Project Hope     home >> stonecroft>>roho mtakatifut
Stonecroft - Roho Mtakatifut
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

Utangulizi
JE ROHO MTAKATIFU YUKO WAPI?

Wengi wangeu elezea ukristo kama uzoefu wa Mzunguko-maisha yaliyojawa na mabonde, watue wanaofurahia kuwa na Mungu lakini wasioweza kuepuka matokeo ya kukatishwa tama,kuwa chini na wakati mgunmu na dhambi.

Jonathjan Edwards anayejulika kama mwanatheolojia mkubwa wa Marekani,alisema mafanikio ya mkristo sio mara zote kuwa katika hali nzuri ya juu, lakini ni ile hali ya kuwa na hakika kuwa Mungu yupo nyumbani, shuleni, kazini, kanisani, na jamii ambayo inafurahia kuwa wanaishi maisha ya kimungu.

Hilo ndilo jambo ambalo kujisomea biblia inaleta maana.tunataka kuwa watu tunaojua kuwa roho mtakatifu yupo katika maisha yetu kila siku, ingekuwa inawezekana kuishi maisha ya ukristo pasipo Roho mtakatifu basi Mungu asingemtuma huyu Roho kwetu, ni nguvu zake tu ambazo hutuwezesha kuishi maisha yasiyo legalega.

Hatumtumii Roho mtakatifu
bali Roho mtakatifu hututumia.

Je Roho mtakatifu yuko wapi? Anaishi na kutenda kazi katika maisha ya wale ambao wako kwa Yesu.Bwana akusaidie kufurahia uwepo wake.

Lucille Fern Sollenberger

JINSI YA KUJIFUNZA MASOMO YA BIBLIA KATIKA STONECROFT.

Kwa sababu hii ni shule ya biblia, lengo letu kuu ni kujifunza kile ambacho biblia inasema na jinsi gani tunaweza kutumia katika maisha yetu. Kijitabu hiki na biblia ndivyo vitakuwa vitabu vyetu ambavyo tutavitumia katika masomo yetu.

Inatakiwa tujiandae kwa somo kwa kumaliza maswali katika vijitabu vyetu hivi vya awali. Hii itatusaidia katika majadiliano yetu ya wiki kufanya kwa urahisi na kuelewa vizuri kuhusiana na somo husika kwa wakati huo. Tutajifunza somo la kwanza sote kwa pamoja.

Masomo yetu haya ya biblia yataanza katika muda muafaka na yatachukua muda wa dakika 60 mpka 90. Tutaondoka pale ambapo somo letu husika tunalolisoma litakapokuwa limefikia mwisho kwa hiyo hatutaacha kitu tutamaliza.

Kwa sababu tunatoka katika mazingira tofauti tofauti na (ukijumuishatunatoka katika makanisa tofauti tofauti) kwa hiyo tutaheshimu mawazo ya kila mtu na imani yake.
Katika wiki chache, tungependa kuanza masomo mapya ya biblia katika maeneo mapya na kwa watu wapya. Hebu fikiria mtu ambaye ungependa umwalike katika masomo haya.

Katika kitabu chako cha kusoma.

Katika kila mwisho wa somo kuna maandishi yanasomeka hivi “Vitu ninavyotaka kukumbuka kutoka katika somo”.

Kwa kuanza na somo la pili, mistari imependekezwa kwa ajili ya kusoma kipindi cha wikendi. Hii itakiusaidia wewe kujiandaa na somo husika.

Masomo mengine ya ziada ambayo yanaweza kukusaidia yapo nyuma ya hiki kitatabu. Appendices inakupa taarifa nzuri sana kuhusu tipiki ambazo zimeshasomwa katika masomo haya ya biblia. Kwa hiyo hata hapa katika ukurasa huu ni sehemu ya kuweka rekodi ya mambi yako. Kama ungependa katika kuweka nyongeza ya kusoma biblia, kwa hiyo rekodi agano jipya itakusaidia kuweka kumbukumbu katika zile sura ambazo umeshazisoma.

MBINU ZA KUKARIRI

1. Weka copy ya mstari unaotaka kukariri juu ya dawati, au juu ya friji, au juu ya kioo au andika kwenye kompyuta yako .
2. Soma kwa sauti kubwa kila ukiona ile copy uliyoiweka sehemu husika halafu jiulize inamaanisha nini.
3. Kariri mstari kwa maneno.
4. Weka picha akilini mwako ya kile ukisomacho.
5. Mshirikishe mwenzako yeyote mstari wa kukariri kwa kupitia email, au message, au kwa kutumia barua.
6. Mpigie simu mwenzio kwenye kundi na urudie kile ulicho kariri nay eye akirudie vivyo hivyo.

HUDUMA YA STONCROFT NI NINI?

Stoncroft ni shirika ambalo haliko chini ya kanisa lolote lile. Ambapo maono makuu ya stonecroft ni kuwawezesha akina mama ili waweze kufikia jamii kupitia injili ya Yesu Kristo. Maelfu ya watu wanaojitolea na muda mwingi wakufunzi wanakuwa pamoja ili kuwezesha huduma hii.

Stonecroft inabtoa huduma mbalimbali, ambazo zinawawezesha wanawake kukutana pamoja kwa ajli ya Mungu, kushauriana na kwa ajili nya jamii pia.
Kazi mbali mbali zinafanywa na wanawake ni zile za kijamii na masomo ya kibiblia ya Stonecroft.

Soma zaidi kuhusu stone croft na jinsi unavyoweza kuchangia kifedha tembelea katika tovuti yetu hii.
www.stonecroft.org

Below is the translated version of 'Who is the Holy Spirit?' Stonecroft's Student Study Book in Swahili, the English version of Who is the Holy Spirit? is available online from Stonecroft's website.

This transforming study will reveal who Jesus is, what He does, and what life is like when He lives within you. Learn what the Holy Spirit does in the life of a Christian and how He can help you grow to be more like Christ. (6 lessons)

 

 
 
 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us