Project Hope     home >> stonecroft>>roho mtakatifu yuko wapi?>>somo la tano>> mistari ya biblia
Roho Mtakatifu yuko wapi? - Somo la Tano #5- Mistari ya Biblia
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

Somo la 5

Kuishi katika nguvu za Roho mtatifu

Kitabu mwongozo

Mistari ya Biblia

Kujisomea Biblia kwa Juma

Wagalatia 5:16-26
16 Kwa hiyo nasema, mruhusuni Roho atawale maisha yenu na msitafute kutimiza tamaa za mwili. 17 Kwa maana tamaa za mwili hushindana na Roho; na Roho hushindana na tamaa za mwili. Roho na mwili hupingana, na kwa sababu hiyo ninyi hamwezi kufanya yale mnayotaka. 18 Lakini kama mkiongozwa na Roho, hamko tena chini ya sheria. 19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: uasherati, uchafu, ufisadi,20 kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, mafarakano, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha waonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama haya, hawataurithi Ufalme wa Mungu. 22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumili vu, wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi. Hakuna sheria inayopinga mambo kama haya.

24 Wote walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na tamaa zake.25 Kwa kuwa tunaishi kwa kuongozwa na Roho wa Mungu, basi tufuate uongozi wake. 26 Tusiwe watu wenye maji vuno, tusichokozane na wala tusioneane wivu. Kuchukuliana Mizigo

Warumi 6:1-11
Tusemeje basi? Tuendelee kutenda dhambi ili neema izidi kuongezeka?2 Hata kidogo! Itawezekanaje sisi tuliokufa kwa mambo ya dhambi, tuendelee tena kuishi humo? 3 Au hamfahamu kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika kifo chake? 4 Kwa hiyo tulikufa na kuzikwa naye kwa njia ya ubatizo ili kama vile Kristo alivyofufuliwa kutoka kwa wafu kwa nguvu na utukufu wa Baba, sisi pia tupate kuishi maisha mapya. 5 Kwa maana ikiwa tumeunganika naye katika kifo chake, basi tutaunganika naye katika kufufuka kwake. 6 Tunafahamu kwamba mwili wetu wa asili ulisulubiwa msalabani pamoja na Kristo ili mwili wetu wa dhambi uharibiwe kabisa na tusiwe tena watumwa wa dhambi.
7 Kwa maana mtu anapokufa anakuwa huru na mambo ya dhambi. 8 Lakini ikiwa tumekufa na Kristo, tunaamini kwamba pia tutaishi pamoja naye.

9 Kama tujuavyo, Kristo alikwisha kufufu liwa kutoka kwa wafu kwa hiyo hafi tena; kifo hakina mamlaka juu yake tena. 10 Alikufa kwa ajili ya dhambi mara moja tu, lakini maisha anayoishi anamwishia Mungu.

11 Kwa hiyo ninyi pia hamna budi kujihesabu kuwa wafu kwa mambo ya dhambi bali hai kwa Mungu mkiwa ndani ya Kristo Yesu.

Warumi 6:12-19
12 Basi, msiruhusu dhambi itawale ndani ya miili yenu, ambayo ni ya muda, iwafanye mzifuate tamaa za mwili. 13 Msiku bali kutoa sehemu yo yote ya miili yenu itumike kama vyombo vya uovu kutenda dhambi. Bali jitoeni kwa Mungu kama watu waliotolewa kutoka katika kifo wakaingizwa uzimani. Pia toeni sehemu zote za miili yenu zitumike kama vyombo vya haki. 14 Kwa maana dhambi haitakuwa na mamlaka juu yenu kwa sababu hamtawaliwi na sheria bali mnatawaliwa na neema. Watumwa Wa Haki

15 Tufanyeje basi? Tuendelee kutenda dhambi kwa kuwa hatutawa liwi na sheria bali tuko chini ya neema? La , sivyo! 16 Hamfahamu kuwa kama mkijitoa kumtumikia mtu na kumtii kama watumwa basi mnakuwa watumwa wa huyo mnayemtii? Mnaweza kuwa watumwa wa dhambi ambayo matokeo yake ni mauti au mnaweza kuwa watumwa wa utii ambao huleta haki.17 Lakini Mungu ashukuriwe kwa kuwa ninyi ambao mlikuwa watumwa wa dhambi mmetii kwa moyo wote mafundi sho mliyopewa. 18 Mmewekwa huru, mbali na dhambi na mmekuwa watumwa wa haki. 19 Ninatumia mifano ya kibinadamu kwa sababu ya upungufu wenu wa hali ya asili. Kama mlivyokuwa mkiitoa miili yenu kwa ajili ya mambo ya uchafu na uovu uliokuwa ukiongezeka zaidi na zaidi, sasa itoeni miili yenu itumike kwa ajili ya haki na utakatifu.

Warumi 6:20-23
20 Mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa hamtawaliwi na haki. 21 Lakini mlipata faida gani kwa mambo hayo ambayo sasa mnayaonea aibu? Mwisho wa mambo hayo ni kifo. 22 Lakini sasa kwa kuwa mmewekwa huru kutokana na dhambi na mmekuwa watumwa wa Mungu, faida mnayopata ni utakaso, na hatimaye, uzima wa milele. 23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Warumi 8:1-8
1 Kwa hiyo basi, sasa hakuna tena hukumu kwa wale walio ndani ya Kristo Yesu.
2 Kwa maana sheria ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu imeniweka huru kutokana na sheria ya dhambi na mauti. 3 Mungu amefanya lile ambalo sheria ilishindwa kufanya kwa sababu ya udhaifu wa mwili wetu wa asili. Mungu aliihukumu dhambi kwa kumtuma Mwana wake wa pekee katika hali ya mwili kama sisi, ili awe sadaka kwa ajili ya dhambi. 4 Kwa kufanya hivyo, Mungu ametutimizia matakwa ya haki ya sheria kwa kuwa sasa maisha yetu yanaongozwa na Roho na wala hatuishi tena kwa kufuata mata kwa ya mwili.

5 Kwa maana wale waishio kwa kuongozwa na asili yao ya dhambi, hukaza mawazo yao kwenye mambo ya mwili; bali wale waishio kwa kuongozwa na Roho hukaza mawazo yao katika mambo ya Roho. 6 Matokeo ya mawazo yaliyotawaliwa na tamaa za mwili ni kifo lakini mawazo yaliyotawaliwa na Roho huleta uzima na amani. 7 Watu wenye mawazo yaliyotawaliwa na mambo ya mwili ni adui wa Mungu. Watu kama hao hawakubali kutii sheria ya Mungu, na kwa kweli hawawezi. 8 Watu wanaotawaliwa na mwili, hawawezi kum pendeza Mungu .

Warumi 8:9-17
9 Lakini ninyi hamuishi kwa kufuata matakwa ya mwili, bali mnaongozwa na Roho; ikiwa kweli Roho wa Mungu anaishi ndani yenu. Mtu ye yote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo. 10 Lakini kama Kristo anaishi ndani yenu, ingawa miili yenu imekufa kwa sababu ya dhambi, roho zenu zinaishi kwa sababu mmek wisha kuhesabiwa haki. 11 Na ikiwa Roho wa Mungu ambaye alimfu fua Yesu kutoka kwa wafu anaishi ndani yenu, Mungu aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataipatia uzima miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya huyo Roho wake ambaye anaishi ndani yenu. 12 Kwa hiyo ndugu zangu, hatuwajibiki tena kuishi kama miili yetu inavyotaka. 13 Kwa maana mkiishi kama mwili unavyotaka mta kufa,lakini kama mkiangamiza matendo ya mwili kwa nguvu ya Roho, mtaishi.

14 Kwa maana wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu ni wana wa Mungu.15 Hamkupewa Roho anayewafanya kuwa tena watumwa wa hofu. Lakini mmepokea Roho anayewafanya kuwa wana. Na kwa Roho huyo tunaweza kumwita Mungu, “Abba! Baba!” 16 Ni Roho mwenyewe anayeshuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi ni wana wa Mungu.
17 Na ikiwa sisi ni wana, basi tu warithi. Sisi ni warithi wa Mungu tutakaorithi pamoja na Kristo iwapo tutateseka pamoja naye ili pia tutukuzwe pamoja naye.

2. Waefeso 1:18-20
18 Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yaangaziwe ili mpate kujua tumaini mliloitiwa, na mtambue utajiri wa urithi wa utukufu wake kwa watu wa Mungu; 19 na muu fahamu uweza wake usiopimika ambao ametupa sisi tunaoamini. Uweza huo ni sawa na ile nguvu kuu 20 ambayo aliitumia alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, akamweka akae mkono wake wa kulia katika enzi yake mbinguni.

2 Wakorintho 13:4
4 Kwa maana alisu lubiwa katika udhaifu, lakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Hali kadhalika sisi ni wadhaifu ndani yake, lakini kwa nguvu za Mungu tutaishi pamoja naye ili tuweze kuwahudumia.

Waefeso 2:10
10 Kwa maana sisi ni matokeo ya kazi ya Mungu tulioumbwa katika Kristo Yesu, ili tuwe na matendo mema ambayo Mungu alikwisha andaa, tuishi katika hayo.

3. Waefeso 5:18-20
18 Pia msilewe divai, kwa sababu huo ni upotovu, bali mjazwe Roho. 19 Zungumzeni ninyi kwa ninyi kwa zaburi na nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia Mungu mioyoni mwenu kwa sauti tamu. 20 Wakati wote na kwa kila kitu mshukuruni Mungu Baba katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

1 Wakorintho 3: 1-3
1Lakini ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama watu wa kiroho, bali kama watu wa mwili, na kama watoto wachanga katika Kristo.2 Niliwalisha maziwa, sio chakula kigumu; kwa kuwa mli kuwa hamjawa tayari kukipokea. 3 Kwa maana ninyi bado mnatawaliwa na mambo ya mwili. Je, wakati kuna wivu na kugombana kati yenu, ninyi si watu wa mwili wenye tabia kama za watu wa kawaida?

Matendo Ya Mitume 9: 17; 20
17 Anania akaenda, akaingia mle nyumbani. Akaweka mikono yake juu ya Sauli akasema, “Ndugu yangu Sauli, Bwana Yesu aliyekutokea njiani ame nituma kwako ili upate kuona tena na ujazwe Roho Mtakatifu.”

20 bila kukawia akaenda katika sinagogi akawash uhudia watu kwamba, “Yesu ni Mwana wa Mungu.”

4. Warumi 6:19
19 Ninatumia mifano ya kibinadamu kwa sababu ya upungufu wenu wa hali ya asili. Kama mlivyokuwa mkiitoa miili yenu kwa ajili ya mambo ya uchafu na uovu uliokuwa ukiongezeka zaidi na zaidi, sasa itoeni miili yenu itumike kwa ajili ya haki na utakatifu.

Warumi 12:1
1 Kwa hiyo ndugu zangu nawasihi kwa sababu ya huruma zake Mungu, jitoeni kwake muwe sadaka hai, takatifu na inayompendeza Mungu, ambayo ndio ibada yenu ya kiroho.

1 Petro 4:19
19.Basi wale wanaoteswa kufuatana na mapenzi ya Mungu, wajikabidhi kwa Muumba wao aliye mwaminifu.

Warumi 12:2
2 Msiige tabia na mien endo ya dunia hii bali mbadilishwe, nia zenu zikifanywa kuwa mpya, ili mpate kuwa na hakika ni nini mapenzi ya Mungu: yaliyo mema, yanayopendeza machoni pake na makamilifu.

Warumi 8:1-5
1 Kwa hiyo basi, sasa hakuna tena hukumu kwa wale walio ndani ya Kristo Yesu. 2 Kwa maana sheria ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu imeniweka huru kutokana na sheria ya dhambi na mauti. 3 Mungu amefanya lile ambalo sheria ilishindwa kufanya kwa sababu ya udhaifu wa mwili wetu wa asili. Mungu aliihukumu dhambi kwa kumtuma Mwana wake wa pekee katika hali ya mwili kama sisi, ili awe sadaka kwa ajili ya dhambi. 4 Kwa kufanya hivyo, Mungu ametutimizia matakwa ya haki ya sheria kwa kuwa sasa maisha yetu yanaongozwa na Roho na wala hatuishi tena kwa kufuata mata kwa ya mwili.

 
 

 

The Guide has her own Guidebook to help her lead and guide the lesson.

Download Swahili Lesson #5 Guidebook

Download Swahili Guidebook Bible Verses Lesson #5

Download Swahili Lesson #5 Student Study Book

Mistari ya Biblia

 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us