyesha kwamba yale yaliyoagizwa katika she ria ya Musa yameandikwa ndani ya mioyo yao. Dhamiri zao pia hush uhudia hivyo; kwa maana mawazo yao mara nyingine huwashtaki na mara nyingine huwatetea.

1 Samweli 10:17
Na iwe hivyo, hizo ishara zitakapo kujilia, na ufanye hivyo kwa kuhitaji,kwa kuwa Mungu yu pamoja nawe.

2 Timotheo 3:16
16 Andiko zima lina pumzi ya Mungu nalo lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kuwaongoza na kuwafundisha katika haki

7. 1 Yohana 3:1
Tazameni jinsi Baba alivyotupenda mno, hata tukaitwa watoto wa Mungu! Na hivyo ndivyo tulivyo. Watu wa ulimwengu hawatutambui kwa sababu hawakumjua Mungu.

Yohana 15:15
15 Siwaiti ninyi watumishi tena kwa sababu mtumishi haelewi shughuli za bwana wake; bali nimewaita rafiki, kwa maana mambo yote niliyoyasikia kutoka kwa Baba yangu nimewa fahamisha.

Wafilipi 3:20-21
20 Lakini uraia wetu uko mbinguni. Nasi tunangoja kwa hamu Mwokozi kutoka huko, yaani Bwana wetu Yesu Kristo, 21 ambaye, kwa uwezo unaomwezesha kutawala kila kitu, atabadilisha miili yetu midhaifu ili iwe na utukufu kama alionao yeye.

Waefeso 3:12
12 ambaye tukiwa ndani yake, tuna ujasiri na uhakika wa kumkaribia Mungu kwa njia ya imani katika Kristo.

1 Wakorintho 6:19-20
19 Hamjui kwamba miili yenu ni Hekalu la Roho Mtakatifu anayekaa ndani yenu, ambaye mme pewa na Mungu? Ninyi si mali yenu wenyewe; 20 mmenunuliwa kwa bei kubwa. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu.

8. b. Waefeso 6:10-18
10Hatimaye, muwe imara katika Bwana na katika nguvu zake kuu. 11 Vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kusimama na kupin gana na hila zote za shetani. 12 Kwa maana hatupambani na bina damu, bali tunapambana na tawala na mamlaka na nguvu za ulimwengu huu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13 Kwa hiyo, vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kusimama imara siku ya uovu itakapokuja; na mkishafanya yote, mtakuwa bado mme simama. 14 Kwa hiyo simameni imara mkisha jifunga na kweli kama mkanda kiunoni na haki kama kinga ya kifuani; 15 na kuvaa Injili ya amani kama viatu miguuni, ili muweze kusimama barabara.16 Zaidi ya haya yote, jivikeni imani kama ngao ambayo itawawe zesha kuzuia mishale yenye miale ya moto kutoka kwa yule mwovu. 17 Vaeni wokovu kama kofia ya vita vichwani na chukueni upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu. 18 Ombeni wakati wote katika Roho, katika sala zote na maombi. Kwa hiyo muwe macho na siku zote endeleeni kuwaombea watu wote wa Mungu.

9. Yakobo 4:7-8
7 Kwa hiyo, jinyenyekezeni kwa Mungu . Mpingeni shetani, naye atawakimbia. 8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia. Takaseni mikono yenu, ninyi wenye dhambi; na takaseni mioyo yenu, ninyi wenye nia mbili.

1 Petro 5: 8-10
8 Kaeni macho. Kesheni, maana adui yenu Ibilisi, huzunguka- zunguka akinguruma kama simba, akitafuta mtu atakayemmeza. 9 Mpingeni, mkiwa thabiti katika imani, mkifahamu kwamba ndugu zenu pote duniani wanapatwa na mateso hayo hayo. 10 Na mkisha kuteseka kitambo kidogo, Mungu wa neema yote ambaye amewaita katika utukufu wake wa milele katika Kristo, yeye mwenyewe atawa kamilisheni na kuwathibitisha na kuwatia nguvu.

Waefeso 6:13
13 Kwa hiyo, vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kusimama imara siku ya uovu itakapokuja; na mkishafanya yote, mtakuwa bado mme simama.

Waefeso 4:22-27
22 Vueni maisha yenu ya zamani muweke kando hali yenu ya asili ambayo huharibiwa na tamaa potovu.23 Nia zenu zifanywe upya 24 na mvae utu upya ulioumbwa kwa mfano wa Mungu katika haki na utakatifu. 25 Kwa hiyo, kila mmoja wenu aache kusema uongo, na amwambie ndugu yake ukweli, kwa maana sisi sote ni viungo vya mwili mmoja.
26Mkikasirika, msitende dhambi; msikubali kukaa na hasira kutwa nzima 27 na kumpa she tani nafasi.

10. 2 Wakorintho 10:3-5
3 Ingawa tunaishi duniani lakini hatupigani kama watu wa ulimwengu. 4 Silaha zetu si za kidunia, bali silaha zetu zina nguvu ya kimungu iwezayo kubomoa ngome.5 Tunaharibu hoja na mabishano yaliyo kinyume cha kumjua Mungu. Tunateka mawazo yote na kuyafanya yamtii Kristo,

2 Wakorintho 6:7
7 katika maneno ya kweli na katika uwezo wa Mungu; kwa silaha za haki mkono wa kulia na mkono wa kushoto;

Waefeso 6:17
17 Vaeni wokovu kama kofia ya vita vichwani na chukueni upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu.

Zaburi 50:15
Niite wakati wa taabu, Ntakuokoa, na utanisifu.

1 Yohana 4:4
4 Lakini ninyi watoto wapendwa, ni wa Mungu, nanyi mmekwisha kuwashinda; kwa maana yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yule aliyeko duniani.

11. 2 Petro 3:18
18 lakini kukua katika neema na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo

Wagalatia 5:16
16 Kwa hiyo nasema, mruhusuni Roho atawale maisha yenu na msitafute kutimiza tamaa za mwili.

 
 

The Guide has her own Guidebook to help her lead and guide the lesson.

Download Swahili Lesson #6 Guidebook

Download Swahili Guidebook Bible Verses Lesson #6

Download Swahili Lesson #6 Student Study Book

Mistari ya Biblia

 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us