Project Hope     home >>vijana wa stonecroft>> yesy ni nani?
Yesy ni nani?
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

Utangulizi
YESU NI NANI? YEYE NI MTU WA AJABU SANA NA ANAISHI.

Unajua nini kuhusu yesu? Masomo haya ndio yatajadili kuhusu haya yote kama-

Kujua kuwa yesu kiuhalisia ni nani,
Kwa nini alikuja duniani,
Ujio wake una uhusiano gani na sisi, na
Pia kujjua kama tutamuona tena Yesu .

Tunafikia hatua ya kumjua mungu kupitia kile alichokifanya yesu kwetu kipindi alipokuja hapa duniani. Kuwa na uhusiano wa karibu sana na mungu, ni vizuri kwanza kujua kuhusu yesu mwenyewe. Kwa sababu hiyo inapaswa kujua kuwa yesu ni nani? Kuwa wa kwanza kusoma mpangilio huu: Yesu ni nani? Mungu yukoje? Na Roho mtakatifu yuko wapi?

Unapoendelea kujifunza kuhusu yesu, mwana wa Mungu, unaweza ukamjua yeye kwelikweli na kukubaliana na kile alichojia ulimwenguni kukileta.

Mungu akubariki sana kwa upya na ufunuo mkubwa sana ulioupata kupitia mwana wake na mwokozi wetu, Yesu Kristo.

“Lakini hizi zimeandikwa ili mmpate kuamini ya kwamba yesu ndiye kristo, mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake”
Yohana 20:31

Lucille Fern Sollenberger

Huduma
ya Stonecroft
www.stonecroft.org

Toleo la rejeo
Lucille Sollenberger,BS,M.A

Kimechapishwa na huduma ya Stonecroft
Stonecroft Ministries, Inc.
Office Location: 10561 Barkley, Suite 500,
Overland Park, KS 66212
Phone: 1.800.525.8627
FAX: 816.763.5565
E-mail: connections@stonecroft.org

JINSI YA KUJIFUNZA MASOMO YA BIBLIA KATIKA STONECROFT.

Kwa sababu hii ni shule ya biblia, lengo letu kuu ni kujifunza kile ambacho biblia inasema na jinsi gani tunaweza kutumia katika maisha yetu. Kijitabu hiki na biblia ndivyo vitakuwa vitabu vyetu ambavyo tutavitumia katika masomo yetu.

Inatakiwa tujiandae kwa somo kwa kumaliza maswali katika vijitabu vyetu hivi vya awali. Hii itatusaidia katika majadiliano yetu ya wiki kufanya kwa urahisi na kuelewa vizuri kuhusiana na somo husika kwa wakati huo. Tutajifunza somo la kwanza sote kwa pamoja.

Masomo yetu haya ya biblia yataanza katika muda muafaka na yatachukua muda wa dakika 60 mpka 90. Tutaondoka pale ambapo somo letu husika tunalolisoma litakapokuwa limefikia mwisho kwa hiyo hatutaacha kitu tutamaliza.

Kwa sababu tunatoka katika mazingira tofauti tofauti na (ukijumuishatunatoka katika makanisa tofauti tofauti) kwa hiyo tutaheshimu mawazo ya kila mtu na imani yake.
Katika wiki chache, tungependa kuanza masomo mapya ya biblia katika maeneo mapya na kwa watu wapya. Hebu fikiria mtu ambaye ungependa umwalike katika masomo haya.

Katika kitabu chako cha kusoma.

Katika kila mwisho wa somo kuna maandishi yanasomeka hivi “Vitu ninavyotaka kukumbuka kutoka katika somo”.

Kwa kuanza na somo la pili, mistari imependekezwa kwa ajili ya kusoma kipindi cha wikendi. Hii itakiusaidia wewe kujiandaa na somo husika.

Masomo mengine ya ziada ambayo yanaweza kukusaidia yapo nyuma ya hiki kitatabu. Appendices inakupa taarifa nzuri sana kuhusu tipiki ambazo zimeshasomwa katika masomo haya ya biblia. Kwa hiyo hata hapa katika ukurasa huu ni sehemu ya kuweka rekodi ya mambi yako. Kama ungependa katika kuweka nyongeza ya kusoma biblia, kwa hiyo rekodi agano jipya itakusaidia kuweka kumbukumbu katika zile sura ambazo umeshazisoma.

 
 

YESY NI NANI?

 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us