Project Hope     home >>vijana wa stonecroft>>uongozi wa stonecroft >> maelezo ya imani ya stonecroft
MAELEZO YA IMANI YA STONECROFT
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club


• Huduma ya Stonecroft inaamini katika utendaji wa kiroho,na uvuvio wa neno la Mungu,na tunaamini kuwa biblia haina kosa, inafaa kwa mafundisho na ndio yenye maamuzi ya mwisho na usemi wa mwisho.

• Tunaamini katika utatu wa Mungu – yani Mungu baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu;

• Tunaamini katika utu wa Mungu; Utu na uungu ya Yesu (Yesu na Mungu ni Mtu mmoja, Yesu Kristo ni Mungu aliyekuwa katika mwili) aliyezaliwa kwa uweza wa Roho Mtakatifu na mtu aliyekuwa bikra, yeye ni Mungu halisi na ni Mwanadamu halisi, na ni utu wa Roho mtakatifu.

• Tunaamini katika ufufuo wa Yesu kristo,—kuwa mwili wake ulifufuliwa kutoka katika wafu,sawasawa na maandiko, na pia akapaa kwenda mbinguni na kuketi katika mkono wa kuume wa Mungu baba kama wakili wa waamini.

• Tunaamini katika hali ya dhambi ya mwanadamu—kuwa kila mwanadamu anazaliwa na asili ya dhambi, na hawawezi kujiokoa wenyewe bali wanamuhitaji mkombozi ili awaokoe kutoka dhambini;

• Tunaamini katika utakaso—Kuwa Yesu alifanyika kuwa dhambi pale alipotoa dhabihu ambayo ni damu yake mwenyewe ili dunia nzima wapate msamaha wa dhambi.

• Tunaamni katia umuhimu wa kuzaliwa upya—wokovu ni kwa neema .kwa imani.na sio kwa matendo, imani iokoayo itaimalisha matendo mema katika maisha yetu.

• Tunaamini katika ufufuo halisi wa mwili wa waaminio na wasio amini.

• Tunaamini katika Baraka za umilele kwa walio amini na adhabu ya milele kwa wasio amini.

• Tunaamini katika uinjilisti wa dunia nzima,—Agizo kuu la Mungu ni kuihubiri injili ya Yesu Kristo kwa watu wote wa kila rika.

• Tunaamini juu ya ujio wa mara ya ili wa Yesu sawa sawa na maandiko.

MASOMO YA BIBLIA YA STONECROFT:

 
     
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us