Project Hope     uct >> stonecroft
STONECROFT:

Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

Stonecroft ni shirika la kimataifa ambalo haliko chini ya kanisa lolote.

MAELEZO YA KIUTUME YA STONECROFT:

Utume wa shirika la Stonecroft ni kuwezesha wakina mama ili nao waweze kufikia jamii kwa kupitia injili ya Yesu Kristo, Kumuinua Yesu na kuhakikisha kuwa Yesu anatukuzwa kwa kuhubiri injili ya wokovu.

MAONO YA STONECROFT:
Ni kutoa mwongozo wa kimataifa katika kuwafikia wakina mama kwa ajili ya Yesu, Stonecroft inawawezesha na kuwatia moyo wakina mama ili wamuhubiri Yesu.

Uinjilist ndilo lengo letu kuu—Msingi wa kila jitihada za huduma .Utume wetu ni kuwafikia wanawake wa kila umri, na kila kabila kwa ajili ya injili ya Yesu Kristo.

Maombi ndio msingi wa kila jambo tunalo tunalotenda, Yesu alisema ,”Pasipo mimi ,hamuwezi kufanya lolote” (Yohana 15:5).

Kumtegemea Mungu, Kutafuta mwongozo wake na Baraka,ni muhimu,uanafunzi ni nyenzo muhimu katika uinjilisti, mwanamke anakuwa mfuasi wa Yesu,wakati huo huo huduma ya Stonecroft inatoa nyenzo za kumuwezesha huyu mwanamke kukua katika imani, na baada ya hapo ili aweze kuwaongoza wengine kufuata na kuwa na mawasiliano na Yesu.

Kuwawezesha wanawake ndio msingi wa stonecroft, kuwasaidia ili waweze kugundua vipawa Mungu alivyo viweka katika maisha yao. Kuwawezesha ili wawe viongozi makini,ambao wanaleta mabadiliko katika nyumba zao, vijiji, jamii, na hata nchi zao na mwisho kabisa dunia nzima.

Lengo la stonecroft na masomo yake ya biblia ni uanafunzi na uinjilisti ,haya ni masomo rahisi ambayo mtu anaweza akajifunza katika makundi madogo dogo, ili kuwatia moyo katika ukuaji wa kiroho.

Stonecroft inahubiri injili kwa kuwafikia wanawake dunia nzima. Zaidi ya watu 25,000 ambao ni watu wa kujitolea wa Stonecroft wanafanya kazi ya kuwafikia wanawake dunia nzima.

Watu wa kujitolea katika Nchi ya marekani na nchi nyingine zaidi ya 30 wanatumia vitabu vya stonecroft,ili kuhubiri injili, kwa zaidi ya miaka 75 Stonecrift wamekuwa wakitegemea maombi katika kueneza injili.

HISTORIA YA STONECROFT:

UONGOZI WA STONECROFT:
Viongozi wa Stonecroft wanafanya majukumu yao katika ofisi ya kitaifa na hata kazi ambazo ziko mbali na hapo.

Lorraine Potter Kalal: Raisi

Lorraine Potter Kalal Huduma yake iliyo jawa na mafanikio, Pamoja na upendo wake wa Stonecroft na maono na historia, Yeye kama raisi hujiona kuwa ndie Mtumwa mkubwa, Lorrain anahitaji kuona kuwa huduma ya Stonecroft ikimtegemea Mungu ili kukamilisha mahitaji yote.

Doris Thompson: Makamu wa Raisi

Doris Thompson anawasaidia wanawake kufikia maono yao na mawazo yao katika matendo, akiwa kama makamu wa Raisi, Doris anataka kuwafikia wanawake wengi zaidi katika ulimwengu huu,na anawasaidia wanawake wengi kupitia Stonecroft,na anawasaidia wale wanao jitolea kuwafikia wengine katika maeneo mengi zaidi. Anafanya kazi ya kuibadiri Stonecroft ili iweze kuwafikia watu walio katika maeneo mapya zaidi, Pia kuna watu wengi zaidi katika uongozi ambao hamuwezi kuwa na mawasiliano nao.

Soma...

MAELEZO YA IMANI YA STONECROFT:

• Huduma ya Stonecroft inaamini katika utendaji wa kiroho, na uvuvio wa neno la Mungu, na tunaamini kuwa biblia haina kosa, inafaa kwa mafundisho na ndio yenye maamuzi ya mwisho na usemi wa mwisho.
• Tunaamini katika utatu wa Mungu – yani Mungu baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu ;

• Tunaamini katika utu wa Mungu; Utu na uungu ya Yesu (Yesu na Mungu ni Mtu mmoja, Yesu Kristo ni Mungu aliyekuwa katika mwili) aliyezaliwa kwa uweza wa Roho mtakatifu na mtu aliyekuwa bikra, yeye ni Mungu halisi na ni Mwanadamu halisi, na ni utu wa Roho mtakatifu.

• Tunaamini katika ufufuo wa Yesu kristo,—kuwa mwili wake ulifufuliwa kutoka katika wafu, sawasawa na maandiko, na pia akapaa kwenda mbinguni na kuketi katika mkono wa kuume wa Mungu baba kama wakili wa waamini.

• Tunaamini katika hali ya dhambi ya mwanadamu—kuwa kila mwanadamu anazaliwa na asili ya dhambi, na hawawezi kujiokoa wenyewe bali wanamuhitaji mkombozi ili awaokoe kutoka dhambini;

• Tunaamini katika utakaso—Kuwa Yesu alifanyika kuwa dhambi pale alipotoa dhabihu ambayo ni damu yake mwenyewe ili dunia nzima wapate msamaha wa dhambi.

• Tunaamni katia umuhimu wa kuzaliwa upya—wokovu ni kwa neema .kwa imani na sio kwa matendo,imani iokoayo itaimalisha matendo mema katika maisha yetu.

• Tunaamini katika ufufuo halisi wa mwili wa waaminio na wasio amini.

• Tunaamini katika Baraka za umilele kwa walio amini na adhabu ya milele kwa wasio amini.

• Tunaamini katika uinjilisti wa dunia nzima,—Agizo kuu la Mungu ni kuihubiri injili ya Yesu Kristo kwa watu wote wa kila rika.

• Tunaamini juu ya ujio wa mara ya ili wa Yesu sawa sawa na maandiko.

Stonecroft Ministries, Inc.

Office Location: 10561 Barkley, Suite 500,
Overland Park, KS 66212
Phone: 1.800.525.8627
FAX: 816.763.5565
E-mail: connections@stonecroft.org

 
     
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us