Project Hope     home >> stonecroft>>roho mtakatifu yuko wapi?>>somo la tatu>> mistari ya biblia
Roho Mtakatifu yuko wapi? - Somo la Tatu #3 - Mistari ya Biblia
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

Somo 3

Je Roho mtakatifu anaweza kunisadia kukua?

Kitabu mwongozo

Mistari ya Biblia

Kujisomea Biblia kwa Juma

Yohana 14:1-14
Yesu akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia. 2 Katika nyumba ya baba yangu mna nafasi nyingi. Kama sivyo, nisingeliwaambia kwamba nakwenda kuwaandalia makao. 3 Na nikishawaandalia, nitarudi kuwachukua mkae pamoja nami; ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo. 4 Ninyi mnajua njia ya kufikia ninakokwenda.”5 Tomaso akamwuliza, “Bwana, hatujui unakokwenda; tutaijuaje njia?”6 Yesu akawaam bia, “Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu. 7 Kama mngekuwa mnajua mimi ni nani, mngemfahamu na Baba yangu. Tangu sasa mnamfahamu Baba yangu na mmemwona.”

8 Filipo akamwambia Yesu, “Bwana, tuonyeshe Baba yako nasi tutaridhika.”9 Yesu akamjibu, “Filipo, imekuwaje hunifahamu baada ya mimi kuwa pamoja nanyi muda wote huu? Mtu ye yote ambaye ameniona mimi, amemwona Baba. Sasa inakuwaje unasema, ‘Tuonyeshe Baba’? 10 Je, huamini ya kuwa mimi niko ndani ya Baba yangu, na Baba yangu yuko ndani yangu? Mambo ninayowaambia siyasemi kwa mamlaka yangu mwenyewe, bali yanatoka kwa Baba yangu ambaye anaishi ndani yangu, na ndiye anayetenda haya yote. 11 Niaminini ninapowaambia ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu na Baba yangu yu ndani yangu. La sivyo, niaminini kwa sababu ya haya mambo ninayotenda. 12 Ninawaambia hakika, mtu ye yote akiniamini ataweza kufanya miujiza kama hii na hata zaidi, kwa kuwa mimi ninakwenda kwa Baba yangu. 13 Kitu cho chote mtakachoomba kwa jina langu, nitawafanyia, ili Baba yangu apate kutukuzwa kwa yale ambayo mimi Mwanae nitawafanyia. 14 Mkiniomba cho chote kwa jina langu nitawafanyia.”

Yohana 14:15-31
15 “Kama mnanipenda mtatimiza amri zangu. 16 Nami nitam womba Baba, naye atawapeni Msaidizi mwingine akae nanyi siku zote. 17 Huyo ndiye Roho wa Kweli ambaye watu wasioamini hawawezi kumpokea. Watu kama hao hawamwoni wala hawamfahamu. Ninyi mnamfahamu kwa kuwa anakaa ndani yenu na ataendelea kuwa nanyi. 18 Sitawaacha kama yatima. Nitarudi kwenu. 19 Baada ya muda mfupi watu wa ulimwengu hawataniona tena, ila ninyi mta niona; na kwa kuwa mimi ni hai, ninyi pia mtakuwa hai.

20 Wakati huo utakapofika mtajua ya kuwa mimi niko ndani ya Baba yangu na ninyi mko ndani yangu. 21 Mtu anayezishika amri zangu na kuziti miza ndiye anayenipenda. Na mtu anayenipenda, Baba yangu atam penda; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.” 22 Yuda, siyo Iskariote, akamwuliza, “Bwana, itakuwaje ujidhihirishe kwetu tu na si kwa ulimwengu mzima?”23 Yesu akamjibu, “Mtu akinipenda atashika mafundisho yangu na Baba yangu atampenda, nasi tutafanya makao yetu kwake. 24 Mtu asiyenipenda hayashiki mafundisho yangu na mafundisho niliyowapeni si yangu bali yametoka kwa Baba yangu aliyenituma.

25 “Nimewaambia mambo haya wakati nikiwa bado nipo nanyi. 26 Lakini yule Msaidizi, yaani Roho Mtakatifu, ambaye Baba yangu atamtuma kwenu kwa jina langu, atawafundisha mambo yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. 27 Ninawaachia amani. Nawapeni amani yangu; amani hii ulimwengu hauwezi kuwapa. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.28 Kumbukeni nilivyowaambia, ‘Ninakwenda, na nitarudi.’ Kama kweli mngalinipenda mngefurahi, kwa kuwa nakwenda kwa Baba; na Baba yangu ni mkuu kuliko mimi. 29 Na sasa nimewaambia mambo haya kabla hayajatokea ili yataka potokea mpate kuamini. 30 Sitasema tena mengi nanyi kwa sababu mtawala wa dunia hii anakuja. Yeye hana uwezo juu yangu. 31 Lakini ninatii amri ya Baba ili ulimwengu upate kujua kwamba nampenda Baba. Simameni tuondoke hapa.’ ’

Yohana 15:1-17
‘Mimi ni mzabibu wa kweli na Baba yangu ndiye mkulima. 2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda, Baba yangu hulikata; na kila tawi lizaalo, yeye hulisafisha ili lipate kuzaa matunda zaidi. 3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya mafundisho nili yowapa. 4 Kaeni ndani yangu nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa matunda pasipo kuwa sehemu ya mzabibu, vivyo hivyo, ninyi msipokaa ndani yangu hamwezi kufanya lo lote. 5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi; anayekaa ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa matunda mengi sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya lo lote. 6 Mtu asipokaa ndani yangu hutupwa nje kama tawi na kunyauka. Matawi hayo hukusanywa na kutupwa motoni, yakateketea. 7 Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lo lote mtakalo nanyi mtatendewa. 8 Mnapozaa matunda kwa wingi Baba yangu anatukuzwa, na hivyo mnadhihirisha kuwa ninyi ni wanafunzi wangu. 9 “Kama Baba alivyonipenda mimi, hivyo ndivyo mimi nilivy owapenda ninyi; dumuni katika pendo langu. 10 Mkizishika amri zangu mtakaa ndani ya pendo langu kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.

11 “Nimewaambia haya kusudi furaha yangu iwe ndani yenu, nanyi mpate kuwa na furaha iliyokamilika.

12 “Amri yangu ni hii: pendaneni kama nilivyowapenda. 13 Hakuna mtu mwenye upendo unaozidi ule wa mtu anayejitoa afe kwa ajili ya rafiki zake.14 Ninyi ni rafiki zangu ikiwa mtafa nya ninayowaagiza. 15 Siwaiti ninyi watumishi tena kwa sababu mtumishi haelewi shughuli za bwana wake; bali nimewaita rafiki, kwa maana mambo yote niliyoyasikia kutoka kwa Baba yangu nimewa fahamisha. 16 Hamkunichagua, bali mimi nimewachagua ninyi na nimewatuma mwende mkazae matunda, na matunda yenu yapate kudumu, ili lo lote mtakalomwomba Baba katika jina langu, awatimizie. 17 Hii ndio amri yangu: pendaneni.

Yohana 15:18-27
18 “Kama ulimwengu ukiwachukia, fahamuni kwamba ulinichukia mimi kabla haujawachukia ninyi. 19 Kama mngekuwa watu wa ulim wengu huu, ulimwengu ungeliwapenda. Ulimwengu unawachukia kwa sababu ninyi si wa ulimwengu huu na mimi nimewachagua kutoka katika ulimwengu.

20 “Kumbukeni lile neno nililowaambia, ‘Hakuna mtumishi aliye mkuu kuliko bwana wake.’ Kama wamenitesa mimi na ninyi pia watawatesa; kama wamelishika neno langu na neno lenu watalishika pia. 21 Lakini yote haya watawatendea kwa ajili yangu kwa sababu hawamfahamu Baba yangu ambaye amenituma. 22 Kama sikuja na kusema nao wasingalikuwa na hatia. Lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi zao. 23 Mtu ye yote anayenichukia mimi anamchukia na Baba yangu. 24 Kama nilikuwa sikuwafanyia miujiza ambayo haijapata kufanywa na mtu mwingine ye yote, wasingalikuwa na hatia ya dhambi. Lakini wameona miujiza hii na bado wakatuchukia mimi na Baba yangu. 25 “Hali hii imetokea kama ilivyoandikwa katika Sheria kwamba, ‘Walinichukia pasipo sababu.’ 26 Lakini atakapokuja yule Msaidizi nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, yaani yule Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia mimi. 27 Na ninyi pia ni mashahidi wangu kwa maana tangu mwanzo mmekuwa pamoja nami.”

Yohana 16:1-15
Nimewaambia mambo haya yote ili msipoteze imani mtakapokutana na matatizo. 2 Watu watawafukuza mtoke katika masinagogi[a] na msirudi humo tena. Hakika, unakuja wakati watapofikiri kuwa kwa kuwaua ninyi watakuwa wanatoa huduma kwa Mungu. 3 Watafanya hivyo kwa sababu hawajamjua Baba, na hawajanijua mimi pia. 4 Nimewaambia haya sasa ili kuwaandaa. Hivyo wakati wa mambo haya kutimia utakapofika, mtakumbuka kwamba niliwapa tahadhari mapema.

Kazi za Roho Mtakatifu
Sikuwaambia mambo haya tangu mwanzo, kwa sababu bado nilikuwa pamoja nanyi. 5 Sasa narudi kwake yeye aliyenituma, ingawa hakuna hata mmoja wenu anayeniuliza, ‘Unakwenda wapi?’ 6 Nanyi mmejawa na huzuni kwa vile nimewaambia mambo haya yote. 7 Hakika nawaambieni, ni kwa faida yenu mimi nikiondoka. Nasema hivi kwa sababu, nitakapoondoka nitamtuma kwenu Msaidizi. Lakini nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja.

8 Ila huyo Msaidizi atakapokuja, atawaonesha watu wa ulimwengu jinsi walivyofanya dhambi. Atawaonesha nani ana hatia ya dhambi, nani ana haki mbele za Mungu, na nani anastahili kuhukumiwa na Mungu. 9 Huyo Msaidizi atawaonesha kuwa wana hatia ya dhambi kwa sababu hawaniamini mimi. 10 Atawaonesha jinsi wasivyoelewa mtu anavyohesabiwa haki na Mungu. Hakika mimi nina kibali kwa sababu naenda kwa Baba nanyi hamtaniona tena. 11 Naye atawaonesha watu wa ulimwengu huu jinsi hukumu yao isivyo sahihi, kwa sababu mkuu wao ulimwenguni[b] amekwisha hukumiwa.

12 Ninayo mambo mengi ya kuwaeleza, lakini ni magumu kwenu kuyapokea kwa sasa. 13 Hata hivyo atakapokuja huyo Roho wa kweli, Yeye atawaongoza hadi kwenye kweli yote. Hatasema maneno yake mwenyewe bali atayasema yale tu anayosikia na atawajulisha yale yatakayotokea baadaye. 14 Roho wa kweli atanipa mimi utukufu kwa kuwaeleza ninyi yote aliyopokea kutoka kwangu. 15 Yote aliyonayo Baba ni yangu pia. Ndiyo sababu nilisema kwamba Roho atawaeleza yote anayopokea kutoka kwangu.

Yohana 16:16-33

Huzuni Itageuzwa Kuwa Furaha

16 Baada ya kipindi kifupi hamtaniona. Kisha baada ya kipindi kingine kifupi mtaniona tena.”

17 Baadhi ya wafuasi wake wakaambiana wao kwa wao, “Ana maana gani anaposema, ‘Baada ya kipindi kifupi hamtaniona tena. Kisha baada ya kipindi kifupi kingine mtaniona tena?’ Tena ana maana gani anaposema, ‘Kwa sababu naenda kwa Baba’?” 18 Wakauliza pia, “Ana maana gani anaposema ‘Kipindi kifupi’? Sisi hatuelewi anayosema.” 19 Yesu alitambua kuwa wafuasi wake walitaka kumwuliza juu ya jambo hilo. Hivyo akawaambia, “Je, mnaulizana ninyi kwa ninyi kwamba nilikuwa na maana gani niliposema, ‘Baada ya kipindi kifupi hamtaniona. Kisha baada ya kipindi kifupi kingine mtaniona tena’? 20 Hakika nawaambia, ninyi mtapata huzuni na kulia, bali ulimwengu utakuwa na furaha. Ndio, mtapata huzuni, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha.

21 Mwanamke anapojifungua mtoto, hupata maumivu, kwa sababu wakati wake umefika. Lakini baada ya mtoto kuzaliwa, huyasahau maumivu yale. Husahau kwa sababu huwa na furaha kwa kuwa mtoto amezaliwa ulimwenguni. 22 Ndivyo ilivyo hata kwenu pia. Sasa mna huzuni lakini nitawaona tena, nanyi mtafurahi. Mtakuwa na furaha ambayo hakuna mtu atakayewaondolea. 23 Katika siku hiyo, hamtapaswa kuniuliza mimi kitu chochote. Nami kwa hakika nawaambia, Baba yangu atawapa lo lote mtakalomwomba kwa jina langu. 24 Hamjawahi kuomba lo lote kwa namna hii hapo awali. Bali ombeni kwa jina langu nanyi mtapewa. Kisha mtakuwa na furaha iliyotimia ndani yenu.

Ushindi Dhidi ya Ulimwengu

25 Nimewaambia mambo haya kwa kutumia maneno yenye mafumbo. Isipokuwa utakuja wakati ambapo sitatumia tena maneno ya jinsi hiyo kuwaeleza mambo. Nami nitasema nanyi kwa maneno ya wazi wazi juu ya Baba. 26 Kisha, mtaweza kumwomba Baba vitu kwa jina langu. Sisemi kwamba nitapaswa kumwomba Baba kwa ajili yenu. 27 Baba mwenyewe anawapenda kwa sababu ninyi mmenipenda mimi. Naye anawapenda kwa sababu mmeamini kwamba nimetoka kwa Mungu. 28 Mimi nimetoka kwa Baba kuja ulimwenguni. Sasa naondoka ulimwenguni na kurudi kwa Baba.”

29 Kisha wafuasi wake wakasema, “Tayari unaongea nasi wazi wazi. Hutumii tena maneno yanayoficha maana. 30 Sasa tunatambua kuwa unajua mambo yote. Wewe unajibu maswali yetu hata kabla hatujayauliza. Hii inatufanya tuamini kwamba ulitoka kwa Mungu.”

31 Yesu akasema, “Kwa hiyo sasa mnaamini? 32 Basi nisikilizeni! Wakati unakuja mtakapotawanywa, kila mmoja nyumbani kwake. Kwa hakika, wakati huo tayari umekwisha fika. Ninyi mtaniacha, nami nitabaki peke yangu. Lakini kamwe mimi siko peke yangu, kwa sababu Baba yupo pamoja nami.

33 Nimewaambia mambo haya ili muwe na amani ndani yangu. Katika ulimwengu huu mtapata mateso. Lakini muwe jasiri! Mimi nimeushinda ulimwengu!”

1. a. 1 Yohana 2:27
27 Lakini yule Roho Mtakatifu mliyempokea anakaa ndani yenu wala hamhitaji mtu kuwafundisha. Lakini kama vile huyo Roho Mtakatifu anavyowafundisha mambo yote, naye ni wa kweli wala si wa uongo; kama alivyowafundisha, dumuni ndani yake.

b. Yohana 16:13-14
13 Akija yule Roho wa kweli atawaongoza muijue kweli yote. Yeye hatanena kwa uwezo wake mwenyewe bali atanena yote atakayosikia. Atawafundisha kuhusu mambo yote yajayo. 14 Atanitukuza mimi, kwa maana atayachukua yaliyo yangu na kuwaambia ninyi.

c. Warumi 8:14
14 Kwa maana wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu ni wana wa Mungu.

d. Wagalatia 5:22-23
22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumili vu, wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi. Hakuna sheria inayopinga mambo kama haya

e. Matendo 1:8
8 Lakini mtapokea nguvu akishawajilia Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu na Yudea yote na Samaria, hadi mwisho wa dunia.”

Marko 1: 35
35 Kesho yake alfajiri, kabla hapajapambazuka, Yesu akaamka akaenda mahali pa faragha, akaomba.

2. Warumi 8:26
26 Hali kadhalika Roho hutusaidia katika udhaifu wetu. Kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu usioelezeka kwa maneno.

1 Yohana 5: 14-15
14 Na sisi tunao ujasiri huu mbele za Mungu kwamba, tukiomba cho chote sawa na mapenzi yake, atatusikia.15 Na tukijua kwamba anatusikia kwa lo lote tunaloomba basi tuna hakika kwamba tumekwisha pata yale tuliyomwomba.

3. a. 1 Tessalonike 5:17
17 ombeni pasipo kukoma,

4. a. Mathayo 6:5-6
5 “Na mnaposali, msiwe kama wanafiki; maana wao wanapenda kusimama na kusali katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu. Nawaambieni kweli, wao wamekwisha kupata tuzo yao. 6 Unaposali, nenda chumbani kwako ufunge mlango na umwombe Baba yako aliye sirini. Na Baba yako aonaye sirini atakupa tha wabu.

b. Zaburi 55:17
Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua,Naye ataisikia sauti yangu.

1 Wakorintho 1: 18
18 Kwa maana ujumbe wa msalaba ni upuuzi kwa watu wanaopo tea. Lakini kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.

Utiifu

6. Yakobo 1:22-25
22 Basi muwe watendaji wa neno na wala msiwe wasikilizaji tu, ambao wanajidanganya wenyewe. 23 Kwa maana kama mtu ni msi kilizaji tu wa neno na wala hatekelezi alilosikia, atafanana na mtu ajitazamaye uso wake katika kioo, 24 na baada ya kujiona alivyo, huenda zake na mara moja husahau anavyofanana. 25 Lakini mtu anayeangalia kwa makini katika sheria kamilifu, ile sheria iletayo uhuru, na akaendelea kufanya hivyo bila kusahau alichosi kia, bali akakitekeleza, atabarikiwa katika kile anachofanya.

Wagalatia 5:17
17 Kwa maana tamaa za mwili hushindana na Roho; na Roho hushindana na tamaa za mwili. Roho na mwili hupingana, na kwa sababu hiyo ninyi hamwezi kufanya yale mnayotaka.

1 Wakorintho 10:13
13 Hakuna jaribu lo lote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Na Mungu ni mwaminifu; hata- ruhusu mjaribiwe kupita uwezo wenu. Lakini mnapojaribiwa atawapa na njia ya kutokea ili mweze kustahimili.

7. Waefeso 4:25-32
25 Kwa hiyo, kila mmoja wenu aache kusema uongo, na amwambie ndugu yake ukweli, kwa maana sisi sote ni viungo vya mwili mmoja. 26 Mkikasirika, msitende dhambi; msikubali kukaa na hasira kutwa nzima 27 na kumpa she tani nafasi. 28 Mwizi asiibe tena, bali afanye kazi halali kwa mikono yake ili aweze kuwa na kitu cha kuwapa wenye kuhitaji msaada. 29 Msiruhusu maneno machafu yatoke vinywani mwenu, bali mazungumzo yenu yawe ya msaada katika kuwajenga wengine kufuatana na mahitaji yao, ili wale wanaowasikiliza wapate kufaidika. 30 Na msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu ambaye ni mhuri wenu wa uthibitisho kwa siku ya ukombozi. 31 Ondoeni kabisa chuki yote, ghadhabu, hasira, ugomvi na matusi, pamoja na kila aina ya uovu. 32 Muwe wema na wenye mioyo ya upendo kati yenu, na kusameheana kama Mungu alivyowasamehe kwa ajili ya Kristo. Watoto Wa Nuru.

Waefeso 4:30
30 Na msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu ambaye ni mhuri wenu wa uthibitisho kwa siku ya ukombozi.

1 Wakorintho 6:19-20
19 Hamjui kwamba miili yenu ni Hekalu la Roho Mtakatifu anayekaa ndani yenu, ambaye mme pewa na Mungu? Ninyi si mali yenu wenyewe; 20 mmenunuliwa kwa bei kubwa. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu.

8. Wagalatia 5: 16
16 Kwa hiyo nasema, mruhusuni Roho atawale maisha yenu na msitafute kutimiza tamaa za mwili.

 
 

The Guide has her own Guidebook to help her lead and guide the lesson.

Download Swahili Lesson #3 Guidebook

Download Swahili Guidebook Bible Verses Lesson #3

Download Swahili Lesson #3 Student Study Book

Mistari ya Biblia

 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us